< 1 Wakorintho 16 >

1 Sasa kuhusu michango kwa ajili ya waumini, kama nilivyo elekeza makanisa ya Galatia, vivyo hivyo mwapaswa kufanya.
En cuanto a la colecta para los santos, según he ordenado a las Iglesias de Galacia, haced también vosotros.
2 Katika siku ya kwanza ya wiki, kila mmoja wenu aweke kitu fulani kando na kukihifadhi, kama muwezavyo. Fanyeni hivyo ili kwamba kusiwe na michango wakati nikija.
El primer día de la semana, cada uno de vosotros ponga aparte para sí lo que sea de su agrado, reservándolo, no sea que cuando llegue yo, se hagan entonces las colectas.
3 Na nitakapofika, yeyote mtakayemchagua, nitamtuma pamoja na barua kutoa sadaka yenu huko Yerusalem.
Y cuando yo haya llegado, a aquellos que vosotros tuviereis a bien, los enviaré con cartas, para que lleven vuestro don a Jerusalén;
4 Na kama ni sahihi kwa mimi kwenda pia, watakwenda pamoja nami.
y si conviene que vaya también yo, irán conmigo.
5 Lakini nitakuja kwenu, wakati ninapitia Makedonia. Kwa kuwa nitapitia Makedonia.
Iré a veros después de recorrer la Macedonia; pues por Macedonia tengo que pasar.
6 Labda naweza kukaa nanyi au hata kumaliza majira ya baridi, ili kwamba muweze kunisaidia katika safari yangu, popote niendako.
Y puede ser que me detenga entre vosotros y aun pase el invierno; para que me despidáis a dondequiera que vaya.
7 Kwa kuwa sitarajii kuwaona sasa kwa muda mfupi. Kwani ninatumaini kukaa nanyi kwa muda fulani, kama Bwana ataniruhusu.
Porque esta vez no quiero veros de paso, y espero permanecer algún tiempo entre vosotros, si el Señor lo permite.
8 Lakini nitakaa Efeso mpaka Pentekoste,
Me quedaré en Éfeso hasta Pentecostés;
9 kwa kuwa mlango mpana umefunguliwa kwa ajili yangu, na kuna maadui wengi wanipingao.
porque se me ha abierto una puerta grande y eficaz, y los adversarios son muchos.
10 Sasa wakati Timotheo akija, muoneni kwamba yuko na ninyi pasipo kuogopa, anafanya kazi ya Bwana, kama ninavyofanya.
Si Timoteo llega, mirad que esté entre vosotros sin timidez, ya que él hace la obra del Señor lo mismo que yo.
11 Mtu yeyote asimdharau. Mumsaidie katika njia yake kwa amani, ili kwamba aweze kuja kwangu. Kwa kuwa ninamtarajia aje pamoja na ndugu.
Que nadie, pues, le menosprecie; despedidle en paz para que venga a mí, porque le estoy esperando con los hermanos.
12 Sasa kuhusiana na ndugu yetu Apolo. Nilimtia moyo sana kuwatembelea ninyi pamoja na ndugu. Lakini aliamua kutokuja kwa sasa. Hata hivyo, atakuja wakati ana nafasi.
En cuanto al hermano Apolo, mucho le encarecí que fuese a vosotros con los hermanos, mas no tuvo voluntad alguna de ir ahora; irá cuando tenga oportunidad.
13 Muwe macho, simameni imara, mtende kama wanaume, muwe na nguvu.
Velad; estad firmes en la fe; portaos varonilmente; confortaos.
14 Basi yote myafanyayo yafanyike katika upendo.
Todas vuestras cosas se hagan con amor.
15 Mnaijua kaya ya Stefana. Mnajua kwamba walikuwa waamini wa kwanza huko Akaya, na kwamba walijiweka wenyewe kwenye huduma ya waumini. Na sasa nawasihi, kaka na dada zangu,
Os exhorto, hermanos —porque conocéis la casa de Estéfanas, que es primicias de Acaya y que se han consagrado al servicio de los santos—,
16 kuweni wanyenyekevu kwa watu kama hao, na kwa kila mtu anayesaidia katika kazi na watenda kazi pamoja nasi.
que también vosotros os pongáis a disposición de ellos y de todo el que colabore y se afane.
17 Na ninafurahi kwa ujio wa Stefana, Fotunato, na Akiko. Wamesimama mahali ambapo ninyi mgepaswa kuwa.
Me regocijo de la llegada de Estéfanas, Fortunato y Acaico; porque ellos han suplido vuestra falta,
18 Kwa kuwa wameifurahisha roho yangu na yenu. Kwa hiyo sasa, watambueni watu kama hawa.
recreando mi espíritu y el vuestro. Estimádselo, pues, a hombres como ellos.
19 Makanisa ya Asia wametuma salamu kwenu. Akila na Priska wanawasalimu katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko nyumbani kwao.
Os saludan las Iglesias de Asia. Os mandan muchos saludos en el Señor, Aquila y Prisca, junto con la Iglesia que está en su casa.
20 Kaka na dada zangu wote wanawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.
Os saludan todos los hermanos. Saludaos unos a otros en ósculo santo.
21 Mimi, Paulo, naandika hivi kwa mkono wangu.
Va la salutación de mi propio puño: Pablo.
22 Kama yeyote hampendi Bwana, basi laana iwe juu yake. Bwana wetu, njoo!
Si alguno no ama al Señor, sea anatema. ¡Maran-atha!
23 Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi.
La gracia del Señor Jesús sea con vosotros.
24 Upendo wangu uwe pamoja nanyi katika Kristo Yesu.
Mi amor está con todos vosotros, en Cristo Jesús.

< 1 Wakorintho 16 >