< 1 Wakorintho 11 >
1 Nifuateni mimi, kama na mimi ninavyomfuata Kristo.
Bądźcie naśladowcami moimi, jakom i ja Chrystusowy;
2 Sasa nawasifu kwasababu ya vile mnavyonikumbuka katika mambo yote. Nawasifu kwasababu mmeyashika mapokeo kama nilivyoyaleta kwenu.
A chwalę was, bracia! iż pamiętacie wszystkie moje nauki, a jakom wam podał, podania trzymacie.
3 Basi nataka mfahamu ya kuwa Kristo ni kichwa cha kila mwanaume, naye mwanaume ni kichwa cha mwanamke, na ya kuwa Mungu ni kichwa cha Kristo.
A chcę, abyście wiedzieli, iż każdego męża głową jest Chrystus, a głową niewiasty mąż, a głową Chrystusową Bóg.
4 Kila mwanaume aombaye au atoae unabii akiwa amefunika kichwa anakiabisha kichwa chake.
Każdy mąż, gdy się modli albo prorokuje z przykrytą głową, szpeci głowę swoję.
5 Lakini kila mwanamke aombae au kutoa unabii hali kichwa chake kikiwa wazi anakiaibisha kichwa chake. Kwa maana ni sawa sawa na kama amenyolewa.
I każda niewiasta, gdy się modli albo prorokuje, nie nakrywszy głowy swojej, szpeci głowę swoję; boć to jedno, a toż samo jest, jakoby ogolona była.
6 Ikiwa kama mwanamke hatafunika kichwa chake, na akatwe nywele zake ziwe fupi. Maana ikiwa ni aibu mwanamke kukata nywele zake au kunyolewa, basi afunike kichwa chake.
Albowiem jeźli się nie nakrywa niewiasta, niechże się też strzyże; a jeźli szpetna rzecz jest niewieście, strzyc się albo golić, niechże się nakrywa.
7 Kwani haimpasi mwanamume kufunika kichwa chake, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.
Albowiem mąż nie ma nakrywać głowy, gdyż jest wyobrażeniem i chwałą Bożą; ale niewiasta jest chwałą mężową.
8 Maana mwanamume hakutokana na mwanamke. Bali mwanamke alitokana na mwanamume.
Bo mąż nie jest z niewiasty, ale niewiasta z męża.
9 Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke. Bali mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanamume.
Albowiem mąż nie jest stworzony dla niewiasty, ale niewiasta dla męża.
10 Hii ndio sababu mwanamke anapaswa kuwa na ishara ya mamlaka juu ya kichwa chake, kwa sababu ya malaika.
A przetoż niewiasta powinna mieć władzę na głowie dla Aniołów.
11 Hata hivyo, katika Bwana, mwanamke hayupo peke yake pasipo mwanamume, au mwanamume pasipo mwanamke.
A wszakże mąż nie jest bez niewiasty, ani niewiasta nie jest bez męża w Panu.
12 Maana kama vile mwanamke alitoka kwa mwanamume, vile vile mwanamume alitoka kwa mwanamke. Na vitu vyote hutoka kwa Mungu.
Albowiem jako niewiasta z męża jest, tak też mąż przez niewiastę; jednak wszystkie rzeczy są z Boga.
13 Hukumuni wenyewe: Je! ni sahihi mwanamke amuombe Mungu hali kichwa chake kikiwa wazi?
Sami u siebie rozsądźcie, przystoili niewieście bez nakrycia modlić się Bogu?
14 Je hata asili peke yake haiwafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?
Azaż was i samo przyrodzenie nie uczy, iż mężowi, gdyby włosy zapuszczał, jest mu ku zelżywości?
15 Je asili haiwafundishi ya kwamba mwanamke akiwa na nywele ndefu ni utukufu kwake? Maana amepewa zile nywele ndefu kama vazi lake.
Ale niewiasta, jeźli zapuszcza włosy, jest jej ku poczciwości, przeto iż jej włosy dane są za przykrycie.
16 Lakini ikiwa mtu yeyote anataka kubishana juu ya hili, sisi hatuna namna nyingine, wala makanisa ya Mungu.
A jeźliby się kto zdał być swarliwym, my takiego obyczaju nie mamy, ani zbory Boże.
17 Katika maagizo yafuatayo, mimi siwasifu. Maana mnapokusanyika, sio kwa faida bali kwa hasara.
A to opowiadając nie chwalę, że się nie ku lepszemu, ale ku gorszemu schodzicie.
