< 1 Nyakati 26 >

1 Huu ulikuwa mgawanyiko wa walinzi wa lango: Kutoka kwa Wakora, Meshelemia mwana wa Kore, wa uzao wa Asafu.
למחלקות לשערים--לקרחים משלמיהו בן קרא מן בני אסף
2 Meshelemia alikuwa na wana wa kiume: Zekaria mzaliwa wa kwanza, Yediaeli wapili, Zebadia watatu, Yathinieli wanne,
ולמשלמיהו בנים--זכריהו הבכור ידיעאל השני זבדיהו השלישי יתניאל הרביעי
3 Elamu watano, Yehohanani wasita, Eliehoenai wasaba.
עילם החמישי יהוחנן הששי אליהועיני השביעי
4 Obedi alikuwa na wana wa kiume: Shemaia wa kwanza, Yehozabadi wapili, Yoa watatu, na Sakari wanne, na Nethanieli watano,
ולעבד אדם בנים--שמעיה הבכור יהוזבד השני יואח השלשי ושכר הרביעי ונתנאל החמישי
5 Amieli wasita, Isakari wasaba, Peulethai wanane, kwa kuwa Mungu alimbariki Obedi Edomu.
עמיאל הששי יששכר השביעי פעלתי השמיני כי ברכו אלהים
6 Kwa Shemaia mwanae walizawa wana walio tawala familia zao; walikuwa wanaume wenye uwezo mbali mbali.
ולשמעיה בנו נולד בנים הממשלים לבית אביהם כי גבורי חיל המה
7 Wana wa Shemaia walikuwa Othini, Refaeli, Obedi, na Elizabadi. Ndugu zake Elihu na Semakia walikuwa wanaume wenye uwezo mbali mbali.
בני שמעיה עתני ורפאל ועובד אלזבד אחיו--בני חיל אליהו וסמכיהו
8 Hawa wote walikuwa uzao wa Obedi Edomu. Wao na wanao na ndugu zao walikuwa wanaume wenye uwezo wa kufanya wajibu wao katika huduma ya hema la kuabudia. Palikuwa na sitini na mbili walio kuwa na undugu na Obedi Edomu.
כל אלה מבני עבד אדם המה ובניהם ואחיהם איש חיל בכח לעבדה--ששים ושנים לעבד אדם
9 Meshelemia alikuwa na wana na ndugu, wanaume wenye uwezo, jumla ya kumi na nane.
ולמשלמיהו בנים ואחים בני חיל--שמונה עשר
10 Hosa, mzao wa Merari, alikuwa na wana: Shimiri kiongozi (japo hakuwa mzaliwa wa kwanza, baba yake alimfanya kiongozi),
ולחסה מן בני מררי בנים--שמרי הראש כי לא היה בכור וישימהו אביהו לראש
11 Hilikia wapili, Tebalia watatu, Zekaria wanne. Wote wa wana wa Hosa na ndugu walikuwa kumi na tatu kwa idadi.
חלקיהו השני טבליהו השלשי זכריהו הרבעי כל בנים ואחים לחסה שלשה עשר
12 Huu mgawanyiko wa walinzi wa lango, sambamba na viongozi, ulikuwa na majukumu, kama ndugu zao, kutumika katika nyumba ya Yahweh.
לאלה מחלקות השערים לראשי הגברים משמרות--לעמת אחיהם לשרת בבית יהוה
13 Walirusha kura, wadogo kwa wakubwa, kulingana na familia zao, kwa kila lango.
ויפילו גורלות כקטן כגדול לבית אבותם--לשער ושער
14 Kura ilipo rushwa kwa lango la mashariki, ilimuangukia Shelemia. Kisha wakarusha kura kwa Zekaria mwana wake, mshauri makini, na kura yake ikatokea lango la kaskazini.
ויפל הגורל מזרחה לשלמיהו וזכריהו בנו יועץ בשכל הפילו גורלות ויצא גורלו צפונה
15 Kwa Obedi Edomu kulipangiwa lango la kusini, na wanae walipangiwa nyumba za ghala.
לעבד אדם נגבה ולבניו בית האספים
16 Shufimu na Hosa walipangiwa lango la magharibi pamoja na lango la Shalekethi, kwa barabara ya juu. Lindo lilikabiidhiwa kwa kila familia.
