< 1 Wafalme 20 >

1 Beni Hadadi mfalme wa Shamu akakusanya jeshi lake lote pamoja. Kulikuwa na wafalme thelathini na mbili wasaidizi pamoja naye, na magari na farasi. Akapanda, akaihusuru Samaria na kupigana nayo.
亞蘭王便‧哈達聚集他的全軍,率領三十二個王,帶着車馬上來圍攻撒馬利亞;
2 Akatuma wajumbe katika mji kwa Ahabu mfalme wa Israeli, akamwambia, “Beni Hadadi anasema hivi:
又差遣使者進城見以色列王亞哈,對他說:「便‧哈達如此說:
3 Fedha zako na dhahabu zako ni zangu. Pia wake zako na watoto, wale wazuri, sasa ni wangu.”
你的金銀都要歸我,你妻子兒女中最美的也要歸我。」
4 Mfalme wa Israeli akajibu akasema, “Na iwe kama unavyosema, bwana wangu, mfalme. Mimi pamoja na vile nilivyo navyo ni mali yako.”
以色列王回答說:「我主我王啊,可以依着你的話,我與我所有的都歸你。」
5 Wale wajumbe wakaja tena wakasema, “Beni Hadadi anasema hivi, 'Nilituma neno kwako nikisema kwamba lazima ukabidhi kwangu fedha zako, dhahabu zako, wake zako na watoto wako.
使者又來說:「便‧哈達如此說:我已差遣人去見你,要你將你的金銀、妻子、兒女都給我。
6 Lakini kesho nitatuma watumishi wangu kwako wakati kama huu, nao wataichunguza nyumba yako na nyumba za watumishi wako. Nao watatia mikononi mwao na kukichukua kila wakipendacho machoni mwao.'”
但明日約在這時候,我還要差遣臣僕到你那裏,搜查你的家和你僕人的家,將你眼中一切所喜愛的都拿了去。」
7 Ndipo mfalme wa Israeli akawaita wazee wote wa nchi pamoja akawaambia, ''Hebu angalieni jinsi huyu mtu anavyotafuta matatizo. Amenitumia ujumbe kwamba anataka kuchukua wake zangu, watoto wangu, fedha na dhahabu zangu, nami sijamkatalia.”
以色列王召了國中的長老來,對他們說:「請你們看看,這人是怎樣地謀害我,他先差遣人到我這裏來,要我的妻子、兒女,和金銀,我並沒有推辭他。」
8 Wazee wote na watu wote wakamwambia Ahabu, “Usimsikilize wala kukubaliana na matakwa yake.”
長老和百姓對王說:「不要聽從他,也不要應允他。」
9 Ahabu akawaambia wajumbe wa Beni Hadadi, “Mwambieni bwana wangu mfalme kwamba, 'Ninakubaliana na kila kitu ambacho kwanza uliwatuma watumishi wako kufanya kwangu, lakini sikubaliani na matakwa yako haya ya pili.'” Wale watumishi wa Beni Hadadi wakaondoka wakampelekea mrejesho Beni Hadadi.
故此,以色列王對便‧哈達的使者說:「你們告訴我主我王說:王頭一次差遣人向僕人所要的,僕人都依從;但這次所要的,我不能依從。」使者就去回覆便‧哈達。
10 Naye Beni Hadadi akatuma tena majibu yake kwa Ahabu, akaisema, “basi miungu inifanyie hivyo na zaidi, kama hata mavumbi ya Samaria yatawatosheleza watu watu wote wanaonifuata kuchukua kila mmoja angalau konzi mkononi mwake.”
便‧哈達又差遣人去見亞哈說:「撒馬利亞的塵土若夠跟從我的人每人捧一捧的,願神明重重地降罰與我!」
11 Naye mfalme wa Israeli akamjibu akisema, “Mwabieni Beni Hadadi, 'Hakuna abebaye silaha yake, atakayejivuna kama wakati wa kuishusha.”'
以色列王說:「你告訴他說,才頂盔貫甲的,休要像摘盔卸甲的誇口。」
12 Beni Hadadi aliusikia ujumbe huu wakati alipokuwa akinywa, yeye na wafalme walikuwa pamoja naye waliokuwa kwenye mahema yao. Beni Hadadi akayaamuru majaeshi yake, “Jipangeni katika sehemu zenu kwa ajili ya vita.” Kwa hiyo wakajiandaa kivita ili kuuvamia mji.
