< 1 Nyakati 6 >

1 Wana wa Levi walikuwa Gerishoni, Kohathi, na Merari.
Wana wa Lawi walikuwa: Gershoni, Kohathi na Merari.
2 Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Izhari, Hebroni, na Uzieli.
Wana wa Kohathi walikuwa: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
3 Wana wa Amramu walikuwa Aruni, Musa, Miriamu. Wana wa Aruni walikuwa Nadabu, Abihu, Eleazari, na Ithamari.
Amramu alikuwa na wana: Aroni, Mose, na Miriamu. Aroni alikuwa na wana: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
4 Eleazari akawa baba wa Finehasi, na Finehasi akawa baba wa Abishua.
Eleazari akamzaa Finehasi, Finehasi akamzaa Abishua,
5 Abishua akawa baba wa Buki, na Buki akawa baba wa Uzi.
Abishua akamzaa Buki, Buki akamzaa Uzi,
6 Uzi akawa baba wa Zerahia, na Zerahia akawa baba wa Meraioti.
Uzi akamzaa Zerahia, Zerahia akamzaa Merayothi,
7 Meraioti akawa baba wa Amaria, na Amaria akawa baba wa Ahitubi.
Merayothi akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu,
8 Ahitubi akawa baba wa Zadoki, na Zadoki akawa baba wa Ahimazi.
Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Ahimaasi,
9 Ahimazi akawa baba wa Azaria, na Azaria akawa baba wa Yohanani.
Ahimaasi akamzaa Azaria, Azaria akamzaa Yohanani,
10 Yohanani akawa baba wa Azaria, aliye hudumu katika hekalu alilo lijenga Sulemani ndaniya Yerusalemu.
Yohanani akamzaa Azaria (ndiye alifanya kazi ya ukuhani katika Hekalu alilojenga Mfalme Solomoni huko Yerusalemu),
11 Azaria akawa baba wa Amaria, na Amaria akawa baba wa Ahitubi.
Azaria akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu,
12 Ahitubi akawa baba wa Zadoki, na Zadoki akawa baba wa Shalumu.
Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Shalumu,
13 Shalumu akawa baba wa Hilikia, na Hilikia akawa baba wa Azaria.
Shalumu akamzaa Hilkia, Hilkia akamzaa Azaria,
14 Azaria akawa baba Seraia, na Seraia akawa baba wa Yehozadaki.
Azaria akamzaa Seraya, Seraya akamzaa Yehosadaki.
15 Yehozadaki akaenda matekani Yahweh alipo wapeleka utumwani Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Nebukadneza.
Yehosadaki alihamishwa wakati Bwana aliwapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Mfalme Nebukadneza.
16 Wana wa Levi walikuwa Gerishomu, Kohathi, na Merari.
Wana wa Lawi walikuwa: Gershoni, Kohathi na Merari.
17 Wana wa Gerishomu walikuwa Libini na Shimei.
Haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni: Libni na Shimei.
18 Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Izhari, Hebroni, na Uzieli.
Wana wa Kohathi walikuwa: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
19 Wana wa Merari walikuwa Mahili na Mushi. Hawa walikuwa koo za Walawi kwa familia za baba zao.
Wana wa Merari walikuwa: Mahli na Mushi. Zifuatazo ni koo za Walawi zilizoorodheshwa kufuatana na baba zao:
20 Uzao wa Gerishomu ulianza na mwanae Libini. Mwana wa Libini alikuwa Jahathi. Mwanae alikuwa Zima.
Wazao wa Gershoni: Gershoni akamzaa Libni, Libni akamzaa Yahathi, Yahathi akamzaa Zima,
21 Mwanae alikuwa Yoa. Mwanae alikuwa alikuwa Ido. Mwanae alikuwa Zera. Mwanae alikuwa Yeatherai.
Zima akamzaa Yoa, Yoa akamzaa Ido, Ido akamzaa Zera, Zera akamzaa Yeatherai.
22 Uzao wa Kohathi ulianza na mwanae Aminadabu. Mwanae alikuwa Kora. Mwanae alikuwa Asiri.
Wazao wa Kohathi: Kohathi akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Kora, Kora akamzaa Asiri,
23 Mwanae alikuwa Elikana. Mwanae alikuwa Ebiasa. Mwanae alikuwa Asiri.
Asiri akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Ebiasafu, Ebiasafu akamzaa Asiri,
24 Mwanae alikuwa Tahathi. Mwanae alikuwa Urieli. Mwanae alikuwa uzia. Mwanae alikuwa Shauli.
Asiri akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Urieli, Urieli akamzaa Uzia, Uzia akamzaa Shauli.
