< 1 Wakorintho 9 >

1 Mimi si huru? Mimi si mtume? Mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Ninyi si matunda ya kazi yangu katika Bwana?
Nene si huru? Nene si mtume? Nene nsmbwene lepi Yesu Bwana watete? muenga si matunda gha mbombo ya nene katika Bwana?
2 Ikiwa mimi si mtume kwa wengine, angalau ni mtume kwenu ninyi. Kwa maana ninyi ni uthibitisho wa utume wangu katika Bwana.
Ikiwa nene si mtume kwa bhangi angalau ni mtume kwa yhomo muenga. Kwa maana muenga ni uthibitisho wa utume wanene katika Bwana.
3 Huu ndio utetezi wangu kwa wale wanaonichunguza mimi.
Obho ndio utetezi wanene kwa bhala bhakanichunguza nene.
4 Je hatuna haki ya kula na kunywa?
Je tuyelepi ni haki ya kulya ni kunywa?
5 Hatuna haki kuchukua mke aliye amini kama wafanyavyo mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?
Tuyelepi ni haki kutola ndala ya amini kama yakibhikheta mitume bhangi, ni bhalongo bha Bwana, ni Kefa?
6 Au ni mimi peke yangu na Barnaba ambao tunapaswa kufanya kazi?
Au ni nene namwene ni Barnaba ambavo twipasibhwa kufuanya mbombo?
7 Ni nani afanyaye kazi kama askari kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mzabibu na asile matunda yake? Au ni nani achungaye kundi asiyekunywa maziwa yake?
Niani yaifuanya ya muene? Ni niani yaipanda mzabibu na akolokulya matunda ghaki? Au ni niani yaichunga likundi yaibela kunywa maziwa ghaki?
8 Je ninasema haya kwa mamlaka ya kibinadamu? Sheria nayo haisemi haya?
Je nijobha agha kwa mamlaka gha kibinadamu? Sheria ni yhene yijobha hee naha?
9 Kwa kuwa imeandikwa katika sheria ya Musa, “usimfunge ng'ombe kinywa apulapo nafaka.” Ni kweli kwamba hapa Mungu anajali ng'ombe?
Kwa ndabha iyandikibhu katika sheria ya Musa, “Kolokuikhonga ng'ombi kinywa payilya nafaka.” Ni ukueli kwamba apa K'yara ijali ng'ombi?
10 Au je hasemi hayo kwa ajili yetu? imeandikwa kwa ajili yetu, kwa sababu yeye alimaye nafaka inampasa kulima kwa matumaini, naye avunaye inampasa avune kwa matarajio ya kushiriki katika mavuno.
Au je ijobhalepi kwa ajili ya tete? ujandikibhu kwa ajili ya tete, kwa ndabha yhola yailheme nafaka yikampasa kulhema kwa matumaini, ni muene yaifuna yikampasa afunai kwa matarajio gha kushiriki mu mavuno.
11 Ikiwa tulipanda vitu vya rohoni miongoni mwenu, Je! Ni neno kubwa kwetu tukivuna vitu vya mwilini kutoka kwenu?
Ikiwa twapandili fhenu fya rohoni miongoni mwayhomo, Je! Ni lisu libhaha kwa tete tukavunai fhenu fya mumbhele kuhoma kwa yhomho?
12 Ikiwa wengine walipata haki hii kutoka kwenu, Je! Sisi si zaidi? Hata hivyo, hatukuidai haki hii. Badala yake, tulivumilia mambo yote badala ya kuwa kikwazo cha injili ya Kristo.
Ikiwa bhangi bhakakabhili haki eye kuhoma kwa muenga, Je! tete si zaidi? Hata naha, tukadai hee haki eye. Badala yiaki, twavumilili mambo ghoa badala ya kuya kikwazo kya injili ya Kristu.
13 Hamjui ya kuwa wote wafanyao kazi hekaluni hupata chakula chao kutoka hekaluni? Hamjui ya kuwa wote watendao kazi madhabahuni hupata sehemu ya kile kilichotolewa madhabahuni?
Mumanyili lepi ya kuwa bhoa bhabhifuanya mbombo hekaluni? bhikabha kyakulya kya bhene kuhoma hekaluni? Mumanyili lepi ya kuwa bhoa bhabhitenda mbombo madhabahuni bhikabha sehemu ya khela kakitolibhu madhabahuni?
14 Kwa jinsi iyo hiyo, Bwana aliagiza ya kuwa wote wanaoitangaza injili sharti wapate kuishi kutokana na hiyo injili.
Kwa jinsi eyu eyu, Bwana alaghisi ya kuwa bhoa bhoa bhabhikaitangasya injili sheriti bhakabhai kuishikutokana ni eyu injili.
15 Lakini sijawadai haki zote hizi. Na siandiki haya ili jambo lolote lifanyike kwa ajili yangu. Ni heri mimi nife kuliko mtu yeyote kubatilisha huku kujisifu kwangu.
