< 1 Nyakati 5 >
1 Wana wa Rubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli - sasa Rubeni alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Israeli, lakini haki yake ya mzaliwa wa kwanza ilipewa kwa wana wa Yusufu mwana wa Israeli kwa sababu Rubeni alinajisi kochi la baba yake. Hivyo hajanakiliwa kama mwana wa kwanza.
2 Yuda alikuwa mwenye nguvu kuliko kaka zake, na kiongozi ata toka kwake. Lakini haki ya mzaliwa wa kwanza ilikuwa ya Yusufu -
3 wana wa Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli alikuwa Hanoki, Palu, Hezroni, na Karmi.
4 Uzao wa Yoeli ulikuwa huu: Mwana wa Yoeli alikuwa Shemaia. Mwana wa Shemaia alikuwa Gogi. Mwana wa Gogi alikuwa Shimei.
5 Mwana wa Shimei alikuwa Mika. Mwana wa Mika alikuwa Reaia. Mwana wa Reaia alikuwa Baali.
6 Mwana wa Baali alikuwa Bera, ambaye Tiligathi Pileseri alimpeleka matekani kule Assiria. Bera alikuwa kiongozi katika kabila la Rubeni.
7 Ndugu wa Bera kwa makabila yao ni hawa wafuatao, wameorodheshwa katika nakala za uzao wao: Yeieli wa kwanza, Zekaria, na
8 Bela mwana wa Azazi mwana wa Shema mwana wa Yoeli. Waliishi Aroeri, kwa umbali wa Nebo na Baali Meoni,
9 na mwanzo wa mashariki mwa jangwa lenye umbali wa hadi Mto Efarati. Hii ni kwa sababu walikuwa na mifugo mingi katika nchi ya Gileadi.
10 Katika siku za Sauli, kabila la Rubeni lilishambulia Wahagiri na kuwa shinda. Wakaishi ndani ya hema za Wahagiri katika nchi yote mashariki mwa Gileadi.
11 Kabila la Gadi liliishi karibu nao, katika nchi ya Bashani umbali wa Saleka.
12 Viongozi wao walikuwa Yoeli, aliyekuwa kichwa wa ukoo, na Shafamu alikuwa kichwa wa ukoo mwingine, na Yanai na Shafati walikuwa wa Bashani.
13 Ndugu zao, kwa familia za baba yao, walikuwa Mikaeli, Meshulamu, Sheba, Yorai, Yakani, na Eberi - jumla saba wote.
14 Hawa watu walio tajwa hapo juu ni uzao wa Abihaili, na Abihaili alikuwa mwana wa Huri. Huri alikuwa mwana w a Yaroa. Yaroa alikuwa mwana wa Gileadi. Gileadi alikuwa mwana wa Mikaeli. Mikaeli alikuwa mwana wa Yeshishai. Yeshishai alikuwa mwana wa Yado. Yado alikuwa mwana wa Buzi.
15 Ahi mwana wa Abidieli mwana wa Guni, alikuwa kichwa cha familia ya baba yake.
16 Waliishi Gileadi, Bashani, katika miji, na katika nchi zote za malisho ya Sharoni kwa umbali wa mipaka yake.
17 Hawa wote waliorodheshwa katika nakaka za uzao katika siku za Yothamu mfalme wa Yuda na Yeroboamu mfalme wa Israeli.
18 Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase walikuwa na wana jeshi elfu arobaini na nne walio fuzu kwa vita, walio beba ngao na upanga, na pinde na mishale.
19 Waliwashambulia Wahagri, Yeturi, Nafishi, na Nodabu.
20 Walipokea msaada wa Kimungu dhidi yao. Katika hili Wahagri na wote walio kuwa nao walishindwa. Hii ni kwa sababu Waisraeli walipaza sauti katika vita, na yeye akawajibu, kwa sababu waliweka tumaini lao kwake.
21 Walikamata wanya wao, pamoja na ngamia elfu hamsini, kondoo 250, 000, punda elfu mbili, na wanaume 100, 000.
22 Kwa sababu Mungu aliwapigania, waliua maadui wengi. Waliishi katika nchi yao mpaka mateka.
23 Baadhi ya watu wa kabila la Manase waliishi katika nchi ya Bashani kwa umbali wa Hermoni na Seniri (hiyo ni, Mlima Hermoni).
24 Hawa walikuwa viongozi wa familia zao: Eferi, Ishi, Elieli, Azrieli, Yeremia, Hodavia, na Yahdieli. Walikuwa wenye nguvu na wanaume wa jasiri, wanaume maharufu, viongozi wa familia zao.
25 Lakini walikuwa sio wa aminifu kwa Mungu wa babu zao. Badala yake, waliabudu miungu ya watu waio nchi, ambao Mungu aliwaangamiza mbele yao.
26 Mungu wa Israeli alimchochea Puli mfalme wa Assiria ( ambaye pia uitwa Tiligathi Pileseri, mfalme wa Assiria). Aliwa peleka matekani Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase. Aliwaleta kwa Hala, Habori, Hara, na kwenye mto wa Gozani, ambapo wapo adi leo.