< 1 Wakorintho 8 >

1 Sasa kuhusu vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu: tunajua ya kwamba “sisi sote tuna maarifa.” Maarifa huleta majivuno, bali upendo hujenga.
至論祭邪神的肉,我們知道「我們都有知識。」但知識只會使人傲慢自大,愛德才能立人。
2 Ikiwa mtu yeyote anadhani kwamba anajua jambo fulani, mtu huyo bado hajui kama impasavyo kujua.
若人自以為知道什麼,這是他還不知道他該怎樣知道。
3 Lakini ikiwa mmoja wapo akimpenda Mungu, mtu huyo anajulikana naye.
而誰若愛天主,這人才為天主所認識。
4 Basi kuhusu kula vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu: twajua kuwa “sanamu si kitu katika dunia hii,” na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu.”
至論吃祭邪神的肉,我們知道:世上並沒有什麼邪神;也知道:除了一個天主外,沒有什麼神。
5 Kwa maana kuna wengi waitwao miungu ikiwa ni mbinguni au duniani, kama vile walivyo “miungu na mabwana wengi.”
因為雖然有稱為神的,或在天上,或在地下,就如那許多「神」和許多「主,」
6 “Ijapokuwa kwetu kuna Mungu mmoja tu ambaye ni Baba, vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake, na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na kwa yeye sisi tupo.”
可是為我們只有一個天主,就是聖父,萬物都出於祂,而我們也歸於祂;也只有一個主,就是耶穌基督,萬物藉祂而有,我們也藉祂而有。
7 Hata hivyo, ujuzi huu haupo ndani ya kila mmoja. Badala yake, wengine walishiriki ibada za sanamu hapo zamani, na hata sasa wanakula vyakula hivi kana kwamba ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu. Dhamiri zao zimepotoshwa kwa kuwa ni dhaifu.
不過這種知識不是人人都有的;有些人直到如今因拜慣了邪神,以為所吃的是祭邪神的肉,因為他們的良心軟弱,就受了玷污。
8 Lakini chakula hakitatuthibitisha sisi kwa Mungu. Sisi sio wabaya sana kama tusipo kula, wala wema sana ikiwa tutakula.
其實,食物不能使我們取悅天主:我們不吃也無損,吃了也無益。
9 Lakini iweni makini ya kwamba uhuru wenu usiwe sababu ya kumkwaza aliye dhaifu katika imani.
但你們要慬慎,免得你們這自由的決擇,成了軟人的絆腳石。
10 Hebu fikiri kwamba mtu amekuona, wewe uliye na ujuzi, unakula chakula katika hekalu la sanamu. Dhamiri yake mtu huyo haitathibitika hata yeye naye ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu?
因為,如果有人看見你們這有知識的,在邪神廟裏坐席,他的良心若是軟弱,豈不受到鼓勵而去吃祭邪神的肉嗎?
11 Kwa hiyo kwa sababu ya ufahamu wako wa ukweli juu ya asili ya sanamu, kaka au dada yako aliye dhaifu, ambaye pia Kristo alikufa kwa ajili yake, anaangamizwa.
那麼這軟弱的人,基督為他而死的弟兄,也就因了你的知識而喪亡!
12 Hivyo, unapofanya dhambi dhidi ya kaka na dada zako na kuzijeruhi dhamiri zao zilizo dhaifu, mnatenda dhambi dhidi ya Kristo.
你們這樣得罪了修士們,了傷了他們軟弱的良心,就是得罪基督。
13 Kwa hiyo, ikiwa chakula kinasababisha kumkwaza kaka au dada, sitakula nyama kamwe, ili nisimsababishe kaka au dada yangu kuanguka. (aiōn g165)
為此,若是食物使我的弟兄跌倒,我就永遠不吃肉,免得叫我的弟兄跌倒。 (aiōn g165)

< 1 Wakorintho 8 >