< 1 Wakorintho 3 >
1 Na mimi, kaka na dada zangu, sikusema nanyi kama watu kiroho, lakini kama na watu wa kimwili. Kama na watoto wadogo katika Kristo.
2 Niliwanywesha maziwa na si nyama, kwa kuwa hamkuwa tayari kwa kula nyama. Na hata sasa hamjawa tayari.
3 Kwa kuwa ninyi bado ni wa mwilini. Kwa kuwa wivu na majivuno yanaonekana miongoni mwenu. Je, hamuishi kulingana na mwili, na je, hamtembei kama kawaida ya kibinadamu?
4 Kwa kuwa mmoja husema, “Namfuata Paulo” Mwingine husema “Namfuata Apolo,” hamuishi kama wanadamu?
5 Apolo ni nani? na Paulo ni nani? Watumishi wa yule mliyemwamini, kwa kila ambaye Bwana alimpa jukumu.
6 Mimi nilipanda, Apolo akatia maji, lakini Mungu akakuza.
7 Kwa hiyo, si aliye panda wala aliyetia maji ana chochote. Lakini ni Mungu anayekuza.
8 Sasa apandaye na atiaye maji wote ni sawa, na kila mmoja atapokea ujira wake kulingana na kazi yake.
9 Kwa kuwa sisi tu watendakazi wa Mungu, ninyi ni bustani ya Mungu, jengo la Mungu.
10 Kutokana na neema ya Mungu niliyopewa kama mjenzi mkuu, niliuweka msingi, na mwingine anajenga juu yake. Lakini mtu awe makini jinsi ajengavyo juu yake.
11 Kwa kuwa hakuna mwingine awezaye kujenga msingi mwingine zaidi ya uliojengwa, ambao ni Yesu Kristo.
12 Sasa, kama mmoja wenu ajenga juu yake kwa dhahabu, fedha, mawe ya thamani, miti, nyasi, au majani,
13 kazi yake itafunuliwa, kwa mwanga wa mchana utaidhihirisha. Kwa kuwa itadhihirishwa na moto. Moto utajaribu ubora wa kazi wa kila mmoja alichofanya.
14 Kama chochote mtu alichojenga kitabaki, yeye atapokea zawadi.
15 Lakini kama kazi ya mtu ikiteketea kwa moto, atapata hasara. Lakini yeye mwenyewe ataokolewa, kama vile kuepuka katika moto.
16 Hamjui kuwa ninyi ni hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu yule. Kwa kuwa hekalu la Mungu ni takatifu, na hivyo na ninyi.
18 Mtu asijidanganye mwenyewe, kama yeyote miongoni mwenu anadhani ana hekima katika nyakati hizi, awe kama “mjinga” ndipo atakuwa na hekima. (aiōn )
19 Kwa kuwa hekima ya dunia hii ni ujinga mbele za Mungu, Kwa kuwa imeandikwa, “Huwanasa wenye hekima kwa hila zao”
20 Na tena “Bwana anajua mawazo ya wenye busara ni ubatili.”
21 Hivyo mtu asijivunie wanadamu! Kwa kuwa vitu vyote ni vyenu.
22 Kama ni Paulo, au Apolo, au Kefa, au dunia, au maisha, au kifo, au vitu vilivyopo, au vitakavyokuwepo. Vyote ni vyenu,
23 na ninyi ni wa Kristo na Kristo ni wa Mungu.