< 1 Wafalme 15 >

1 Katika mwaka wa kumi na tano wa mfame Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya alianza kutawala juu yaYuda.
Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya akawa mfalme wa Yuda,
2 Alitawala kwa miaka mitata kule Yerusalemu. Jina la mama yake allikuwa Maaka. Alikuwa binti wa Absalomu.
naye akatawala huko Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka binti Abishalomu.
3 Naye alitembea katika dhambi zote ambazo baba yake alizifanya kabla yake; moyo wake haukuwa mkalifu kwa BWANA, Mungu wake kama moyo wa Daudi, babu yake ulivyokuwa.
Alitenda dhambi zote baba yake alizotenda kabla yake; moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana Mungu wake kama moyo wa Daudi baba yake ulivyokuwa.
4 Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi, BWANA, Mungu wake alimpa taa Yerusalemu kwa kumwinua mwanae baada yake ili kuiimarisha Yerusalemu.
Pamoja na hayo, kwa ajili ya Daudi, Bwana Mungu wake akampa taa katika Yerusalemu kwa kumwinua mwana atawale badala yake na kwa kuifanya Yerusalemu kuwa imara.
5 Mungu alifanya haya kwa sababu Daudi alifanya yaliyo mema machoni pake; wakati wote wa uhai wake, hakugeuka wala hakukosa katika yote aliyomwamuru, isipokuwa tu swala la Uria Mhiti.
Kwa kuwa Daudi alifanya yaliyo mema machoni pa Bwana na hakushindwa kushika maagizo yote ya Bwana siku zote za uhai wake, isipokuwa katika habari ya Uria, Mhiti.
6 Sasa kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Jeroboamu katika siku zote za maisha ya Abiya.
Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu wakati wote wa maisha ya Abiya.
7 Kwa mambo mengine ya Abiya, yote aliyofanya, je, hayajaandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda? Sasa kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.
Kwa habari ya matukio mengine ya utawala wa Abiya na yote aliyofanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.
8 Abiya akalala na mababu zake, nao wakamzika katika mji wa Daudi. Asa mwanae akawa mfalme mahali pake.
Naye Abiya akalala na baba zake akazikwa katika Mji wa Daudi. Asa mwanawe akawa mfalme baada yake.
9 Katika mwaka wa ishirini wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Asa akaanza kutawala Yuda.
Katika mwaka wa ishirini wa utawala wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Asa akawa mfalme wa Yuda,
10 Alitawala kwa miaka arobaini na moja kule Yerusalemu. Bibi yake alikuwa Maaka, binti wa Absalomu.
naye akatawala katika Yerusalemu miaka arobaini na mmoja. Bibi yake aliitwa Maaka binti Abishalomu.
11 Asa akafanya yaliyo mema machono mwa BWANA, kama alivyofanya Daudi, babu yake.
Asa akatenda yaliyo mema machoni mwa Bwana, kama alivyokuwa ametenda Daudi baba yake.
12 Yeye aliwafukuza kutoka katika nchi wale makahaba wa kipagani na akaziondoa sanamu zote ambazo babu zake walikuwa wametengeneza.
Akawafukuza mahanithi wa mahali pa kuabudia miungu kutoka nchi na kuondoa sanamu zote ambazo baba zake walikuwa wametengeneza.
13 Pia alimwondoa bibi yake asiwe Malkia, kwa sababu alikuwa amefanya sanamu ya kuchukiza kwa Ashera. Asa aliikata sanamu ya kuchukiza na kuiteketeza katika Bonde la Kidroni.
Hata akamwondoa bibi yake Maaka kwenye wadhifa wake kama mama malkia, kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akaikata hiyo nguzo na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni.
14 Lakini pale mahali pa juu hapakuchukuliwa. Hata hivyo. Moyo wa Asa ulikuwa mkamilifu mbele ya BWANA katika siku zake zote.
Ijapokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa Bwana kikamilifu maisha yake yote.