便‧哈達和諸王正在帳幕裏喝酒,聽見這話,就對他臣僕說:「擺隊吧!」他們就擺隊攻城。
13 Tazama, nabii akaja kwa Ahabu mfalme wa Israeli akasema, “BWANA asema, 'Je umeliona hili jeshi kubwa? Tazama, nitaliweka katika mkono wako leo, nawe utatambua kuwa mimi ni BWANA.'”
有一個先知來見以色列王亞哈,說:「耶和華如此說:『這一大群人你看見了嗎?今日我必將他們交在你手裏,你就知道我是耶和華。』」
14 Naye Ahabu akajibu, ''kwa nani? BWANA akamjibu akasema, “kwa kuwatumia viijana wanaotumikia maliwali wa wilaya.” kisha Ahabu akasema, “Ni nani atakayepewa hiyo vita?' BWANA akamwambia, “wewe.”
亞哈說:「藉着誰呢?」他回答說:「耶和華說,藉着跟從省長的少年人。」亞哈說:「要誰率領呢?」他說:「要你親自率領。」
15 Ndipo Ahabu alipowataarifu wale vijna wanaowatumikia maliwali wa wilaya. Idadi yao ilikuwa 232. Baada yao aliwahesabu wanajeshi wote, jeshi lote la Israeli; idadi yao ilikuwa elfu saba.
於是亞哈數點跟從省長的少年人,共有二百三十二名,後又數點以色列的眾兵,共有七千名。
16 Nao wakatoka wakati wa adhuhuri. Naye Beni Hadadi alikuwa akinywa na kulewa hemani mwake, yeye na wale wafalme wadogo thelathini na mbili waliokuwa wakimsaidia.
午間,他們就出城;便‧哈達和幫助他的三十二個王正在帳幕裏痛飲。
17 Wale maakida vijana waliokuwa wakiwasaidia maliwali wa wilaya walitangulia kwanza. Kisha Beni Hadadi alitaarifiwa na wanaskauti aliokuwa amewatuma kwamaba, “kuna watu wanakuja kutoka Samaria.”
跟從省長的少年人先出城;便‧哈達差遣人去探望,他們回報說:「有人從撒馬利亞出來了。」
18 Beni Hadadi akasema, “wawe wamekuja kwa amani au kwa vita, wakamteni wakiwa hai.”
他說:「他們若為講和出來,要活捉他們;若為打仗出來,也要活捉他們。」
19 Kwa hiyo wale vijvana wanaowatumikia maliwali wa wilaya wakaenda mjini na jeshi likawafuata kwa nyuma.
跟從省長的少年人出城,軍兵跟隨他們;
20 Kila mmoja akaua adui wake na wale washami wakakimbia. Israeli ikawashinda. Beni Hadadi mfalme wa Shamu akatoroka kwa farasi pamoja na wapanda farasi.
各人遇見敵人就殺。亞蘭人逃跑,以色列人追趕他們;亞蘭王便‧哈達騎着馬和馬兵一同逃跑。
21 Kisha mfalme wa Israeli akaenda akawashambulia farasi na magari, na kuwaua washami kwa mauaji makubwa.
以色列王出城攻打車馬,大大擊殺亞蘭人。
22 Yule nabii akaja kwa mfalme wa Israeli akamwambia, “Nenda, ukajiimarishe mwenyewe, uelewa na kupanga kile unachofanya, kwa sababu mwakani mfalme wa Shamu atapanda dhidi yako tena.”
那先知來見以色列王,對他說:「你當自強,留心怎樣防備;因為到明年這時候,亞蘭王必上來攻擊你。」
23 Wale watumishi wa mfalme wa Shamu wakamwambia, “Mungu wao ni mungu wa milimani. Hiyo ndiyo sababu walikuwa na nguvu kuliko tulivyokuwa. Lakini sasa hebu tupigane nao katika nchi tambarare, na kwa hakika tutakuwa na nguvu kuliko wao.
