< 1 Wafalme 1 >
1 Mfalme Daudi alipokuwa mzee sana, walimfunika kwa nguo, lakini hakupata joto.
2 Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, “Na tutafute msichana bikra kwa ajili ya mfalme bwana wetu. Ili amtumikie na kumtunza. Naye atalala kwenye mikono yake ili bwana mfalme wetu apate joto.
3 Kwa hiyo wakatafuta msichana mrembo katika mipaka yote ya Israeli. Wakampata Abishagi Mshunami wakamlte kwa mfalme.
4 Yule msichana alikuwa mrembo sana. Naye akamtumikia mfalme na kumtunza, Lakini mfalme hakumjua.
5 Wakati huo, Adoniya mwana wa Hagithi alijiinua akisema, “Nitakuwa mfalme.” Kwa hiyo akajiandalia magari na wapanda farasi hamsini ili wapige mbio mbele yake.
6 Baba yake alikuwa hajawahi kumsumbua, kwa kusema, “kwa nini umefanya hili na lile?” Adoniya allikuwa mwanamume mzuri sana aliyezaliwa baada ya Absalomu.
7 Akashauriana na Yoabu mwana wa Seruya na Abiathari kuhani. Wakamfuata Adoniya wakamsaidia.
8 Lakini Sadoki kuhani, Benaya mwana wa Yehoyada, nabii Nathani, Shimei, Rei, na watu mashujaa wa Daudi hawakumfuata Adoniya.
9 Adoniya akataoa dhabihu za Kondoo, na ndama walionona kwenye jiwe la Sohelethi, ambalo liko karibu na Eni Rogeli. Akawakaribisha ndugu zake wote, watoto wa mfalme, wanaume wote wa Yuda, na watumishi wa mfalme.
10 Lakini hakumkaribisha nabii Nathan, Benaya, wanaume mashujaa, au ndugu yake Sulemani.
11 Kisha Nathani akamwambia Bethisheba mama wa Sulemani, akaisema, “Je, haujasikia kuwa Adoniya mwana wa Hagathi amekuwa mfalme, na Daudi bwana wetu halijui hilo?
12 Kwa hiyo sasa nakupa ushauri, ili kwamba uweze kuokoa maisha yako na maisha ya mwanao Suleimani.
13 Nenda kwa mfalme Daudi; ukamwambie, 'Bwana wangu mfalme, Je, haukumwapia mtumishi wako, ukisema, “Hakika Sulemani mwanao atatawala baada yangu, na ataketi kwenye kiti changu cha enzi?” Kwa nini basi Adoniya anatawala?'
14 Wakati ukiwa pale ukiongea na mfalme, Nitaingia baada yako na kuthibitisha hayo.
15 Kwa hiyo Bathisheba akaingia chumbani kwa mfalme. Wakati huo mfalme alikuwa mzee sana, na Abishagi Mshunami alikuwa akimtunza mfalme.
16 Bathisheba akaiinama kifudifudi mbele ya mfalme. Na kisha mfalme akasema, “Una haja gani?”
17 Naye akamwambia, “Bwana wangu, ulimwapia mtumishi wako kwa jina la BWANA, Mungu wako, ukisema, 'Hakika Sulemani mwanao atatawala, baada yangu, naye ataketi kwenye kiti changu cha enzi.'
18 Sasa, tazama, Adoniya ni mfalme, na bwana wangu mfalme hajui jambo hili.
19 Ametoa dhabihu ya makisai, ndama walionona, na kondoo wengi, na amewakaribisha wana wote wa mfalme, Abiathari kuhani, na Yoabu jemedari wa jeshi, lakini hajamkaribisha Sulemani mtumishi wako.
20 Mfalme bwana wangu, macho yote ya Israeli yako kwako, yakisubiri usemi wako juu ya nani atakayeti kwenye kiti cha enzi baada yako, bwana wangu.
21 Vinginevyo itatokea, wakati bwana wangu atakapolala na baba zake, kwamba Mimi na mwanangu Sulemani kuhesabiwa wahaini.”
22 Wakati alipokuwa akiendelea na mfalme, nabii Nathani aliingia.
23 Watumshi wakamwambia mfalme, “Nabii Nathani yuko hapa,” Naye alipoingia mbele ya mfalme, akalala kifudifudi mbele ya mfalme na uso wake ukielekea chini.
24 Nathani akamwambia, “Mfalme bwana wangu, Je, umesema, Adoniya atatawala baada yangu, na ataketi kwenye kiti changu cha enzi?
25 kwani leo ameshuka na ametoa dhabihu ya makisai, ndama walionona, na kondoo wengi, na amewakaribisha wana wote wa mfalme, jemedari wa jeshi, na Abiatahari kuhani. Nao wanakuka na kunywa mbele zake, na kusema, 'Mfalme Adoniya na aishi milele!'
26 Lakini mimi, mtumishi wako, Sadoki kuhani, Benaya mwana wa Yehoyada, na mtumishi wako Suleimani, hajatukaribisha.
27 Je, bwana wangu mfalme amefanya haya pasipo kutuambia sisi, watumishi wako, ni nani atakayeketi kwenye kiti cha enzi baada yake?”
