< 1 Wakorintho 2 >

1 Nilipokuja kwenu kaka na dada zangu, sikuja kwa maneno ya ushawishi na hekima kama nilivyohubiri kweli iliyofichika kuhusu Mungu.
When I came to you, brothers, I did not come with superiority of speech or wisdom, proclaiming to you the mystery of God.
2 Niliamua kutojua chochote nilipokuwa miongoni mwenu isipokuwa Yesu Kristo, na yeye aliyesulubiwa.
For I determined not to know anything among you, except Jesus (the) Messiah, and him crucified.
3 Na nilikuwa nanyi katika udhaifu, na katika hofu, na katika kutetemeka sana.
When I was with you, I was weak and afraid and I shook.
4 Na ujumbe wangu na kuhubiri kwangu hakukuwa katika maneno ya ushawishi na hekima. Badala yake, yalikuwa katika kumdhihirisha Roho na ya nguvu,
My speech and my preaching were not in persuasive words of wisdom, but in demonstration of the Spirit and of power,
5 ili kwamba imani yenu isiwe katika hekima ya wanadadamu, bali katika nguvu ya Mungu.
that your faith would not rest on human wisdom, but on the power of God.
6 Sasa tunaizungumza hekima miongoni mwa watu wazima, lakini si hekima ya dunia hii, au ya watawala wa nyakati hizi, ambao wanaopita. (aiōn g165)
We speak wisdom, however, among those who are mature, but a wisdom not of this age or of the rulers of this age, who are passing away. (aiōn g165)
7 Badala yake, tunaizungumza hekima ya Mungu katika ukweli uliofichika, hekima iliyofichika ambayo Mungu aliichagua kabla ya nyakati za utukufu wetu. (aiōn g165)
But we speak God's wisdom in a mystery, the wisdom that has been hidden, which God determined in advance before the ages for our glory, (aiōn g165)
8 Hakuna yeyote wa watawala wa nyakati hizi aliyeijua hekima hii, Kama wangeifahamu katika nyakati zile, wasingelimsulubisha Bwana wa utukufu. (aiōn g165)
which none of the rulers of this age has understood. For had they known it, they would not have crucified the Lord of glory. (aiōn g165)
9 Lakini kama ilivyoandikwa, “Mambo mbayo hakuna jicho limeyaona, hakuna sikio lililoyasikia, mawazo hayakufikiri, mambo ambayo Mungu ameyaandaa kwa ajili ya wale wampendao yeye.”
But as it is written, No eye has seen, and no ear has heard, and no mind has imagined the things which God has prepared for those who love him.
10 Haya ni mambo ambayo Mungu ameyafunua kwetu kupitia Roho, Kwa kuwa Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani ya Mungu.
But to us God revealed it through the Spirit. For the Spirit searches all things, even the deep things of God.
11 Kwa kuwa nani afahamuye mawazo ya mtu, isipokuwa roho ya mtu ndani yake? Hivyo pia, hakuna ajuaye mambo ya ndani ya Mungu, isipokuwa Roho wa Mungu.
For what person knows the things of a person except the spirit of the person that is in him? So also, no one knows the things of God except the Spirit of God.
12 Lakini hatukupokea roho ya dunia, lakini Roho ambaye anatoka kwa Mungu, ili kwamba tuweze kujua kwa uhuru mambo tuliyopewa na Mungu.
But we received, not the spirit of the world, but the Spirit which is from God, that we might know the things that were freely given to us by God.
13 Tunasema mambo haya kwa maneno, ambayo hekima ya mtu haiwezi kufundisha, lakini ambayo Roho hutufundisha. Roho hutafasiri maneno ya kiroho kwa hekima ya kiroho.
And we speak of these things, not with words taught by human wisdom, but with those taught by the Spirit, comparing spiritual things with spiritual things.
14 Mtu asiye wa kiroho hapokei mambo ambayo ni ya Roho wa Mungu, kwa kuwa hayo ni upuuzi kwake. Hawezi kuyajua kwa sababu yanatambuliwa kiroho.
Now the natural person does not receive the things of the Spirit of God, for they are foolishness to him, and he cannot understand them, because they are spiritually discerned.
15 Kwa yule wa kiroho huhukumu mambo yote. Lakini huhukumiwa na wengine.
But he who is spiritual discerns all things, and he himself is judged by no one.
16 “Ni nani anaweza kuyajua mawazo ya Bwana, ambaye anaweza kumfundisha yeye?” Lakini tuna mawazo ya Kristo.
For, "Who has known the mind of the Lord? Who will instruct him?" But we have the mind of Messiah.

< 1 Wakorintho 2 >