< 1 Wakorintho 13 >

1 Tuseme kwamba ninanena kwa lugha za wanadamu na za malaika. Lakini kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo au upatu uvumao.
Tujovaghe kuuti ku njovele isa vaanhu kange njovele isa vanyamola. Looli nambe nilinsila lughano, nilishaba jino jikuta nambe iking'ola kino kikujila.
2 Na kwamba nina karama ya unabii na ufahamu wa kweli zilizofichika na maarifa, na kwamba ninayo imani ya kuhamisha milima. Lakini ikiwa sina upendo, mimi si kitu.
Nakuuti nilinikipelua ikya vuviili nhuvukagusi vwa kyang'haani vuno vufisime nuvukagusi, nakuuti nilinilwitiko ulwakuhamia ifidunda. Looli nave nilinsila ulughano, une na kyekiinu.
3 Na tuseme kwamba ninatoa milki yangu yote na kuwalisha masikini, na kwamba ninautoa mwili wangu ili nichomwe moto. Lakini kama sina upendo, hainifaidii kitu.
Pe tujove kuuti nihumia kutema kulyumue na kukuvalasia avakotofu, na kuuti nihumia um'bili ghwango ninyanyue nu mwooto. Looli nave nilinsila lughano, nanikwambula kimonga.
4 Upendo huvumilia na hufadhili. Upendo haujisifu au kujivuna. Hauna kiburi
Ulughano lukuguda kange lulinulutango. Ulughano nalukughinia kange nalukupula. Ghulinsila matingo
5 au ukorofi. Hautafuti mambo yake, hauoni uchungu haraka, wala hauhesabu mabaya.
nambe umovesi. naghulonda amasio ghaghene, nalukujagha uvuvafi vwa ng'aning'ani, nambe naluvalila amavivi.
6 Haufurahii udhalimu. Badala yake, hufurahi katika kweli.
Naluhovoka uvuvotevote. Apene looli luhovoka nuvwa kyang'haani.
7 Upendo huvumilia mambo yote; huamini mambo yote, una ujasiri katika mambo yote, na hustahimili mambo yote.
Ulughano lukughana amasio ghoni; lukwitika amasio ghoni, lulinulukangasio mumasio ghooni, kange lunoghile amasio ghoni.
8 Upendo haukomi. Ikiwa kuna unabii, wote utapita. Ikiwa kuna lugha, zitakoma. Ikiwa kuna maarifa, yatapita.
Ulughano naludugha. Nave kwevule uvu viili, lwoni lukiling'ania. Nave kwejile injovele, sidughaghe. Nave kwevule uvu mang'anyi vukiling'ania.
9 Kwa kuwa tunajua kwa sehemu na tunafanya unabii kwa sehemu.
Ulwakuva tukagule lubale kange tuvomba uvuviili lubale.
10 Lakini ijapo ile iliyo kamili, ile isiyo kamili itapita.
Looli luliva lukwisa luno lukiline, lula luno nalukwiline lukiling'ania.
11 Nilipokuwa mtoto, nilisema kama mtoto, nilifikiri kama mtoto, niliamua kama mtoto. Nilipokuwa mtu mzima, niliweka mbali nami mambo ya kitoto.
Pano nilyale mwana, nikajovagha ndavule umwana, nikasaghile ndavule umwana, nikalamulagha ndavule umwana. pano nilyale muunhu n'goyo, nilyaghavikile kutaali nune ghoni ghaala agha kijana.
12 Kwa kuwa sasa tunaona kama kwa kioo, kama sura gizani, lakini wakati ule tutaona uso kwa uso. Sasa ninajua kwa sehemu, lakini wakati ule nitajua sana kama na mimi ninavyojulikana sana.
Ulwakuva lino tulola heene ni kilolelo, heene sura ku ng'isi, looli unsiki ghula tulolagha maso kwa maso. Lino nikagwile lubale, looli unsiki ghula nilakagula kyongo ndavule najune nikagulike kyongo.
13 Lakini sasa mambo haya matatu yanadumu: imani, tumaini lijalo, na upendo. Lakini lililo kuu zaidi ya haya ni upendo.
Looli lino agha gha tatu ghali nhi danda: lwitiko, uluhumilo luno lukwisa, nulughano. Loolibilivaha kyongo kukila iisi lwe lughano.

< 1 Wakorintho 13 >