28 Ndipo mfalme Daudi lipojibu na kusema, “Mwiteni Bathisheba arudi.” Naye akaja akasimama mbele ya mfalme.
29 Mfalme akafanya kiapo akasema, “Kama BWANA aishivyo, ambaye ameniokoa toka tabu zote,
30 kama nilivyokuapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli, nikisema, 'Sulemani mwanao atatawala baada yangu, naye ndiye atakayeketi kwenye kiti changu cha enzi, mahali pangu,' Nitafanya hivi leo.”
31 Kisha Bathisheba akalala kifudifudi na sura yake ikielekea chini mbele ya mfalme akasema, “Bwana wangu mfalme Daudi n a aishi milele!”
32 Mflme Daudi akasema, “Niitieni Sadoki kuhani, nabii Nathani na Benaya mwana wa Yehoyada.” Nao wakaja mbele ya mfalme.
33 Mfalme akawaambia, “Uwachukue watumishi wangu, bwana wako, na umfanye Sulemani mwanangu apande juu ya nyumba yangu mimi na mkamtelemshe mpaka chini Gihoni.
34 Na Sadoki kuhani na nabii Nathani wamtawaze awe mfalme wa Israeli na tarumbeta zipigwe, 'Mfalme Suleimani na uishi milele!'
35 Kisha njoni mkiwa nyuma yake, naye atakuja na kukaa kwenye kiti changu cha enzi; kwani yeye ndiye atakayekuwa mfalme mahali pangu. Nimemchagua yeye kuwa mtawala wa Israeli na Yuda.”
36 Benaya mwana wa Yehoyada akamjibu mfalme, akasema, “Na iwe hivyo! Na BWANA, Mungu wa mfalme bwana wangu, alithibitishe hilo.
37 Kama vile BWANA alivyokuwa na mfalme bwana wangu na awe na Sulemani hivyo hivyo, na kuifanya enzi yake kuwa kubwa kuliko zaidi ya enzi ya bwana wangu Daudi.”
38 Kwa hiyo Sadoki kuhani, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, na Wakerethi na Wapelethi wakamfanya Sulemani akapanda juu ya nyumba ya mfalme Daudi; wakamleta Gihoni.
39 Naye Sadoki kuhani akachukua pembe lenye mafuta hemani akamtia mafuta Sulemani kisha wakapiga tarumbeta, na watu wote wakasema, 'Mfalme Sulemani na aishi milele!'
40 Kisha watu wote wakamfuata, na watu wakapiga zomari wakafurahi furaha kubwa mno, kiasi kwamba dunia ikatetemeka kwa sauti zao.
41 Kisha Adoniya na wageni wake waliokuwa pamoja naye wakasikia hayo walipomaliza kula. Yoabu alipozisikia sauti za panda, akasema, “Kwa nini jiji lilko katika hali ya taharuki?”
42 Wakati alipokuwa akiongea, Yonatahani mwana wa Abiathari kuhani alifika. Adoniya akamwambia, “Karibu, 'kwa kuwa wewe wastahili kutuletea habari.”
43 Naye Yonathani akamjibu Adoniya, “Mfalme bwana wetu Daudi amemfanya Sulemani kuwa mfalme.
44 Na mfalme amemtuma pamoja naye Sadoki, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, na Wakerethi pamoja na Wapelethi. Wamempandisha Sulemani juu ya nyumba ya mfalme.
45 Sadoki kuhani na nabii Nathani wamemtawaza kuwa mfalme kule Gihoni, na wametokea huko wakifurahi, ndiyo maana jiji liko katika taharuki. Na hizi ndizo sauti ulizosikia.
46 Pia, Sulemani ameketi kwenye kiti cha enzi cha ufalme.
47 Zaidi ya yote, watumishi wa mfalme walikuja kumbariki mfalme bwana wetu Daudi, wakisema, 'Mungu wako na alifanye jina la Sulemani kuwa zuri kuliko jina lako, na kuifanya enzi yako kuwa kubwa kuliko yako.' na mfalme akasujudu mwenyewe kitandani.
48 Mfalme pia alisema, 'Abarikiwe BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye amempa mtu kuketi kwenye enzi yangu siku hii ya leo, na kwamba macho yangu yamejionea hilo.'”
49 Ndipo wageni wote wa Adoniya walipoogopa sana. Wakasimama na kila mtu akaenda njia yake.
50 Pia Adoniya alimwaogopa Sulemani na akasimama, na akaondoka, akachukua pembe la madhabahuni.
51 Kisha Sulemani akaambiwa hilo, wakasema, “Tazama, Adoniya amemwogopa mfalme Sulemani, kwa kuwa ameshikilia pembe la madhabahuni, akisema, 'Mfalme Sulemani na aniapie kwanza kuwa hatamwua mtumishi wake kwa upanga.'”
52 Sulemani akasema, “Kama atajionyesha kuwa ni mtu wa kweli, hakuna hata unywele mmoja utakaoanguka duniani, bali kama uovu utaonekana kwake, atakufa.”
53 Kwa hiyo mfalme Sulemani akatuma watu, waliomleta Adoniya kutoka madhabahuni. Naye akaja akapiga magoti kwa Sulemani, na Sulemani akamwambia, “Nenda nyumbani kwako.”