< 1 Wafalme 16 >
1 Neno la BWANA lilimjia Yehu mwana wa Hanani kinyume cha Baasha, likisema,
2 Ingawa Nilikuinua kutoka kwenye mavumbi na kukufanya kuwa kiongozi wa watu wangu Israeli, Lakini umetembea katika njia za Yeroboamu na umewafanya watu wangu Israeli kufanya dhambi, ili kunikasirisha dhidi ya dhambi zao.
3 Tazama, Nitamfagia kabisa Baasha na familia yake na nitaifanya familia yako kama familia ya Yeroboamu mwana wa Nebati.
4 Mbwa watamla yeyote ambaye anatoka kwa Baasha wanaofia mjini, na ndege wa angani watamla yeyote anayaefia shambani.”
5 Lakini kwa mambo mengine yanayohusiana na Baasha, aliyofanya, na uwezo wake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
6 Baasha akalala na mababu zake na akazikwa Tirza, na Ela mwanae akawa mfalme mahali pake.
7 Kwa kupitia nabii Yehu mwana wa Hanani neno la BWANA likaja kinyume na Baasha na familia yake, wote kwa sababu ya maovu yote aliyofanya machoni pa BWANA, akamghadhabisha kwa kazi ya mikono yake, kama familia ya Yeroboamu, na kwa sababu alikuwa ameiua familia yote ya Yeroboamu.
8 Katika mwaka wa kumi na sita wa Asa mfalme wa Yuda, Ela mwana wa Baasha akaanza kutawala juu ya Israeli kule Tirza; akatawala kwa miaka miwili.
9 Mtumishi wake Zimri, mkuu wa nusu ya magari yake akatengeneza hila dhidi yake. Wakati huo Ela alikuwa Tirza, akinywa na kulewa kwenye nyumba ya Arza, ambaye alikuwa mkuu wa watumishi wa nyumbani huko Tirza.
10 Zimri akaiingia ndani, akamshambulia na kumwua, katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, naye akawa mfalme mahali pake.
11 Zimri alipoaanza kutawala, mara tu baada ya kukaa kwenye kiti cha enzi, akawaua wanafamilia wote wa Baasha. Hakumwacha mtoto hata mmoja wa kiume, hakuna hata wa ndugu yake wala wa rafiki zake.
12 Kwa hiyo Zimri aliingamiza familia yote ya Baasha, kama alivyokuwa ameambiwa kwa neno la BWANA, ambalo lilinenwa kinyume na Baasha na nabii Yehu,
13 kwa dhambi zote za Baasha na za Ela mwanae ambazo walizifanya, ambazo kwazo waliisababisha Israeli kufanya dhambi, kiasi c ha kumghadhabisha BWANA, Mungu wa Israeli, kuzikasilikia sanamu zao.
14 Kwa mambo mengine yanayohusiana na Ela, yote ambayo alifanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
15 Katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri alitawala kwa siku saba tu kule Tirza. Jeshi likafanya kambi kule Gibethoni, ambao ni mji wa Wafilisti.
16 Lile jeshi lililokuwa limeweka kambi kule lilisikika lilksema, “Zimri amepanga njama na amemwua mfalme.” Kwa hiyo siku hiyo hapo kambini, Israeli yote ikamtangaza Omri, mkuu wa jeshi, kuwa mfalme wa Israeli.
17 Omri akapanda kutoka Gibethoni na Israeli yote pamoja naye, nao wakauhusuru Tirza.
18 Kwa hiyoZimri alipoona kuwa mji umetekwa, akaingia kwenye ngome na akaivamia ikulu ya mfalme na kulichoma moto jengo lote pamoja na yeye; kwa hiyo akafa kwa moto.
19 Hii ilikuwa ni kwa sababu ya dhambi alizofanya kwa kufanya maovu mbele ya macho ya BWANA, kwa kutembea katika njia ya Yeroboamu na katika dhambi ambazo alifanya, kiasi cha kuifanya Israeli wafanye dhambi.
20 Pia kwa mambo mengiine yanayomhusu Zimri, na fitina yake aliyofanya, je, hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
21 Sasa watu wa Israeli walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili. Nusu ya watu walimfuata Tibni mwana wa Ginathi, wakamfanya kuwa mfalme, na Nusu walimfufata Omri.
22 Lakini watu waliomfuata Omri walikuwa na nguvu kuliko wale waliomfuata Tibni mwana wa Ginathi. Kwa hiyo Tibni akafa, na Omri akawa mfalme.
23 Omri alianza kutawala juu ya Israeli katika mwaka wa thelathini na moja wa Asa mfalme wa Yuda, naye akatawala miaka kumi na miwili. Alitawala akiwa Tirza kwa miaka sita.
24 Akakinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa kilo 68 za fedha. Akajenga mji juu ya mlima na ule mji akauita Samaria, kwa sababu ya jina la Shemeri, mmiliki wa awali wa kile kilima.
25 Omri akafanya maovu mbele ya BWANA na akafanya yaliyo maovu zaidi kuliko wale waliokuwa kabla yake.
26 Kwa kuwa alitembea katika njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati na katika dhambi zake ambazo kwa hizo aliwaongoza Waisraeli kufanya dhambi, ili kumkasirisha BWANA, Mungu wa Israeli, ili kuwa na hasira juu ya sanamu zao za ubatili.
27 Kwa mambo mengine yanayomhusu Omri ambayo alfanya, na nguvu zake alizoonyesha, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
28 Kwa hiyo Omri akalala na mababu zake na akazikwa Samaria na Ahabu mwanae akawa mfalme mahali pake.
29 Katika mwaka wa thelathiini na nane wa Asa mfalme wa Yuda, Ahabu mwana wa Omri akaanza kutawala juu ya Israeli. Ahabu mwana wa Omri akatawala Israeli kule Samaria kwa miaka ishirini na mbili.
30 Ahabu mwana wa Omri akafanya yaliyo maovu mbele ya BWANA, zaidi ya wote waliokuwa kabla yake.
31 Ikawa kidogo tu Ahabu ayaendee makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, kwa hiyo akamwoa Yezebeli binti wa Ethibaali, mfalme wa Wasidoni; akaenda akamwabudu baali na akamsujudia.
32 Akamjengea madhabahu Baali, ambayo alikuwa ameijenga kule Samaria.
33 Ahabu akatengeneza Ashera. Ahabu akafanya maovu zaidi kumghadhabisha BWANA, Mungu wa Isareli, akamkasirisha kuliko wafalme wote wa Israeli waliokuwa kabla yake.
34 Katika siku zake Hieli Mbetheli aliijenga tena Yeriko. Akaijenga misingi ya mji kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, naye akayajenga malango ya mji kwa kufiwa na mwanae mdogo Segebu, na walifanya hivi kwa sababu walitii neno la BWANA, ambalo alikuwa amelinena kwa kinywa cha Joshua mwana wa Nuni.