< 1 Wakorintho 10 >
1 Nataka ninyi mjue kaka na dada zangu, ya kuwa baba zetu walikuwa chini ya wingu na wote walipita katika bahari.
And I do not wish you to be ignorant, brothers, that all our fathers were under the cloud, and all passed through the sea,
2 Wote walibatizwa wawe wa Musa ndani ya wingu na ndani ya bahari,
and all were immersed into Moses in the cloud, and in the sea;
3 na wote walikula chakula kile kile cha roho.
and all ate the same spiritual food,
4 Wote walikunywa kinywaji kile kile cha roho. Maana walikunywa kutoka katika mwamba wa roho uliowafuata, na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
and all drank the same spiritual drink, for they were drinking of a spiritual rock following them, and the rock was the Christ;
5 Lakini Mungu hakupendezwa sana na wengi wao, na maiti zao zilisambazwa jangwani.
but in the most of them God was not well pleased, for they were strewn in the wilderness,
6 Basi mambo haya yote yalikuwa mifano kwetu, ili sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya kama na wao walivyofanya.
and those things became types of us, for our not passionately desiring evil things, as also these desired.
7 Msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa. Hii ni kama ilivyoandikwa, “Watu walikaa chini wakila na kunywa, na waliinuka kucheza kwa tamaa za mapenzi.”
Neither become idolaters, as certain of them, as it has been written: “The people sat down to eat and to drink, and stood up to play”;
8 Tusifanye uasherati kama wengi wao walivyofanya. Wakafa siku moja watu ishirini na tatu elfu kwa sababu hiyo.
neither may we commit whoredom, as certain of them committed whoredom, and there fell in one day twenty-three thousand;
9 Wala tusimjaribu Kristo, kama wengi wao walivyofanya na wakaharibiwa kwa nyoka.
neither may we tempt the Christ, as also certain of them tempted, and perished by the serpents;
10 Na pia msinung'unike, kama wengi wao walivyonung'unika na kuharibiwa na malaika wa mauti.
neither murmur, as also some of them murmured, and perished by the destroyer.
11 Basi mambo hayo yalitendeka kama mifano kwetu. Yakaandikwa ili kutuonya sisi - tuliofikiliwa na miisho ya zamani. (aiōn )
And all these things happened to those persons as types, and they were written for our admonition, to whom the end of the ages came, (aiōn )
12 Kwa hiyo kila ajionaye amesimama awe makini asije akaanguka.
so that he who is thinking to stand—let him observe, lest he fall.
13 Hakuna jaribu lililowapata ninyi lisilo kawaida ya wanadamu. Ila Mungu ni mwaminifu. Hatawaacha mjaribiwe kupita uwezo wenu. Pamoja na jaribu yeye atawapa mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
No temptation has taken you—except that of man; and God is faithful, who will not permit you to be tempted above what you are able, but He will make, with the temptation, also the outlet, for your being able to bear [it].
14 Kwa hiyo, wapendwa wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.
For this reason, my beloved, flee from the idolatry;
15 Nasema nanyi kama watu wenye akili, ili muamue juu ya ninalosema.
as to wise men I speak—judge what I say.
16 Kikombe cha baraka tubarikicho, si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?
The cup of the blessing that we bless—is it not the fellowship of the blood of the Christ? The bread that we break—is it not the fellowship of the body of the Christ?
17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja. Sisi sote twapokea mkate mmoja kwa pamoja.
Because one bread, one body, are we the many—for we all partake of the one bread.
18 Watazameni watu wa Israeli: Je! Wale wote walao dhabihu si washiriki katika madhabahu?
See Israel according to the flesh! Are those not eating the sacrifices in the fellowship of the altar?
19 Nasema nini basi? Ya kuwa sanamu ni kitu? Au ya kuwa chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu?
What do I say then? That an idol is anything? Or that a sacrifice offered to an idol is anything?
20 Lakini nasema juu ya vitu vile wavitoavyo sadaka watu wapagani wa Mataifa, ya kuwa wanatoa vitu hivi kwa mapepo na sio kwa Mungu. Nami sitaki ninyi kushirikiana na mapepo!
[No, ] but that the things that the nations sacrifice—they sacrifice to demons and not to God; and I do not wish you to come into the fellowship of the demons.
21 Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mapepo. Hamwezi kuwa na ushirika katika meza ya Bwana na katika meza ya mapepo.
You are not able to drink the cup of the LORD and the cup of demons; you are not able to partake of the table of the LORD and of the table of demons;
22 Au twamtia Bwana wivu? Tuna nguvu zaidi yake?
do we arouse the LORD to jealousy? Are we stronger than He?
23 “Vitu vyote ni halali,” lakini si vyote vifaavyo. “Vitu vyote ni halali,” lakini si vyote viwajengavyo watu.
All things are lawful to me, but not all things are profitable; all things are lawful to me, but not all things build up;
24 Hakuna hata mmoja angetafuta mazuri yake tu. Badala yake, kila mmoja angetafuta mazuri ya mwenzake.
let no one seek his own—but each another’s.
25 Mnaweza kula kila kitu kiuzwacho sokoni bila kuuliza -uliza kwa ajili ya dhamiri.
Eat whatever is sold in the meat-market, not inquiring, because of the conscience,
26 Maana “dunia ni mali ya Bwana, na vyote viijazavyo.”
for the earth and its fullness [are] the LORD’s;
27 Na mtu asiyeamini akiwaalika kula, na mnataka kwenda, kuleni chochote awapacho pasipo kuuliza maswali ya dhamiri.
and if anyone of the unbelieving calls you, and you wish to go, eat all that is set before you, inquiring nothing, because of the conscience;
28 Lakini mtu akiwaambia, “Chakula hiki kimetokana na sadaka ya wapagani,” msile. Hii ni kwa ajili yake aliyewaambia, na kwa ajili ya dhamiri.
and if anyone may say to you, “This is a thing sacrificed to an idol,” do not eat, because of that one who showed [it], and of the conscience, for the LORD’s [is] the earth and its fullness:
29 Nami simaanishi dhamiri zenu, bali dhamiri ya yule mwingine. Maana kwanini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?
and conscience, I say, not of yourself, but of the other, for why [is it] that my liberty is judged by another’s conscience?
30 Ikiwa mimi natumia chakula kwa shukrani, kwanini nitukanwe kwa kitu ambacho nimeshukuru kwacho?
And if I partake thankfully, why am I spoken of [as] evil, for that for which I give thanks?
31 Kwa hiyo, chochote mnachokula au kunywa, au chochote mfanyacho, fanyeni yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
Whether, then, you eat, or drink, or do anything, do all to the glory of God;
32 Msiwakoseshe Wayahudi au Wayunani, au kanisa la Mungu.
become offenseless, both to Jews and Greeks, and to the Assembly of God;
33 Jaribuni kama mimi ninavyojaribu kuwapendeza watu wote kwa mambo yote. Sitafuti faida yangu mwenyewe, bali ya wengi. Nami nafanya hivi ili wapate kuokolewa.
as I also please all in all things, not seeking my own profit, but that of many—that they may be saved.