< 1 Wafalme 10 >

1 Malkia wa Sheba aliposikia uvumi wa Sulemani kuhusu jina la BWANA, alikuja kumjaribu kwa maswali magumu.
[舍巴女王來訪]舍巴女王聽說撒羅滿因上主之名獲得的聲望,即前來以難題考問撒羅滿。
2 Alikuja Yerusalemu na msafara mrefu, pamoja na ngamia waliokuwa wamebeba mizigo ya manukato, dhahabu nyingi, na mawe mengi ya thamani, akamwambia Sulemani yote yaliyokuwa moyoni mwake.
她帶了許多隨員,駱駝裝載大批的香料、黃金和寶石,來到了耶路撒冷;當她進見撒羅滿時,就向他提出了心中的一切疑難,
3 Sulemani akajibu maswali yake yote. Hapakuwepo na swali ambalo aliuliza na mfalme akashindwa kujibu.
撒羅滿對她所問的一切難題,一一給她解答了,沒有一樣可難住君王,而不能給她解答的。
4 Malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Sulemani, na ikulu aliyokuwa amejenga,
舍巴女王看見了撒羅滿的種種智慧和建造的宮殿,
5 chakula cha mezani kwake, kuketi kwa watumishi wake, kazi ya watumishi wake na kuvaa kwao, pia wanyweshaji wake, na jinsi alivyotoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya BWANA, roho yake ilizimia.
筵席上的餚饌,群臣的坐次,僕從的侍候和服裝,供應的飲料,以及他在上主殿內奉獻的全燔祭,驚訝得出神,
6 Akamwambia mfalme, “Ni kweli, ile taarifa ambayo nimeisikia nchini kwangu juu ya maneno yako na hekima yako.
因而對君王說:「關於你的言行和智慧,我在我國內所聽到的傳說,的確是真的!
7 Sikuamini kile nilichosikia hadi nilipofika hapa, na sasa macho yangu yamejionea. Hata nusu ya hekima na utajiri wako! Umezidi uvumi ambao nilikuwa nimesikia.
以前我原不相信這些傳聞,及至我來親眼見了,纔知道人告訴我的還不及一半;你的智慧和你的富貴遠超過我所聽聞的。
8 Tazama jinsi walivyobarikiwa wake zako, na jinsi walivyobarikwa watumishi wako ambao daima husimama mbele yako, kwa sababu wanasikia hekima zako.
你的妻妾,你的臣僕,能常常侍立在你面前,聆聽你的智慧,是多麼有福!
9 BWANA, Mungu wako asifiwe, ambaye amependezwa na wewe, ambaye alikuweka kwenye kiti cha enzi cha Israeli. Kwa sababu BWANA aliipenda Israeli milele, na sasa amekufanya wewe kuwa mfalme, ili kwamba utoe hukumu ya kweli na ya haki.
上主你的天主應受讚美!他喜愛你,使你坐了以色列的王位;上主因為永遠喜愛以色列,纔立你為王,秉公行義。」
10 Basi Malikia alimpatia mfalme zaidi ya kilo 4500 za dhahabu na kiasi kikubwa cha mawe ya thamani. Hapakuwahi kutokea kiasi kikubwa cha viungo kama hiki ambacho Malkia wa Sheba alitoa kwa mfalme Sulemani kuwahi kutolewa tena.
舍巴女王遂將一百二十「塔冷通」黃金,大批香料和寶石,贈送給君王;以後進入的香料,再沒有像舍巴女王送給撒羅滿的那樣多。
11 Ile merikebu ya Hiramu, ambayo ilileta dhahabu kutoka Ofri, pia ilileta Kutoka Ofri kiasi kikubwa cha miti ya msandali na vito vya thamani.
從敖非爾運金子的希蘭船隻,也從敖非爾運來了大批檀香木和寶石。
12 Mfalme alitengeneza nguzo za hekalu kwa ajili ya hekalu la BWANA na kwa nyumba ya mfalme, na vinubi na vinanda kwa hao waimbaji. haijatokea kiasi cha miti ya misandali kama hicho ambacho kimewahi kutokea hadi leo.
君王用檀香木,為上主的殿和君王的宮殿製造了欄杆,又為歌詠者製造了琴和瑟;以後再沒有這樣的檀香木運進來,也沒有人再看見過,直到今天。
13 Mfame Sulemani alimpatia Malkia wa Sheba kila kitu ambacho alihitaji, na kila kitu alichoomba, na zaidi ya yote Sulemani alimpatia kwa ukarimu wake vitu vya kifalme. Kisha akarudi kwake na watumishi wake.
撒羅滿王除了照王的寬洪大量送給舍巴女王的禮品外,凡女王所要求的喜愛的物品,君王都送給了她。以後,她和自己的臣僕走了,回了本國。撒羅滿的財富
14 Kiasi cha dhahabu ambazo zililetwa kwa Sulemani kwa mwaka mmoja kilikuwa takribani kilo elfu ishirini na tatu za dhahabu,
撒羅滿每年收入的金子,重量有六百六十六「塔冷通;」
15 zaidi ya dhahabu ambazo wafanya biashara na wachuuzi walileta. Wafame wote wa Uarabuni na maliwali wa nchi pia walileta dhahabu na fedha kwa Sulemani.