15 Alivirerjesha katika nyumba ya BWANA vitu vile vilivyokuwa vimetengwa kwa ajili ya BWANA, na vile vitu vyake vilivyokuwa vimetengezwa kwa fedha, na dhahabu na vyombo.
Akaleta ndani ya Hekalu la Bwana fedha na dhahabu na vile vyombo ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu.
16 Basi kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli, kwa miaka yao yote.
Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli siku zote za utawala wao.
17 Baasha mfalme wa Israeli, akaivamia na kuijenga Rama, kiasi kwamba hakumruhusu yeyote kuondoka au kuingia katika nchi ya Asa mfalme wa Yuda.
Mfalme Baasha wa Israeli akashambulia Yuda na kuweka ngome mji wa Rama ili kumzuia yeyote asitoke wala kuingia nchi ya Mfalme Asa wa Yuda.
18 Kisha Asa akazichukua zile fedha na dhahabu zilizokuwa zimebaki kwenye hazina kwenye nyumba ya BWANA, na katika hazina ya ikulu ya mfalme. Akaziweka katika mikono ya watumishi wake na kuzituma kwa Beni Hadadi mwana wa Tabrimoni mwana wa Hezioni, mfalme wa Shamu ambaye alikuwa akishi Dameski. Akamwambia,
Kisha Asa akachukua fedha yote na dhahabu iliyokuwa imeachwa katika hazina za Hekalu la Bwana na za jumba lake mwenyewe la kifalme. Akawakabidhi maafisa wake na kuwatuma kwa Ben-Hadadi mwana wa Tabrimoni, mwana wa Hezioni, mfalme wa Aramu, aliyekuwa akitawala Dameski.
19 “Naomba tufanye patano kati yangu na wewe, kama ilivyokuwa kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, Nimekutumia zawadi ya fedha na dhahabu. Ili uvunje agano lako na Baasha mfalme wa Israeli, ili kwamba aniache.”
“Akasema na pawepo mkataba kati yangu na wewe, kama ulivyokuwepo kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, nimekuletea zawadi ya fedha na dhahabu. Sasa vunja mkataba wako na Baasha mfalme wa Israeli ili aniondokee mimi.”
20 Beni Hadadi akamsikiliza mfalme Asa na kutuma wakuu wa majeshi yake, nao wakaishambulia miji ya Israeli. Wakaishambulia Ijoni, Dani, Abeliya Bethi Maaka, na Kinerothi yote, pamoja na nchi yote ya Naftali.
Ben-Hadadi akakubaliana na Mfalme Asa na kutuma majemadari wa majeshi yake dhidi ya miji ya Israeli. Akaishinda miji ya Iyoni, Dani, Abel-Beth-Maaka na Kinerethi yote, pamoja na Naftali.
21 Ikawa Baasha aliposikia haya, akaacha kuijenga Rama akarudi Tirza.
Wakati Baasha aliposikia hili, akaacha kuijenga Rama na akaenda kuishi Tirsa.
22 Kisha mfalme Asa akaitangazia Yuda yote. Hakuna aliyeachwa. Wakayabeba mawe na miti ya Rama ambayo Baasha alikuwa akijengea mji. Kisha mfalme Asa akavitumia hivyo vitu kuijenga Geba ya Benjamini na Mispa.
Kisha Mfalme Asa akatoa amri kwa Yuda yote, pasipo kumbagua hata mmoja, kubeba mawe na mbao kutoka Rama, ambazo Baasha alikuwa akitumia huko. Mfalme Asa akazitumia kujengea Geba iliyoko Benyamini na Mispa pia.
23 Mambo mengine yanyohusu utawala wa Asa, uwezo wake wote, yote aliyofanya, na miji aliyoijenga, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda? Lakini wakati wa uzee wake alipata ugonjwa wa miguu.
Kwa matukio yote ya utawala wa Asa, mafanikio yake yote, yote aliyofanya na miji aliyoijenga, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? Katika uzee wake, hata hivyo, alipata ugonjwa wa miguu.
