< 1 Nyakati 7 >

1 Isiakari alikuwa na wana wanne Tola, Pua, Yashubi, na Shimironi.
Quant aux descendants d’Issachar, c’étaient: Tola, Poua, Yachoub et Chimron, soit quatre.
2 Wana wa Tola walikuwa Uzi, Refaia, Yerie, Yamai, Ibisami, Shemueli. Walikua vichwa katika nyumba za baba yao, toka uzao wa Tola na waliorodheshwa kama mashujaa hodari miongoni mwa kizazi chao. Katika siku za Daudi walikua na idadi ya 22, 600.
Les fils de Tola furent Ouzzi, Refaïa, Yeriël, Yahmaï, Yibsam et Samuel. C’Étaient les chefs des familles de Tola, tous guerriers, selon leurs généalogies. Leur nombre était, au temps de David, de vingt-deux mille six cents.
3 Mwana wa Uzi alikua Izrahia. Mwana wake alikua Michaeli, Obadia, Yoeli, na Ishia, wote watano walikua viongozi wa ukoo
Fils d’Ouzzi: Yizrahia. Fils de Yizrahia: Mikhaël, Obadia, Joël, Yichia, chefs tous les cinq.
4 Pamoja nao walikua na jeshi la watu elfu thelathini na sita kwa mapambano, Kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao, kwa kuwa walikuwa na wake wengi pamoja na wana.
Ils devaient fournir, suivant leurs généalogies, d’après leurs familles, des troupes de gens de guerre au nombre de trente-six mille hommes, car ils avaient un nombre considérable de femmes et d’enfants.
5 Kaka zao, kabila la Isakari, walikua na wanaume wa vita themanini na saba, kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao.
Quant à leurs frères, en comptant toutes les familles d’Issachar, ils fournissaient, en fait de guerriers, quatre-vingt-sept mille hommes, d’après le recensement global.
6 Wana watatu wa Benjamini walikuwa Bela, Beka, na Yediaeli.
Benjamin: Béla, Békher, Yedïaêl, soit trois.
7 Wana watano wa Bela walikuwa Ezibono, Uzi, Uzieli, Yerimoti, na Iri. Walikua ni wanajeshi na waanzilishi wa koo. Watu wao walikuwa na idadi ya wanaume wa vita 22, 034, kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao.
Les fils de Béla furent Eçbôn, Ouzzi, Ouzziël, Yerimot et Iri, tous les cinq, chefs de familles, hommes de guerre. Leur rôle généalogique donnait le chiffre de vingt-deux mille trente-quatre.
8 Wana wa Beka walikuwa Zemira, Yoashi, Elieza, Elionai, Omri, Yeremoti, Abiya, Anatoti, na Alemeti. Wote hawa walikuwa wana wake.
Les fils de Békher étaient: Zemira, Yoach, Eliézer, Elyoênaï, Omri, Yerêmot, Abiyya, Anatot et Alémet, tous fils de Békher.
9 Orodha ya koo zao ilikua na idadi ya 20, 200 viongozi wa familia na wanaume wa vita.
Le rôle généalogique des chefs de leurs familles, tous guerriers, donnait un chiffre de vingt-deux mille deux cents.
10 Mwana wa Yediaeli alikuwa Bilhani. Wana wa Bilhani walikuwa Yeushi, Benjamini, Ehudi, Kenaana, Zetani, Tarishishi, na Ahishahari.
Fils de Yedïaêl: Bilhân. Fils de Bilhân: Yeouch, Benjamin, Ehoud, Kenaana, Zétân, Tarchich, et Ahichahar.
11 Wote hawa waikuwa wana wa Yediaeli. Waliorodheshwa katika ukoo orodha ilikuwa 17, 200 viongozi na wanaume wa vita imara kwa kazi ya jeshi.
Tous ces descendants de Yedïaêl étaient chefs de clans et hommes de guerre. Ils fournissaient dix-sept mille deux cents soldats pour l’armée.
12 (Shupimu na Hupimu walikuwa wana wa Iri, na Hushimu alikuwa mwana wa Aheri.)