亞蘭王的臣僕對亞蘭王說:「以色列人的神是山神,所以他們勝過我們;但在平原與他們打仗,我們必定得勝。
24 Na ufanye hivi: waondoe wafalme; mwondoe kila mmoja mahali pake ukaweke majemedari mahali pao.
王當這樣行:把諸王革去,派軍長代替他們,
25 Kisha ujihesabie jeshi kama lile jeshi ulilopoteza, farasi kwa farasi na gari kwa gari, nasi tutapigana nao katika nchi tambarare. Kwa hakika tutakuwa na nguvu kuliko walivyo.” Kwa hiyo Beni Hadadi akausikiliza ushauri huo naye akafanya kama alivyoshauriwa.
又照着王喪失軍兵之數,再招募一軍,馬補馬,車補車,我們在平原與他們打仗,必定得勝。」王便聽臣僕的話去行。
26 Baada ya mwanzo wa mwaka mpya, Beni Hadadi akawahesabu Washami na akapanda Afeki kupigana na Israeli.
次年,便‧哈達果然點齊亞蘭人上亞弗去,要與以色列人打仗。
27 Watu wa Israeli walikuwa wamehesabiwa na walikuwa wamejipanga kupigana nao. Watu wa Israeli wakafanya kambi mbele yao kama makundi mawili madogo ya mbuzi, lakini Washami wakaujaza upande wa nchi.
以色列人也點齊軍兵,預備食物,迎着亞蘭人出去,對着他們安營,好像兩小群山羊羔;亞蘭人卻滿了地面。
28 Ndipo mtu wa Mungu akaja karibu akaongea mfalme wa Israeli akamwambia, “BWANA anasema: 'Kwa kuwa Washami wamesema kuwa BWANA ni mungu wa milima, na wala si mungu wa mabondeni, nitaliweka hili jeshi kubwa mkononi mwako, nawe utajua kuwa mimi ni BWANA.'”
有神人來見以色列王,說:「耶和華如此說:『亞蘭人既說我-耶和華是山神,不是平原的神,所以我必將這一大群人都交在你手中,你們就知道我是耶和華。』」
29 Kwa hiyo majeshi yakaweka kambi yakikabiliana kwa muda wa siku saba. Kisha siku ya saba vita vikaanza. Watu wa Israeli wakawaua Washami 100, 000 wanajeshi wa ardhini kwa siku moja.
以色列人與亞蘭人相對安營七日,到第七日兩軍交戰;那一日以色列人殺了亞蘭人步兵十萬,
30 Waliobaki wakakimbilia Afeki, mjini, na ule ukuta ukaanguka juu ya watu ishiriinina saba elfu waliobaki. Naye Beni Hadadi akakimbilia mjini. akaingia kwenye chumba cha ndani.
其餘的逃入亞弗城;城牆塌倒,壓死剩下的二萬七千人。 便‧哈達也逃入城,藏在嚴密的屋子裏。
31 Wale watumishi wa Beni Hadadi wakamwambia, “Tazama sasa, tumesikia kwamba wale wafalme wa nyumba ya Israeli ni wenye rehema. Tafadhali hebu tuvaeni magaunia viunoni mwetu na kamba vichwani mwetu, na twendeni kwa mfalme wa Israeli. Labda atakuokoa roho yako.”
他的臣僕對他說:「我們聽說以色列王都是仁慈的王,現在我們不如腰束麻布,頭套繩索,出去投降以色列王,或者他存留王的性命。」
32 Kwa hiyo wakavaa magunia viunoni mwao na kujifunga kamba vichwani mwao na kisha wakaenda kwa mfalme wa Israeli wakamwambia, “Mtumishi wako Beni Hadadi, anasema, 'tafadhali niachie uhai wangu.” Ahabu akawaambia, “Je, bado yuko hai? Yeye ni ndugu yangu.”
於是他們腰束麻布,頭套繩索,去見以色列王,說:「王的僕人便‧哈達說,求王存留我的性命。」亞哈說:「他還活着嗎?他是我的兄弟。」
33 Sasa wale watu walikuwa wakisikiliza ishara yeyote kutoka kwa Ahabu, kwa hiyo wakamjibu haraka, “Ndiyo ndugu yako Beni Hadadi bado yuko hai.” Ahabu akawaambia, “Nendeni mkamlete.” Ndipo Beni Hadadi alipokuja kwake, na Ahabu akamwacha aje kwenye gari lake.
