< 1 Nyakati 23 >
1 Daudi alipo kuwa mzee na kukaribia mwisho wa maisha yake, alimfanya Sulemani mwanae mfalme juu ya Israeli.
2 Aliwakusanya pamoja viongozi wote wa Israeli, na makuhani na Walawi.
3 Walawi walio kuwa miaka thelathini na zaidi walihesabiwa. Idadi ya elfu thelathini na nane.
4 Kwa hawa, elfu ishirini na nne walikuwa kusimamia kazi ya nyumba ya Yahweh, na elfu sita walikuwa maaskari na waamuzi.
5 Elfu nne walikuwa walinzi wa lango, na elfu nne walikuwa wamsifu Yahweh na vyombo nilivyo vitengeneza vya kusifu.” Daudi akasema.
6 Akawatenganisha kwenye vikundi kulingana na wana wa Levi: Gerishoni, Kohathi, na Merari.
7 Kwa koo za uzao wa Gerishoni, kulilkuwa na Ladani na Shimei.
8 Palikuwa na watatu wa wana wa Ladani: Yehieli kiongozi, Zethami, na Yoeli.
9 Palikuwa na watatu wa wana wa Shimei: Shelomothi, Hazieli, na Harani. Hawa walikuwa viongozi wa koo ya Ladani.
10 Palikuwa na wanne wa wana wa Shimei: Yahathi, Ziza, Yeushi, na Beria.
11 Yahathi alikuwa mkubwa, Ziza wapili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi, hivyo walihesabiwa kama ukoo mmoja na kupangiwa kazi sawa.
12 Palikuwa na wanne wa wana wa Kohathi: Amramu, Izhari, Hebroni, na Uzieli.
13 Hawa walikuwa wana wa Amramu: Aruni na Musa. Aruni alichaguliwa kuandaa vitu vitakatifu, yeye na uzao wake watatoa uvumba kwa Yahweh, kumtumikia na kumpa baraka kwa jina lake.
14 Lakini kwa Musa mtu wa Mungu, wana wake walihesabiwa kuwa Walawi.
15 Wana wa Musa walikuwa Gerishomu na Eliezeri.
16 Uzao wa Gerishomu ulikuwa Shebueli mkubwa.
17 Uzao wa Eliezeri alikuwa Rehabia. Eliezeri hakuwa na wana wengine, lakini Rehabia alikuwa na uzao mkubwa.
18 Mwana wa Izihari alikuwa Shelomithi kiongonzi.
19 Uzao wa Hebroni ulikuwa Yeria, mkubwa, Amaria wapili, Yahazieli watatu, na Yekameamu wanne.
20 Wana wa Uzieli walikuwa Mika mkubwa, na Ishia wapili.
21 Wana wa Merari walikuwa Mahili na Mushi. Wana wa Mahili walikuwa Eleazari na Kishi.
22 Eleazari alikufa bila mtoto wa kiume. Alikuwa na mabinti tu. Wana wa Kishi waliwaoa.
23 Wana wa Mushi watatu walikuwa Mahili, Ederi, na Yeremothi.
24 Hawa walikuwa uzao wa Lawi kuligana na koo zao. Walikuwa viongozi, wamehesabiwa na kuorodheshwa kwa majina, kuanzia koo zilizo fanya kazi katika nyumba ya Yahweh, kutoka miaka ishirini na zaidi.
25 Kwa kuwa Daudi alisema, “Yahweh, Mungu wa Israeli, amewapa pumziko watu wake. Anafanya makao yake Yerusalemu milele.
26 Walawi hawataitaji kubeba hema la kuabuadia na vifaa vyake vinavyo tumika kwenye utumishi wake.”
27 Kwa maneno ya Daudi ya mwisho Walawi walihesabiwa, miaka ishirini na kuendelea.
28 Wajibu wao ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aruni katika utumishi wa nyumba ya Yahweh. Walikuwa washughulikie nyuani, vyumbani, utakasaji wa vitu vyote vya Yahweh, na kazi zingine katika utumishi wa nyumba ya Mungu.
29 Pia walishughulikia mkate wa uwepo, unga safi wa mbegu za sadaka, maandazi ya siotiwa chachu, sadaka za ngano, sadaka ziliochanganywa na mafuta, na vipimo vyote vya idadi n a ukubwa wa vitu.
30 Pia walisimama kila asubui kumshukuru na kumsifu Yahweh. Pia walifanya hivi jioni
31 na kila wakati sadaka ya kuteketezwa ilipo tolewa kwa Yahweh, siku ya Sabato na sherehe za mwezi mpya na siku za maakuli. Idadi iliyo pangwa, iliyo tolewa kwa amri, ilipaswa kuwa mbele ya Yahweh.
32 Walikuwa viongozi wa hema la kukutania, patakatifu, na kuwasaidia ndugu zao wa uzao wa Aruni katika utumishi wa nyumba ya Yahweh.