Chouppim et Houppim étaient descendants de Ir, et Houchim ceux d’un autre.
13 Wana wa Naftali walikuwa Yazieli, Guni, Yezeri, na Shalumu. Hawa walikuwa wajukuu wa Bilhahi.
Les fils de Nephtali étaient Yahciêl, Gouni, Yécer, Challoum, fils de Bilha.
14 Manasse alikua na mtoto wa kiume aliitwa Asrieli, Ambaye suria wake wa Kiaramia alimzalia. Pia alimzaa na Makiri, baba wa Gileadi.
Les fils de Manassé étaient Asriêl, qu’enfanta sa concubine araméenne. Elle lui donna aussi Makhir, le père de Ghilad.
15 Makiri alimchukua mke wake kutoka Hupite na Shupite. Jina la dada yake lilikuwa Maaka. Mwingine wa uzao wa Manasse alikuwa Zalofehadi, ambaye alikuwa na mabinti pekee.
Makhir prit femme parmi les Houppim et les Chouppim. Le nom de sa sœur était Maakha, et le nom du second Celofhad; celui-ci n’eut que des filles.
16 Maaka mke wa Makiri, alimzaa mwana na alimuita Pereshi. Kaka yake aliitwa Shereshi, na wana wake walikuwa Ulamu na Rakemu.
Maakha, femme de Makhir, enfanta un fils qu’elle appela Pérech. Le frère de celui-ci fut Chérech et ses fils: Oulam et Rékem.
17 Mwana wa Ulami alikuwa Bedani. Hawa walikuwa uzao wa Gileadi mwana wa Makiri mwana wa Manase.
Fils d’Oulam: Bedân. Tels furent les descendants de Ghilad, fils de Makhir, fils de Manassé.
18 Dada wa Gileadi Hamoleketi alimzaa Ishihodi, Abi Ezeri, na Mahila.
Sa sœur, la Reine, enfanta Ichhod, Abiézer et Mahla.
19 Wana wa Shemida walikuwa Ahiana, Shekemu, Liki, na Aniamu.
Les fils de Chemida furent: Ahyvân, Chékhem, Likhi et Anïâm.
20 Uzao wa Efraimu ulikuwa kama ifuatavyo: Efraimu mwana wa Shutela. Shutela mwana wa Beredi. Beredi mwana wa Tahati.
Descendants d’Ephraïm: Choutélah. Celui-ci eut pour fils Béred, celui-ci Tahat, celui-ci Eleada, celui-ci Tahat,
21 Tahati mwana wa Eleada. Eleada mwana wa Shutela. (Eza na Eleadi waliuawa na wanaume wa Gati, wenyeji wa nchi, walipoenda kuiba mifugo yao.
celui-ci Zabad, celui-ci Choutélah, celui-ci Ezer et Elead. Ils furent tués par les gens de Gath, nés dans le pays, pour être descendus razzier leurs troupeaux.
22 Efraimu baba yao aliomboleza kwa siku nyingi, na kaka zake walikuja kumfariji.
Ephraïm, leur père, fut en deuil de longs jours, et ses frères vinrent pour le consoler.
23 Alilala na mkewe. Akapata mimba akamzaa mwana. Efraimu akamuita Beria, kwa sababu maafa yalishakuja nyumbani mwake.
Puis il eut commerce avec sa femme; celle-ci conçut et enfanta un fils. Il lui donna pour nom: Berïa, parce que le malheur était entré dans sa maison.
24 Binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga miji juu na chini Beth Horon na Uzzen Sheerah.)
Sa fille Chééra bâtit Beth-Horôn inférieur et supérieur, et Ouzzên Chééra.