18 Maana kwanza, nasikia ya kuwa mkutanikapo kanisani, kuna migawanyiko kati yenu, na kwa sehemu ninaamini.
Albowiem najprzód, gdy się wy schodzicie we zborze, słyszę, iż rozerwania bywają między wami, i poniekąd wierzę.
19 Kwa maana ni lazima iwepo misuguano kati yenu, ili kwamba wale waliokubaliwa wajulikane kwenu.
Bo muszą być kacerstwa między wami, aby ci, którzy są doświadczeni, byli jawnymi między wami.
20 Kwa maana mkutanikapo, mnachokula sio chakula cha Bwana.
Gdy się wy tedy wespół schodzicie, nie jest to używać wieczerzy Pańskiej.
21 Mnapokula, kila mmoja hula chakula chake mwenyewe kabla wengine hawajala. hata huyu ana njaa, na huyu amelewa.
Albowiem każdy wieczerzę swoję pierwej zjada i jeden łaknie, a drugi jest pijany.
22 Je hamna nyumba za kulia na kunywea? Je mnalidharau kanisa la Mungu na kuwafedhehesha wasio na Kitu? Niseme nini kwenu? Niwasifu? Sitawasifu katika hili!
Azaż domów nie macie do jedzenia i do picia? Albo zborem Bożym gardzicie i zawstydzacie tych, którzy nie mają? Cóż wam rzekę? Pochwalęż was? W tem nie chwalę.
23 Maana nilipokea kutoka kwa Bwana kile ambacho nimewapa ninyi ya kuwa Bwana Yesu, usiku ule aliposalitiwa, alichukua mkate.
Albowiem jam wziął od Pana, com też wam podał, iż Pan Jezus tej nocy, której był wydan, wziął chleb,
24 Baada ya kushukuru, aliuvunja na kusema, “Huu ndio mwili wangu, ulio kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi.”
A podziękowawszy, złamał i rzekł: Bierzcie, jedzcie; to jest ciało moje, które za was bywa łamane; to czyńcie na pamiątkę moję.
25 Na vivi hivi akachukua kikombe baada ya kula, na kusema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi mara nyingi kila mywapo, kwa kunikumbuka mimi.”
Także i kielich, gdy było po wieczerzy mówiąc: Ten kielich jest nowy testament we krwi mojej; to czyńcie, ilekroć pić będziecie, na pamiątkę moję
26 Kwa kila muda mlapo mkate huu na kukinywea kikombe, mwaitangaza mauti ya Bwana mpaka atakapokuja.
Albowiem ilekroć byście jedli ten chleb i ten kielich byście pili, śmierć Pańską opowiadajcie, ażby przyszedł.
27 Kwa hiyo, kila aulaye mkate au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.
A tak, kto by jadł ten chleb, albo pił ten kielich Pański niegodnie, będzie winien ciała i krwi Pańskiej.
28 Mtu ajihoji mwenyewe kwanza, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.
Niechże tedy człowiek samego siebie doświadczy, a tak niech je z chleba tego i z kielicha tego niechaj pije.
29 Maana alaye na kunywa bila kuupambanua mwili, hula na kunywa hukumu yake mwenyewe.
Albowiem kto je i pije niegodnie, sąd sobie samemu je i pije, nie rozsądzając ciała Pańskiego.
30 Hii ndiyo sababu watu wengi kati yenu ni wagonjwa na dhaifu, na baadhi yenu wamekufa.
Dlatego między wami wiele jest słabych i chorych, i niemało ich zasnęło.
31 Lakini tukijichunguza wenyewe hatutahukumiwa.
Bo gdybyśmy się sami rozsądzali, nie bylibyśmy sądzeni.
32 Ila tunapohukumiwa na Bwana, twarudiwa, ili tusije tukahukumiwa pamoja na dunia.
Lecz gdy sądzeni bywamy, od Pana bywamy ćwiczeni, abyśmy z światem nie byli potępieni.
33 Kwa hiyo, kaka na dada zangu, mkutanikapo mpate kula, ngojeaneni.
Ale tak, bracia moi! gdy się schodzicie ku jedzeniu, oczekiwajcie jedni drugich.
34 Mtu akiwa na njaa, na ale nyumbani kwake, ili kwamba mkutanikapo pamoja isiwe kwa hukumu. Na kuhusu mambo mengine mliyoandika, nitawaelekeza nitakapokuja.
A jeźli kto łaknie, niechże je w domu, abyście się na sąd nie schodzili. A inne rzeczy, gdy przyjdę, postanowię.