25 Wana wa Elikana walikuwa Amasai, Ahimothi, na Elikana.
Wazao wa Elikana walikuwa: Amasai na Ahimothi,
26 Mwana wa huyu Elikana wa pili alikuwa Zofai. Mwanae alikuwa Nahathi.
Ahimothi akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Sofai, Sofai akamzaa Nahathi,
27 Mwanae alikuwa Eliabu. Mwanae alikuwa Yehoramu. Mwanae alikuwa Elikana.
Nahathi akamzaa Eliabu, Eliabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Samweli.
28 Wana wa Samwali walikuwa mzaliwa wa kwanza, Yoeli, na Abija, wa pili.
Wana wa Samweli walikuwa: Yoeli mzaliwa wake wa kwanza, na Abiya mwanawe wa pili.
29 Mwana wa Merari alikuwa Mahili. Mwanae alikuwa Libini.
Wafuatao ndio wazao wa Merari: Merari akamzaa Mahli, Mahli akamzaa Libni, Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza,
30 Mwanae alikuwa Shimei. Mwanae alikuwa Uza. Mwanae alikuwa Shimea. Mwanae alikuwa Hagia. Mwana alikuwa Asaia.
Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia, Hagia akamzaa Asaya.
31 Haya ndio majina ya wanaume ambao Daudi waliwaeka kusimamia muziki katika nyumba ya Yahweh, baada ya sanduku kuja hapo.
Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Bwana, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko.
32 Walitumika kwa kuimba mbele ya hema, hema la kukutania, mpaka Sulemani alipo jenga nyumba ya Yahweh ndani ya Yerusalemu. Walikamilisha wajibu wao kwa kadiri ya maelekezo waliopewa.
Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la Bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.
33 Hawa walitumika pamoja na wana wao. Katika makabila ya Wakohathi alitoka Hemani mwana muziki. Babu zake walikuwa hawa, kurudi nyuma ya wakati: Hemani alikuwa mwana wa Yoeli. Yoeli alikuwa mwana wa Samweli.
Wafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao: Kutoka ukoo wa Kohathi walikuwa: Hemani, mpiga kinanda, alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli,
34 Samweli alikuwa mwana wa Elikana. Elikana alikuwa mwana wa Yerohamu. Yerohamu alikuwa mwana wa Elieli. Elieli alikuwa mwana wa Toa.
mwana wa Elikana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elieli, mwana wa Toa,
35 Toa alikuwa mwana wa Zufi. Zufi alikuwa mwana wa Elikana. Elikana alikuwa mwana wa Mahathi. Mahathi alikuwa mwana wa Amasai. Amasai alikuwa mwana wa Elikana.
mwana wa Sufu, mwana wa Elikana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai,
36 Elikana alikuwa mwana wa Yoeli. Yoeli alikuwa mwana wa Azaria. Azaria alikuwa mwana wa Zefania.
mwana wa Elikana, mwana wa Yoeli, mwana wa Azaria, mwana wa Sefania,
37 Zefania alikuwa mwana wa Tahathi. Tahathi alikuwa mwana wa Asiri. Asiri alikuwa mwana wa Ebiasa. Ebiasa alikuwa mwana wa Kora.
mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora,
38 Kora alikuwa mwana wa Izhari. Izhari alikuwa mwana wa Kohathi. Kohathi alikuwa mwana wa Levi. Levi alikuwa mwana wa Israeli.
mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli;
39 Msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliye simama mkono wake wa kuume. Asafu alikuwa mwana Berekia. Berekia alikuwa mwana wa Shimea.
na msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliyesimama mkono wa kuume: Asafu mwana wa Berekia, mwana wa Shimea,
40 Shimea alikuwa mwana Mikaeli. Mikaeli alikuwa mwana wa Baaseia. Baaseia alikuwa mwana wa Malikiya.
mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya,
41 Malikiya alikuwa mwana wa Ethini. Ethini alikuwa mwana wa Zera. Zera alikuwa mwana wa Adaia.
mwana wa Ethni, mwana wa Zera, mwana wa Adaya,
42 Adaia alikuwa mwana wa Ethani. Ethani alikuwa mwana wa Zima. Zima alikuwa mwana wa Shimei.
mwana wa Ethani, mwana wa Zima, mwana wa Shimei,
43 Shimei alikuwa mwana wa Yahathi. Yahathi alikuwa mwana wa Gerishomu. Gerishomu alikuwa mwana wa Levi.
mwana wa Yahathi, mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi.
44 Upande wa mkono wa koshoto wa Hemani walikuwa wasaidizi wake wana wa Merari. Alikuwa Ethani mwana wa Kishi. Kishi alikuwa mwana wa Abdi. Abdi alikuwa mwana wa Maluki.