25 Mwana wake alikuwa Rafa. Mwana wa Rafa alikuwa Reshefi. Mwana wa Reshafi alikuwa Tela. Mwana wa Tela alikuwa Tahani.
Berïa eut pour fils Réfah, celui-ci Réchef, celui-ci Télah, celui-ci Tahan,
26 Mwana wa Tahani alikuwa Ladani. Mwana wa Ladani alikuwa Amihudi. Mwana wa Amihudi alikuwa Elishama.
celui-ci Ladân, celui-ci Amihoud, celui-ci Elichama,
27 Mwana wa Elishama alikuwa Nuni. Mwana wa Nuni alikuwa Joshua.
celui-ci Nôn, celui-ci Josué.
28 Mali zao na makazi yao yalikuwa Betheli na yalizungukwa na vijiji. Waliongeza upande wa mashariki hadi Naarani na upande wa magharibi hadi Gezeri na vijiji vyake, na Shekemu na vijiji vyake hadi Aya na vijiji vyake.
Leur patrimoine et leurs établissements étaient à Béthel, avec sa banlieue, à l’est Naarân, à l’ouest Ghézer avec sa banlieue, Sichem avec sa banlieue, jusqu’à Ayya et sa banlieue.
29 Katika mipaka pamoja na Manasse kulikuwa na Beti shani na vijiji vyake, Taanaki na vijiji vyake, Megido na vijiji vyake, na Dori na vijiji vyake. Katika huu mji waliishi uzao wa Josefu mwana wa Israeli.
Au pouvoir des fils de Manassé étaient tombés Beth-Cheân et sa banlieue, Taanakh et sa banlieue, Meghiddo et sa banlieue, Dor et sa banlieue. C’Est dans ces villes que s’établirent les descendants de Joseph, fils d’Israël.
30 Wana wa Asha walikuwa Imna, Ishiva, Ishivi, na Beria. Sera alikuwa dada yao.
Fils d’Aser: Yimna, Yichva, Yichvi, Berïa, et Sérah leur sœur.
31 Wana wa Beria walikuwa Heberi na Malchieli, Ambaye alikuwa baba wa Birzaiti.
Fils de Berïa: Héber et Malkiêl. Celui-ci fut le "père" de Birzavit;
32 Wana wa Heberi walikuwa Yafeti, Shomer, na Hotamu. dada yao alikuwa Shua.
Héber engendra Yaflêt, Chômer, Hotâm et Choua leur sœur.
33 Wana wa Yafeti walikuwa Pasach, Bimhali, na Ashivati. hawa walikuwa watoto wa yafeti.
Les fils de Yaflêt furent Passakh, Bimhal et Activât. Tels furent les fils de Yaflêt.
34 shoma, kaka wa Yafeti alikuwa na wana hawa: Roga, Yehuba, Aram.
Les fils de Chémer: Ahi, Rohga, Houbba et Aram.
35 Kaka yake Shema, Helemu, alikuwa na wana hawa: Zofa, Imna, Sheleshi na Amali.
Fils de Hêlem, son frère: Çofah, Yimna, Chêlech et Amal.
36 Wana wa Zofa walikuwa Sua, Harinefa, Shua, Beri, IMra,
Fils de Çofah: Souah, Harnéfer, Choual, Bêri, Yimra,
37 Beza, Hodi, Shamma, Shilsha, Ithrani, na Beera.
Bécer, Hod, Chamma, Chilcha, Yitrân et Beêra.
38 Wana wa Yeta walikuwa Jefune, Pispa, na Ara.
Fils de Yéter: Yefounné, Pispa et Ara.
39 Wana wa Ulla walikwa Ara, Hannieli, na Rizia.
Fils d’Oulla: Arah, Hanniêl et Ricia.
40 Hawa wote walikuwa uzao wa Asha. Walikua mababu wa ukoo, viongozi wa familia, wananume wa kipekee, wanaume wa vita, na machifu kati ya viongozi. Kulikuwa na wanaume elfu ishirini na sita walioorodheshwa waliokuwa imara kwa kazi ya jeshi, kwa mujibu wa idadi iliyo orodheshwa.
Tous ceux-là étaient descendants d’Aser, chefs des familles, l’élite des hommes de guerre, les premiers parmi les princes, inscrits au rôle de l’armée, et ils fournissaient un contingent de vingt-six mille soldats.

< 1 Nyakati 7 >