24 Kisha Asa akalala na mababu zake na akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi baba yake. Yehoshafati mwanae akawa mfalme mahali pake.
Kisha Asa akalala pamoja na baba zake na kuzikwa pamoja nao katika mji wa Daudi baba yake. Naye Yehoshafati mwanawe akawa mfalme baada yake.
25 Nadabu mwana wa Yerobiamu alianza kutawala huko Israeli wakati wa mwaka wa pili wa Asa mfalme wa Yuda; Aliitawala Israeli kwa miaka miwili.
Nadabu mwana wa Yeroboamu akawa mfalme wa Israeli katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Asa wa Yuda, naye akatawala Israeli kwa miaka miwili.
26 Akafanya yaliyo maovu mbele y a macho ya BWANA naye akatembea katika njia ya baba yake, na katika dhambi yake, aliisababisha Israeli kufanya dhambi.
Akafanya maovu machoni pa Bwana, akienenda katika njia za baba yake na katika dhambi yake, ambayo alisababisha Israeli kuifanya.
27 Baasha mwana wa Ahiya, wa familia ya Isakari, akafanya hila dhidi ya Nadabu; Baasha akamwua huko Gibethoni, ambao ulikuwa mji wa Wafilisti, kwa kuwa Nadabu na Israeli walikuwa wakiuhusuru Gibethoni.
Baasha mwana wa Ahiya wa nyumba ya Isakari akafanya shauri baya dhidi yake, naye akamuua huko Gibethoni, mji wa Wafilisti, wakati Nadabu na Israeli yote walipokuwa wameuzingira.
28 Katika mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha alimwua Nadabu naye akawa mfalme mahali pake.
Baasha akamuua Nadabu katika mwaka wa tatu wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, naye Baasha akaingia mahali pake kuwa mfalme.
29 Mara tu baad ya kuwa mfalme, Baasha aliwaua watu wote wa familia ya Yeroboamu. Hakumwacha hata mmoja wa uzao wa Yeroboamu awe hai; Kwa njia hii akawa ameuharibu ukoo wote wa kifalme, kama vile BWANA alivyokuwa amesema kupitia mtumishi wake Ahiya Mshilo,
Mara tu alipoanza kutawala, aliua jamaa yote ya Yeroboamu. Hakumwachia Yeroboamu yeyote aliyekuwa hai, bali aliwaangamiza wote, kulingana na neno la Bwana lililotolewa kupitia kwa mtumishi wake Ahiya Mshiloni,
30 kwa sababu ya dhambi za Yeroboamu ambazo alifanya na akaisababishia Israeli kufanya dhambi, kwa kuwa alimkasirisha BWANA, Mungu wa Israeli.
kwa sababu ya dhambi alizokuwa amezitenda Yeroboamu na kusababisha Israeli kuzitenda, tena kwa sababu alimkasirisha Bwana, Mungu wa Israeli.
31 Mambo mengine yanayomhusu Nadabu, na yote aliyofanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
Kwa matukio mengine ya utawala wa Nadabu na yote aliyofanya, je hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?
32 Kisha kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli katika siku zao zote.
Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli wakati wote wa utawala wao.
33 Katika mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha mwana wa Ahiya alianza kuitawala Israeli yote huko Tirza naye alitawala kwa miaka ishirini na nne.
Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha mwana wa Ahiya akawa mfalme wa Israeli yote huko Tirsa, naye akatawala kwa miaka ishirini na minne.
34 Naye akafanya yaliyo mabaya katika macho ya BWANA na akatembea katika njia ya Yeroboamu na katika dhambi yake ambayo kwa hiyo aliifanya Israeli kufanya dhambi.
Akatenda maovu machoni pa Bwana, akienenda katika njia za Yeroboamu na dhambi yake, ambayo alikuwa amesababisha Israeli kuitenda.

< 1 Wafalme 15 >