這些人留心探出他的口氣來,便急忙就着他的話說:「便‧哈達是王的兄弟!」王說:「你們去請他來。」便‧哈達出來見王,王就請他上車。
34 Beni Hadadi akamwambia Ahabu, “Nitakurudishia miji yako ambayo baba yangu alichukua toka kwa baba yako, na unaweza kutengeneza masoko kwa ajili yako Dameski, kama baba yangu alivyofanya kule Samaria.” Ahabu akajibu, “Nitakuacha uende kwa agano hili.” Kwa hiyo Ahabu akafanya agano naye kisha akamwacha aende.
便‧哈達對王說:「我父從你父那裏所奪的城邑,我必歸還。你可以在大馬士革立街市,像我父在撒馬利亞所立的一樣。」亞哈說:「我照此立約,放你回去」,就與他立約,放他去了。
35 Mtu mmoja, mmoja wana wa wana wa manabii, akamwambia mmoja wa wale manabii wenzake kwa neno la BWANA, “Tafadhali nipige.” Lakini yule mtu akakataa kumpiga.
有先知的一個門徒奉耶和華的命對他的同伴說:「你打我吧!」那人不肯打他。
36 Kisha yule nabii akamwambia nabii mwenzake, “Kwa sababu umekataa kutii sauti ya BWANA, mara tu utakaponiacha, simba atakuua.” na mara tu baad ya yule mtu kumwacha, simba akamkuta na kumwua.
他就對那人說:「你既不聽從耶和華的話,你一離開我,必有獅子咬死你。」那人一離開他,果然遇見獅子,把他咬死了。
37 Kisha yule nabii akamkuta mtu mwingine akamwambia, “Tafadhali nipige.”Yule mtu akampiga na kumwumiza.
先知的門徒又遇見一個人,對他說:「你打我吧!」那人就打他,將他打傷。
38 Kisha yule nabii akaondoka akaenda kumsubiri yule mfalme barabarani; naye alikuwa amejibadilisha kwa kilemba machoni pake.
他就去了,用頭巾蒙眼,改換面目,在路旁等候王。
39 Ikawa mfalme alipokuwa akipita, Yule nabii akamwita mfalme na kumwambia, “Mtumishi wako alienda katikati ya pigano, na askari akasimama akamleta adui kwangu akasema, 'Mwangalie mtu huyu. Na ikiwa kwa vyovyote atatoroka, basi maisha yako yatatolewa kwa ajili ya maisha yake vinginevyo utalipa kilo thelathini za fedha.
王從那裏經過,他向王呼叫說:「僕人在陣上的時候,有人帶了一個人來,對我說:『你看守這人,若把他失了,你的性命必代替他的性命;不然,你必交出一他連得銀子來。』
40 Lakini kwa kuwa mtumishi wako alikuwa na mambo mengi akienda huku na kule, yule askari adui akatoroka.” Basi mfalme wa Israeli akamwambia, Hivyo ndivyo itakavyokuwa hukukmu yako - umejihukumu mwenyewe.”
僕人正在忙亂之間,那人就不見了。」以色列王對他說:「你自己定妥了,必照樣判斷你。」
41 Ndipo yule nabii alipoondoa haraka kile kilemba machoni pake, na mfalme wa Israeli alipotambua kuwa huyo alikuwa mmoja wa manabii.
他急忙除掉蒙眼的頭巾,以色列王就認出他是一個先知。
42 Yule nabii akamwambia mfalme, “BWANA anasema, 'Kwa sababu umemwachia aende mtu yule niliyekuwa nimemhukumu kifo, maisha yako yatachukua nafasi ya maisha yake.'”
他對王說:「耶和華如此說:『因你將我定要滅絕的人放去,你的命就必代替他的命,你的民也必代替他的民。』」
43 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akaenda nyumbani kwake akiwa na moyo mzito na mwenye hasira, akafika Samaria.
於是以色列王悶悶不樂地回到撒馬利亞,進了他的宮。

< 1 Wafalme 20 >