Lakini nikabhadai haki sioa esu. Na niyandika hee agha ilii jambo lilyoha lhela lifuanyikai kwa ajili ya nene. Ni heri nene nifwai kuliko munu yuywoha kubatilisya khoni kujisifu kwa nene.
16 Maana ikiwa naihubiri injili, sina sababu ya kujisifu, kwa sababu ni lazima nifanye hivi. Na ole wangu nisipoihubiri injili!
Maana ikiwa nihubiri injili, niyelepi ni sababu ni lazima nifuanya naha, ni ole wangu nikabelai kuhubiri injili!
17 Kwa maana nikifanya hivi kwa hiari yangu, nina thawabu. Lakini ikiwa si kwa hiari, bado nina jukumu nililopewa kuwa wakili.
Kwa maana nikafuanyai naha kwa hiari ya nene, nuja ni thawabu. Lakini ikiwa si kwa hiari, nakhona nujele ni jukumu lanipelibhu kuya wakili.
18 Basi thawabu yangu ni nini? Ya kuwa nihubiripo, nitaitoa injili pasipo gharama na bila kutumia kwa utimilifu wa haki yangu niliyonayo katika Injili.
Basi thawabu yanene kiki? ya kuwa panihubiri, nilola kuipisya injili pasipo gharama ni bila kutumila kwa utimilifu wa haki ya nene yaniyenayu mu injili.
19 Maana japo nimekuwa huru kwa wote, nilifanyika mtumwa wa wote, ili kwamba niweze kuwapata wengi zaidi.
Maana japo niyele huru kwa bhoa, nafuanyiki mtumwa wa bhoa, ili kwamba nibhuesyai kubha kabha bhingi zaidi.
20 Kwa Wayahudi nilikuwa kama Myahudi, ili niwapate Wayahudi. Kwa wale walio chini ya sheria, nilikuwa kama mmoja wao aliye chini ya sheria ili niwapate wale walio chini ya sheria. Nilifanya hivyo ingawa mimi binafsi sikuwa chini ya sheria.
Kwa bhayahudi wayele kama myahudi ili nikabhakabhai bhayahudi kwa bhala bhabhayele chini ya sheria nayele kama mmonga wa bhene yayele chini ya sheria ili nibhakabhai bhala bhabhayele chini ya sheria. Nafuanyili naha ingawa nene binafsi nayelepi chini ya sheria.
21 Kwa wale walio nje ya sheria, nilikuwa kama mmoja wao nje ya sheria, ingawa mimi binafsi sikuwa nje ya sheria ya Mungu, bali chini ya sheria ya Kristo. Nilifanya hivyo ili niwapate wale walio nje ya sheria.
Kwa bhala bhabhayele nje ya sheria, nayele kama mmonga wa bhene nje ya sheria, ingawa nene binafsi nayelepi nje ya sheria ya K'yara, bali chini ya sheria ya Kristu. Nafuanyili naha ili nibhakabhai bhala bhabhayele nje ya sheria.
22 Kwa walio wanyonge nilikuwa mnyonge, ili niwapate walio wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa baadhi.
Kwa bhayele bhanyonge, ili nayele mnyonge ili nibhakabhai bhabhayele bhanyonge. Niyele hali sioa kwa bhanu bhoa ili kwa njela syoa nikabhai kubhaokola baadhi.
23 Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya injili, ili nipate kushiriki katika baraka.
Ninene nifuanya mambo ghoa kwa ajili ya injili, ili nikabhai kushiriki katika baraka.
24 Hamjui ya kuwa katika mbio wote washindanao hupiga mbio, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Hivyo pigeni mbio ili mpate tuzo.
Mumanyili lepi ya kuwa mu mbio bhoa bhabhishindana bhipinga mbio, lakini yaipokela tuzo ni mmonga? Henu mkembhelai mbio ili mkabhai tuzo.
25 Mwana michezo hujizuia katika yote awapo katika mafunzo. Hao hufanya hivyo ili wapokee taji iharibikayo, lakini sisi tunakimbia ili tupate taji isiyoharibika.
Mwana michezo kajizuila mu ghoa pauja mu mafunzo. Abhu bhifuanya naha ili bhapokelai taji yaiharibika, lakini tete twivembhela hela ili tukabhaa taji yaibela kuharibika.
26 Kwa hiyo mimi sikimbii bila sababu au napigana ngumi kama kupiga hewa.
Henu nene nikhembhela lepi bila sababu au ni kukomana numi kama kutobha mpongho.
27 Lakini nautesa mwili wangu na kuufanya kama mtumwa, ili kwamba nijapokwisha kuwahubiri wengine, mimi mwenyewe nisiwe wa kukataliwa.
Lakini ikautesya mbhele wa nne ni kuufuanya kama mtumwa, ili kwamba nijapokwisha kubhahubiri bhangi, nene na muene ni kholho kuya wa kubelekilibhwa.

< 1 Wakorintho 9 >