< 1 Nyakati 24 >

1 Makundi vya kazi kulingana na uzao wa Aroni yalikuwa haya: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
Hii ndiyo migawanyo ya wana wa Aroni: Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
2 Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao kufa. Walikuwa hawana watoto, kwahiyo Eleazari na Ithamari walitumika kama makuhani.
Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakahudumu kama makuhani.
3 Daudi pamoja na Zadoki, uzao wa Eleazari, na Ahimeleki, uzao wa Ithamari, waliwagawanya katika makundi yao ya kazi kama makuhani.
Akisaidiwa na Sadoki mwana wa Eleazari na Ahimeleki mwana wa Ithamari, Daudi aliwapanga wazao wa Aroni katika migawanyo kufuatana na wajibu wa huduma zao.
4 Kulikuwa na wanaume viongozi zaidi kati ya uzao wa Eleazari kuliko kati ya uzao wa Ithamari, kwahiyo waligawanya uzao wa Eleazari katika makundi kumi na sita. Walifanya hivyo na viongozi wa ukoo na uzao wa Ithamari. Magawanyo haya yalikuwa nane kwa idadi, sambamba na koo zao.
Idadi kubwa ya viongozi walipatikana miongoni mwa wazao wa Eleazari, kuliko miongoni mwa wazao wa Ithamari, nao waligawanywa kwa uwiano: Viongozi kumi na sita kutoka jamaa ya wazao wa Eleazari na viongozi wanane kutoka jamaa ya wazao wa Ithamari.
5 Waliwagawanya bila upendeleo kwa kura, kwa kuwa walikuwa waamuzi watakatifu na waamuzi wa Mungu, kutoka pande zote uzao wa Eleazari na uzao wa Ithamari.
Waliwagawanya bila upendeleo kwa kupiga kura, kwa kuwa kulikuwa na maafisa wa mahali patakatifu na maafisa wa Mungu miongoni mwa wazao wale wa Eleazari na wale wa Ithamari.
6 Shemaia mwana wa Nethaneli mwandishi, Mlawi, aliandika majina yao mbele ya mfalme, muamuzi, kuhani Zadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa makuhani na familia za Walawi. Ukoo mmoja ulichaguliwa kwa kura kutoka uzao wa Eleazari, na kisha uliofata utachaguliwa kutoka uzao wa Ithhamari.
Mwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.
7 Kura ya kwanza ilienda kwa Yehoiaribu, ya pili kwa Yedaia,
Kura ya kwanza ilimwangukia Yehoyaribu, ya pili Yedaya,
8 ya tatu kwa Harimu, ya nne kwa Seorimu,
ya tatu Harimu, ya nne Seorimu,
9 ya tano kwa Malikija, ya sita kwa Mijamini,
ya tano Malkiya, ya sita Miyamini,
10 ya saba kwa Hakozi, ya nane kwa Abija,
ya saba Hakosi, ya nane Abiya,
11 ya tisa kwa Yeshua, ya kumi kwa Shekania,
ya tisa Yeshua, ya kumi Shekania,
12 ya kumi na moja kwa Eliashibu, ya kumi na mbili kwa Yakimu,
ya kumi na moja Eliashibu, ya kumi na mbili Yakimu,
13 ya kumi na tatu kwa Hupa, ya kumi na nne kwa Yesheheabu,
ya kumi na tatu Hupa, ya kumi na nne Yeshebeabu,
14 ya kumi na tano kwa Biliga, ya kumi na sita kwa Imma,
ya kumi na tano Bilga, ya kumi na sita Imeri,
15 ya kumi na saba kwa Heziri, ya kumi na nane kwa Hapizezi,
ya kumi na saba Heziri, ya kumi na nane Hapisesi,
16 ya kumi na tisa kwa Pethaia, ya ishirini kwa Yehezikeli,
ya kumi na tisa Pethahia, ya ishirini Yehezkeli,
17 ya ishirini na moja kwa Yakini, ya ishirini na mbili kwa Gamuli,
ya ishirini na moja Yakini, ya ishirini na mbili Gamuli,
18 ya ishirini na tatu kwa Delaia, na ya ishirini na nne kwa Maazia.
ya ishirini na tatu Delaya, ya ishirini na nne Maazia.
19 Hii ilikuwa taratibu ya utumishi wao, walipo kuja kwenye nyumba ya Yahweh, wakifuata utaratibu waliopewa na Aruni babu yao, kama Yahweh, Mungu wa Israeli, alivyo waagiza.
Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la Bwana kulingana na masharti waliyoelekezwa na Aroni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.
20 Hawa walikuwa Walawi waliobakia: Wana wa Amiramu, Shebueli; wana wa Shebaeli, Yedeia.
Kuhusu wazao wa Lawi waliobaki: Kutoka kwa wana wa Amramu: alikuwa Shubaeli; kutoka kwa wana wa Shubaeli: alikuwa Yedeya.
21 Wana wa Rehabia: wana wa Rehabia, Ishia kiongozi.
Kwa wa Rehabia, kutoka kwa wanawe: Ishia alikuwa wa kwanza.
22 Wa Waizari, Shelomothi; mwana wa Shelomothi, Yahathi.
Kutoka kwa Waishari: alikuwa Shelomithi, kutoka kwa wana wa Shelomithi: alikuwa Yahathi.
23 Wana wa Hebroni: Yeria kiongozi, Amaria wapili, Yahazieli watatu, na Yekameamu wanne.
Wana wa Hebroni: Yeria alikuwa mkuu, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.
24 Wana wa uzao wa Uzieli ulimjumuisha Mika. Uzao wa Mika ulimjumuisha Shamiri.
Mwana wa Uzieli: alikuwa Mika; kutoka kwa wana wa Mika: alikuwa Shamiri.
25 Kaka wa Mika alikuwa Ishia. Wana wa Ishia akijumuishwa Zakaria.
Ndugu yake Mika: alikuwa Ishia; na kutoka kwa wana wa Ishia: alikuwa Zekaria.
26 Wana na Merari: Mahli na Mushi. Mwana wa Yaazia, Beno.
Wana wa Merari: walikuwa Mahli na Mushi. Mwana wa Yaazia: alikuwa Beno.
27 Wana wa Merari: Yaazia, Beno, Shohamu, Zakuri, na Ibrri.
Wana wa Merari: kutoka kwa Yaazia: ni Beno, Shohamu, Zakuri na Ibri.
28 Wana wa Mahili: eleazari, ambaye alikuwa hana wana.
Kutoka kwa Mahli: alikuwa Eleazari, ambaye hakuwa na wana.
29 Wana wa Kishi: Yerameli
Kutoka kwa Kishi: mwana wa Kishi: alikuwa Yerameeli.
30 wana wa Mushi: Mahli, Eda, na yerimothi. Walikuwa walawi, walio orodheshwa na familia zao.
Nao wana wa Mushi: walikuwa Mahli, Ederi na Yeremothi. Hawa walikuwa Walawi kulingana na jamaa zao.
31 Wanaume hawa ambao walikuwa vichwa katika nyumba za baba zao na kila wadogo zao, walipiga kura katika uwepo wa Mfalme Daudi, na Zadoki na Ahimeleki, pamoja na viongozi wa familia wa makuhani na Walawi. Walirusha kura kama uzao wa Aroni walivyofanya.
Pia walipiga kura kama vile ndugu zao wazao wa Aroni walivyofanya, mbele ya Mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na mbele ya viongozi wa jamaa ya makuhani na ya Walawi. Jamaa za ndugu wakubwa zilitendewa sawasawa na zile za ndugu wadogo.

< 1 Nyakati 24 >