由商人、小販、各國君王和本國太守所進獻的,尚不計算在內。
16 Mfalme Sulemani alitengeneza ngao mia mbili za dhahabu iliyofuliwa, shekeli mia sita za dhahabu zilichukuliwa pamoja na ngao.
撒羅滿王用黃金打造了二百個大盾牌,每個用金六百「協刻耳。」
17 Pia alitengeneza ngao mia tatu za dhahabu iliyofuliwa. Mane tatu za dhahabu ziliambatana pamoja na ngao moja moja; mfalme aliviweka katika ikulu ya mwitu ya Lebanoni.
有用黃金打造了三百個小盾牌,每個用金三「米納。」君王把這些盾牌,都放在黎巴嫩林宮。
18 Kisha mfalme akafanya kiti kikubwa cha enzi kwa pembe na akakisakafia kwa dhahabu laini.
君王又用象牙製造了一個大寶座,用純金包鑲。
19 Hicho kiti kilikuwa na ngazi sita, na kitako chake kilikuwa cha mviringo. Na kilikuwa kimezungushiwa kwa mikono pande zake zote. Na simba wawili walisimama pembeni mwa ile mikono.
寶座有六級台階,座背後有牛頭,座位兩邊有扶手,扶手兩旁立著兩隻獅子。
20 Kulikuwa na simba kumi na wawili waliokuwa wamesimama kwenye ile ngazi. Moja katika kila upande wa ngazi hizo. Hapakuwepo na kiti kama hicho katika ufalme mwingine.
六級台階上立著十二隻獅子,每邊六隻。任何國家都沒有像這樣的寶座。
21 Vikombe vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu. Na vikombe vyote vya kunywea vya ikulu ya mwitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hapakuwepo na kikombe cha fedha, kwa sababu fedha haikuwa na thamani katika siku za Sulemani.
撒羅滿王所有飲器都是金的,黎巴嫩林宮的一切器具,都是純金的,沒有一件是銀子的;銀子在撒羅滿時代並不值什麼。
22 Mfalme alikuwa na merikebu za kusafiri pamoja na merikebu za Hiramu. Mara moja kila mwaka merikebu zilileta dhahabu, fedha, na pembe za ndovu, pamoja na nyani na tumbili.
因為君王有一隊塔爾史士船隻,與希蘭的船隻一同航海;去塔爾史士的船隻,每三年往返一次,運來金、銀、象牙、猿猴和孔雀。撒羅滿的智慧
23 Kwa hiyo mfalme Sulemani aliwazidi wafalme wote ulimwenguni katika utajiri n a hekiima.
這樣,撒羅滿王在富貴和智慧上,超過了世上所有的君王。
24 Dunia yote ilitafuta uwepo wa Sulemani ili kusikia hekima yake, ambayo Mungu alikuwa ameweka katika moyo wake.
全世界上的人都想見撒羅滿的面,聽聽天主賦於他心中的智慧。
25 Na wote waliomtembelea walilipa Kodi, vyombo vya fedha na vya dhahabu, na nguo na manukato na silaha na farasi na nyumbu, mwaka baada ya mwaka.
各人給他帶來自己的禮物:銀器、金器、衣服、兵器、香料、駿馬和騾子:年年都是如此。撒羅滿的馬車
26 Sulemani alikusanya pamoja magari n a wapanda farasi. Alikuwa na magari 1, 400 na wapanda farasi elfu kumi na mbili ambao alikuwa amewaweka kwenye miji ya magari pamoja naye Yerusalemu.
撒羅滿也積聚了戰車和騎兵;他擁有戰車一千四百輛,騎兵一萬二千,駐紮在屯車城和耶路撒冷君王左右。
27 Mfalme alikuwa na fedha kule Yerusalemu, pamoja na mawe ardhini. Alitengeneza miti ya mierezi kuwa mingi kama mikuyu iliyo katika nyanda za chini.
君王在耶路撒冷有的銀子多如石頭,香柏木多如平原的桑樹。
28 Sulemani alimiliiki farasi waliokuwa wamenunuliwa kutoka Misri na Kilikia. Wachuuzi wa mfalme waliwanunua kwa makundi, kila kundi kwa bei yake.
撒羅滿所有的馬,都是從慕茲黎和科厄運來的,是君王的商人付出定價,從科厄買來的。
29 Magari yalinunuliwa kutoka Misri kwa shekeli mia sita za fedha kila moja, na farasi kwa shekeli 150 kila moja. Vitu vingi katika hivi baadaye viliuzwa kwa wafalme wote wa Wahiti na Aramu.
從慕茲黎運來一輛戰車,需銀六百「協刻耳;」一匹馬,需銀一百五十「協刻耳。」同樣,為赫特人和阿蘭人的君王輸送車馬,也是經過這些商人。

< 1 Wafalme 10 >