לשפים ולחסה למערב עם שער שלכת במסלה העולה משמר לעמת משמר
17 Kwa mashariki walikuwa Walawi sita, kaskazini kwa siku moja, kusini kwa siku moja, na nyumba za ghala wawili.
למזרח הלוים ששה לצפונה ליום ארבעה לנגבה ליום ארבעה ולאספים שנים שנים
18 Katika ua kuelekea magharibi wanne walipangwa, wanne barabarani, na wawili katika ua.
לפרבר למערב--ארבעה למסלה שנים לפרבר
19 Haya yalikuwa magawanyiko ya walinzi wa lango. Palijazwa na uzao wa Kora na Merari.
אלה מחלקות השערים לבני הקרחי ולבני מררי
20 Miongoni mwa Walawi, Ahija alikuwa kiongozi wa hazina ya nyumba ya Mungu, na hazina ya vitu vya Yahweh.
והלוים--אחיה על אוצרות בית האלהים ולאצרות הקדשים
21 Wazao wa Ladani, walitoka kwa Gerishoni kupitia kwake na walio kuwa viongozi wa familia za Ladani Mgerishoni, walikuwa Yehieli na wanae,
בני לעדן בני הגרשני ללעדן ראשי האבות ללעדן הגרשני--יחיאלי
22 Zethamu, na Yoeli kaka yake, aliyesimamia ghala za nyumba ya Yahweh.
בני יחיאלי--זתם ויואל אחיו על אצרות בית יהוה
23 Kulikuwa na askari walio chukuliwa kwa koo za Amramu, Izhari, Hebroni, na uzieli.
לעמרמי ליצהרי לחברוני לעזיאלי
24 Shebueli mwana wa Gerishomu mwana wa Musa, alikuwa msimamizi wa nyumba za ghala.
ושבאל בן גרשום בן משה נגיד על האצרות
25 Ndugu zake wa ukoo wa Eliezeri walikuwa Rehabia mwanae, mwana wa Rehabia Yeshaia, mwana wa Yeshaia Yoramu, mwana wa Yoramu Zikiri, na mwana wa Zikiri Shelomothi.
ואחיו לאליעזר--רחביהו בנו וישעיהו בנו וירם בנו וזכרי בנו ושלמות (ושלמית) בנו
26 Shelomothi na ndugu zake walikuwa wasimamizi wa nyumba zote za ghala zinazo hifadhi vitu vyote vya Yahweh, ambavyo Daudi mfalme, viongozi wa familia, wakuu wa maelfu na mamia, na wakuu wa jeshi walivyo vitenga.
הוא שלמות ואחיו על כל אצרות הקדשים אשר הקדיש דויד המלך וראשי האבות לשרי האלפים והמאות--ושרי הצבא
27 Walitenga vitu walivyo vichukuwa kwenye mapambano kwa ajili ya kutunza nyumba ya Yahweh.
מן המלחמות ומן השלל הקדישו--לחזק לבית יהוה
28 Pia walikuwa wahusika wa kila kitu kilicho tengwa kwa ajili ya Yahweh na Samweli nabii, Sauli mwana wa Kishi, Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Zeruia. Kila kitu kilicho tengwa kwa ajili ya Yahweh kilikuwa chini ya ulinzi wa shelomothi na ndugu zake.
וכל ההקדיש שמואל הראה ושאול בן קיש ואבנר בן נר ויואב בן צרויה--כל המקדיש על יד שלמית ואחיו
29 Wa uzao wa Izhari, Kenania na wana wake walikuwa wahusika wa mambo ya ndani ya Israeli. Walikuwa maafisa na waamuzi.
ליצהרי כנניהו ובניו למלאכה החיצונה על ישראל--לשטרים ולשפטים
30 Wa uzao wa Hebroni, Hashabia na kaka zake, wanaume wenye uwezo 1, 700, walikuwa wahusika wa kazi ya Yahweh na kazi ya mfalme. Walikuwa upande wa mgharibi mwa Yordani.
לחברוני חשביהו ואחיו בני חיל אלף ושבע מאות על פקדת ישראל מעבר לירדן מערבה--לכל מלאכת יהוה ולעבדת המלך
31 Kutoka uzao wa Hebroni, Yeriya alikuwa kiongozi wa uzao wake, walihesabiwa kutoka orodha za familia zao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi walitathimini kumbukumbu na kugundua miongoni mwao wanaume wa uwezo katika Yazeri ya Gileadi.
לחברוני יריה הראש לחברוני לתלדתיו לאבות--בשנת הארבעים למלכות דויד נדרשו וימצא בהם גבורי חיל ביעזיר גלעד
32 Yerija alikuwa na ndugu 2, 700, walio kuwa viongozi wenye uwezo katika familia. Daudi aliwafanya waangalizi wa makabila ya Rubeni na Gadi, na nusu kabila la Manase, kwa kila jambo linalo muhusu Mungu, na kwa mambo ya mfalme.
ואחיו בני חיל אלפים ושבע מאות--ראשי האבות ויפקידם דויד המלך על הראובני והגדי וחצי שבט המנשי לכל דבר האלהים ודבר המלך

< 1 Nyakati 26 >