Na kutoka kwa walioshirikiana nao, Wamerari, mkono wake wa kushoto: Ethani mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki,
45 Maluki alikuwa mwana wa Hashabia. Hashabia alikuwa mwana wa Amazia. Amazia alikuwa mwana wa Hilikia.
mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia,
46 Hilikia alikuwa mwana wa Amzi. Amzi alikuwa mwana wa Bani. Bani alikuwa mwana wa Shemeri.
mwana wa Amsi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri,
47 Shemeri alikuwa mwana wa Mahili. Mahili alikuwa mwana wa Mushi. Mushi alikuwa mwana wa Merari. Merari alikuwa mwana wa Levi.
mwana wa Mahli, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi.
48 Walawi, alipangiwa kufanya kazi zote za hema, nyumba ya Mungu.
Ndugu zao wengine Walawi walipewa huduma nyingine za kuhudumia hema takatifu, nyumba ya Mungu.
49 Aruni na wana wake walitoa sadaka katika madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketeza; na sadaka katika madhabahu ya uvumba kwa kazi zote katika pa patakatifu. Hizi sadaka zilifanya maombezi kwa ajili ya Waisraeli, kwa kadiri ya yote ambayo Musa mtumishi wa Mungu aliwaamuru.
Lakini Aroni na uzao wake ndio waliokuwa na wajibu wa kutoa sadaka katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba pamoja na yote yaliyofanyika pa Patakatifu, wakifanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, sawasawa na yale yote aliyoagiza Mose mtumishi wa Mungu.
50 Uzao wa Aruni una kumbukwa kama ifuatavyo: Mwana wa Aruni alikuwa Eleazari. Mwana Eleazari alikuwa Finehasi. Mwana wa Finehasi alikuwa Abishua.
Hawa ndio waliokuwa wazao wa Aroni: Aroni akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi, Finehasi akamzaa Abishua,
51 Mwana wa Abishua alikuwa Buki. Mwana wa Buki alikuwa Uzi. Mwana wa Buki alikuwa Zerahia.
Abishua akamzaa Buki, Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Zerahia,
52 Mwana wa Zerahia alikuwa Meraiothi. Mwana wa Meraiothi alikuwa Amaria. Mwana wa Amaria alikuwa Ahitubi.
Zerahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu,
53 Mwana wa Ahitubi alikuwa Zadoki. Mwana wa Zadoki alikuwa Ahimazi.
Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Ahimaasi.
54 Hizi ni sehemu ambazo wazao wa Aruni walipangiwa kuishi, wazao wa Aruni ambao walitoka katika koo za Wakohathi (maeneo ya kwanza yalikuwa yao).
Zifuatazo ni sehemu walizopewa ziwe nchi yao kwa ajili ya makazi yao (walipewa wazao wa Aroni waliotoka katika ukoo wa Wakohathi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):
55 Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda na nchi ya malisho,
Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda pamoja na sehemu ya malisho inayouzunguka.
56 lakini maeneo ya mji na vijiji alipewa Kalebu mwana wa Yefune.
Lakini mashamba pamoja na vijiji vilivyouzunguka mji alipewa Kalebu mwana wa Yefune.
57 Kwa wazao wa Aruni waliwapa: Hebroni ( mji wa makimblio), na Libina pamoja na nchi ya malisho, Yatiri, Eshitemoa pamoja na nchi ya malisho,
Kwa hiyo wazao wa Aroni walipewa miji ifuatayo pamoja na eneo la malisho: Hebroni (mji wa makimbilio), Libna, Yatiri, Eshtemoa,
58 Hileni pamoja na nchi ya malisho, na Debiri pamoja na nchi ya malisho.
Hileni, Debiri,
59 Waliwapa uzao wa Aruni: Ashani pamoja na nchi ya malisho na Bethi Shemeshi pamoja na nchi ya malisho;
Ashani, Yuta na Beth-Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho.
60 na kutoka katika kabila la Benjamini walipewa Geba pamoja na nchi ya malisho, Alemethi pamoja na nchi ya malisho, na Anothothi na nchi ya malisho. Jumla ya miji yao ilikuwa kumi na tatu.
Kutoka kabila la Benyamini walipewa Gibeoni, Geba, Alemethi na Anathothi, pamoja na maeneo yake ya malisho. Miji hii kumi na mitatu iligawanywa miongoni mwa koo za Wakohathi.
61 Uzao mwengine wa Kohathi waliwapa kwa sehemu miji kumi kutoka kwa kabila la Manase.
Wazao waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za nusu ya kabila la Manase.
62 Kwa uzao wa Gerishomu kwa koo zao tofauti walipewa miji kumi na tatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri, Naftali, na nusu ya kabila la Manase huko Bashani.
Wazao wa Gershoni, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na mitatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.
63 Kwa uzao wa Merari walipewa miji kumi, kulingana na koo zao, kutoka kwa makabila ya Rubeni, Gadi, na Zebuluni.
Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.
