< 1 Wakorintho 7 >
1 Kuhusu mambo mliyoniandikia: Kuna wakati ambapo ni vizuri mwanaume asilale na mke wake.
2 Lakini kwa sababu ya majaribu mengi ya zinaa kila mwanaume awe na mkewe, na kila mwanamke awe na mmewe.
3 Mume anapaswa kumpa mke haki yake ya ndoa, na vile vile mke naye kwa mmewe.
4 Si mke aliye na mamlaka juu ya mwili wake, ni mme. Na vile vile, mme naye hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mke anayo.
5 Msinyimane mnapolala pamoja, isipokuwa mmekubaliana kwa muda maalum. Fanyeni hivyo ili kupata muda wa maombi. Kisha mnaweza kurudiana tena pamoja, Ili kwamba Shetani asije akawajaribu kwa kukosa kiasi.
6 Lakini nasema haya mambo kwa hiari na si kama amri.
7 Natamani kila mmoja angekuwa kama mimi nilivyo. Lakini kila mmoja ana karama yake kutoka kwa Mungu. Huyu ana karama hii, na yule ana karama ile.
8 Kwa wasioolewa na wajane ninasema kwamba, ni vizuri kwao kama wakibaki bila kuolewa, kama nilivyo mimi.
9 Lakini kama hawawezi kujizuia, wanapaswa kuolewa. Kwa kuwa heri kwao kuolewa kuliko kuwaka tamaa.
10 Sasa kwa wale walioolewa nawapa amri, si mimi bali ni Bwana. “Mke asitengane na mme wake.”
11 Lakini kama akijitenga kutoka kwa mmewe, abaki hivyo bila kuolewa au vinginevyo apatane na mmewe. Na “Mme asimpe talaka mke wake.”
12 Lakini kwa waliobaki, nasema- mimi, si Bwana- kwamba kama ndugu yeyote ana mke asiyeamini na anaridhika kuishi naye, hapaswi kumwacha.
13 Kama mwanamke ana mme asiyeamini, na kama anaridhika kuishi naye, asimwache.
14 Kwa mme asiyeamini anatakaswa kwa sababu ya imani ya mkewe. Na mwanamke asiyeamini anatakaswa kwa sababu ya mmewe aaminiye. Vinginevyo watoto wenu wangekuwa si safi, lakini kwa kweli wametakaswa.
15 Lakini mwenzi asiyeamini akiondoka na aende. Kwa namna hiyo, kaka au dada hafungwi na viapo vyao. Mungu ametuita tuishi kwa amani.
16 Unajuaje kama mwanamke, huenda utamwokoa mmeo? Au unajuaje kama mwanaume, huenda utamwokoa mkeo?
17 Kila mmoja tu aishi maisha kama Bwana alivyowagawia, kila mmoja kama Mungu alivyowaita wao. Huu ni mwongozo wangu kwa makanisa yote.
18 Yupo aliyekuwa ametahiriwa alipoitwa kuamini? Asijaribu kuondoa alama ya tohara yake. Yupo yeyote aliyeitwa katika imani hajatahiriwa? Hapaswi kutahiriwa.
19 Kwa hili aidha ametahiriwa wala asiye tahiriwa hakuna matatizo. Chenye matatizo ni kutii amri za Mungu.
20 Kila mmoja abaki katika wito alivyokuwa alipoitwa na Mungu kuamini.
21 Ulikuwa mtumwa wakati Mungu alipokuita? Usijali kuhusu hiyo. Lakini kama unaweza kuwa huru, fanya hivyo.
22 Kwa mmoja aliyeitwa na Bwana kama mtumwa ni mtu huru katika Bwana. Kama vile, mmoja aliye huru alipoitwa kuamini ni mtumwa wa Kristo.
23 Mmekwisha nunuliwa kwa thamani, hivyo msiwe watumwa wa wanadamu.
24 Kaka na dada zangu, katika maisha yoyote kila mmoja wetu tulipoitwa kuamini, tubaki kama vile.
25 Sasa, wale wote ambao hawajaoa kamwe, sina amri kutoka kwa Bwana. Lakini nawapa maoni yangu kama nilivyo. Kwa huruma za Bwana, zinazo aminika
26 Kwa hiyo, ninafikiri hivyo kwa sababu ya usumbufu, ni vyema mwanaume abaki kama alivyo.
27 Umefungwa kwa mwanamke na kiapo cha ndoa? Usitake uhuru kutoka kwa hiyo. Una uhuru kutoka kwa mke au hujaolewa? Usitafute mke.
28 Lakini kama ukioa, hujafanya dhambi. Na kama mwanamke hajolewa akiolewa, hajafanya dhambi. Bado wale wanaoana wanapata masumbufu ya aina mbalimbali. Nami nataka niwaepushe hayo.
29 Lakini nasema hivi, kaka na dada zangu, muda ni mfupi. Tangu sasa na kuendelea, wale walio na wake waishi kama hawana.
30 Wote walio na huzuni wajifanye kama walikuwa hawana huzuni, na wote wanaofurahi, kama walikuwa hawafurahi, na wote wanaonunua kitu chochote, kama hawakumiliki chochote.
31 Na wote wanaoshughulika na ulimwengu, wawe kama hawakushughulika nao. Kwa kuwa mitindo ya dunia inafikia mwisho wake.
32 Ninataka muwe huru kwa masumbufu yote. Mwanaume asiyeoa anajihusisha na vitu vinavyo mhusu Bwana, namna ya kumpendeza yeye.
33 Lakini mwanaume aliyeoa hujihusisha na mambo ya dunia, namna ya kumpendeza mkewe,
34 amegawanyika. Mwanawake asiyeolewa au bikira hujihusisha na vitu kuhusu Bwana, namna ya kujitenga katika mwili na katika roho. Lakini mwanamke aliyeolewa hujihusisha kuhusu vitu dunia, namna ya kumfurahisha mme wake.
35 Nasema hivi kwa faida yenu wenyewe, na siweki mtego kwenu. Nasema hivi kwa vile ni haki, ili kwamba mnaweza kujiweka wakfu kwa Bwana bila kikwazo chochote.
36 Lakini kama mtu anafikiri hawezi kumtendea kwa heshima mwanawali wake, kwa sababu ya hisia zake zina nguvu sana, acha aoane naye kama apendavyo. Siyo dhambi.
37 Lakini kama amefanya maamuzi kutokuoa, na hakuna haja ya lazima, na kama anaweza kutawala hamu yake, atafanya vyema kama hatamwoa.
38 Hivyo, anayemwoa mwanamwali wake afanya vyema, na yeyote ambaye anachagua kutooa atafanya vyema zaidi.
39 Mwanamke amefungwa na mmewe wakati yu hai. Lakini kama mmewe akifa, yuko huru kuolewa na yeyote ampendaye, lakini katika Bwana tu.
40 Bado katika maamuzi yangu, atakuwa na furaha zaidi kama akiishi kama alivyo. Na ninafikiri kuwa nami pia nina Roho wa Mungu.