< 1 Yohana 1 >
1 Kile kilichokuwapo tangu mwanzo-kile tulichokisikia, kile tulichokiona kwa macho yetu, kile tulichokitazama, na mikono yetu imekishika-kuhusu Neno la uzima.
Tunawajulisha lile lililokuwepo tangu mwanzo, lile tulilosikia, ambalo tumeliona kwa macho yetu, ambalo tumelitazama na kuligusa kwa mikono yetu, kuhusu Neno la uzima.
2 Na ule uzima ulifanywa kujulikana wazi, na tumeuona, na kuushuhudia, na kuwatangazia uzima wa milele, ambao ulikuwa kwa Baba na ulifanywa kujulikana kwetu. (aiōnios )
Uzima huo ulidhihirishwa; nasi tumeuona na kuushuhudia, nasi twawatangazia uzima wa milele, ambao ulikuwa pamoja na Baba, nao ukadhihirishwa kwetu. (aiōnios )
3 Kile tulichokiona na kukisikia twakitangaza kwenu pia, ili kwamba muweze kujumuika pamoja nasi, na ushirika wetu pamoja na Baba na Mwanae Yesu Kristo.
Twawatangazia lile tuliloliona na kulisikia, ili nanyi mwe na ushirika nasi. Na ushirika wetu hasa ni pamoja na Baba na Mwanawe, Yesu Kristo.
4 Na tunawandikia mambo haya ninyi ili kwamba furaha yetu iwe timilifu.
Tunaandika mambo haya ili furaha yetu ipate kuwa timilifu.
5 Huu ndio ujumbe tuliousikia kutoka kwake na kuwatangazia: Mungu ni nuru na ndani yake hakuna giza hata kidogo.
Huu ndio ujumbe tuliosikia kutoka kwake na kuwatangazia ninyi: kwamba Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza lolote.
6 Kama tukisema kwamba tunaushirika naye na twatembea gizani, twadanganya na hatutendi kweli.
Kama tukisema kwamba twashirikiana naye huku tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatutendi lililo kweli.
7 Lakini tukitembea katika nuru kama alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu ya Yesu Kristo, mwanae yatutakasa kutoka dhambi zote.
Lakini tukienenda nuruni, kama yeye alivyo nuruni, twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.
8 Kama tukisema hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, na kweli haimo ndani yetu.
Kama tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu.
9 Lakini tukizitubu dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na haki kutusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.
Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutoka kwenye udhalimu wote.
10 Tukisema kwamba hatujatenda dhambi, twamfanya yeye kuwa muongo, na neno lake halimo ndani yetu.
Kama tukisema hatukutenda dhambi, twamfanya yeye kuwa mwongo na neno lake halimo ndani yetu.