64 Hivyo watu wa Israeli walitoa hii miji pamoja na nchi za malisho kwa Walawi.
Kwa hiyo Waisraeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yake ya malisho.
65 Walitoa kwa sehemu miji iliyo tajwa awali kutoka katika kabila la Yuda, Simeoni, na Benjamini.
Kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini walipewa miji iliyotajwa hapo juu.
66 Kwa baadhi ya koo za Wakohathi walitoa miji kutoka kwa kabila la Efraimu.
Baadhi ya koo za Wakohathi walipewa kama nchi yao miji kutoka kabila la Efraimu.
67 Waliwapa: Shekemu ( mji wa makimbilio) pamoja na nchi ya malisho katika milima ya Efraimu, Gezeri na nchi ya malisho,
Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji wa makimbilio) na Gezeri,
68 Jokimeamu pamoja na nchi ya malisho, Bethi Horoni pamoja na nchi ya malisho,
Yokmeamu, Beth-Horoni,
69 Aiyaloni pamoja na nchi ya malisho, na Gathi Rimoni pamoja na nchi ya malisho.
Aiyaloni na Gath-Rimoni, pamoja na maeneo yake ya malisho.
70 Nusu ya kabila la Manase waliwapa Wakohathi: Aneri pamoja na nchi ya malisho na Bileamu pamoja na nchi ya malisho. Hizi zikawa mali za koo za Wakohathi.
Kutoka nusu ya kabila la Manase, Waisraeli waliwapa koo za Wakohathi waliobaki miji ya Aneri na Bileamu pamoja na maeneo yake ya malisho.
71 Kwa uzao wa Gerishomu kutoka koo za nusu ya kabila la Manase, waliwapa: Golani huko Baashani na nchi ya malisho na Ashitarothi pamoja na nchi ya malisho.
Wagershoni walipokea miji ifuatayo pamoja na maeneo yake ya malisho: Katika nusu ya kabila la Manase: walipewa Golani katika Bashani na pia Ashtarothi.
72 Kabila la Isakari liliwapa uzao wa Gerishomu: Kedeshi pamoja na nchi ya malisho, Dabera pamoja na nchi ya malisho,
Kutoka kabila la Isakari walipokea Kedeshi, Daberathi,
73 Ramothi pamoja na nchi ya malisho, na Anemu pamoja na nchi ya malisho.
Ramothi na Anemu, pamoja na maeneo yake ya malisho.
74 Isakari alipokea kutoka kwa kabila la Asheri: Mashali pamoja na nchi ya malisho, Abdoni pamoja na nchi ya malisho,
Kutoka kabila la Asheri walipokea Mashali, Abdoni,
75 Hukoki pamoja na nchi ya malisho, na Rehobu pamoja na nchi ya malisho.
Hukoki na Rehobu, pamoja na maeneo yake ya malisho.
76 Walipokea kutoka kabila la Naftali: Kedeshi iliyo Galileya pamoja na nchi ya malisho, Hamoni pamoja na nchi ya malisho, na Kiriathaimu pamoja na nchi ya malisho.
Kutoka kabila la Naftali walipokea Kedeshi katika Galilaya, Hamoni na Kiriathaimu pamoja na maeneo yake ya malisho.
77 Kwa Walawi wengine, uzao wa Merari, walipewa kutoka kabila la Zebuluni: Rimono pamoja na nchi ya malisho na Tabori pamoja na nchi ya malisho.
Wamerari (Walawi waliobakia) walipokea miji ifuatayo: kutoka kabila la Zabuloni walipokea Yokneamu, Karta, Rimoni na Tabori pamoja na maeneo yake ya malisho.
78 Kwa wao pia walipewa, upande wa pili wa Yordani huko Yeriko, kwa upande wa mashariki mwa mto: Bezeri katika jangwa pamoja na nchi ya malisho, Yahzahi pamoja na nchi ya malisho,
Kutoka kabila la Reubeni, ngʼambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko walipokea Bezeri ulioko jangwani, Yahasa,
79 Kedemothi pamoka na nchi ya malisho, ma Mefathi pamoja na nchi ya malisho. Hizi zilitolewa kutoka kabila la Rubeni.
Kedemothi na Mefaathi pamoja na maeneo yake ya malisho.
80 Walawi walipokea kutoka kabila la Gadi: Ramothi ya Gileadi pamoja na nchi ya malisho, Mahanaimu pamoja na nchi ya malisho,
Na kutoka kabila la Gadi walipokea Ramothi huko Gileadi, Mahanaimu,
81 Heshiboni pamoja na nchi ya malisho, na Yazeri pamoja na nchi ya malisho.
Heshboni na Yazeri, pamoja na maeneo yake ya malisho.

< 1 Nyakati 6 >