< 1 Nyakati 22 >

1 Kisha Daudi akasema, “Hapo ndipo nyumba ya Yahweh Mungu itakuwepo, na madhabahu ya sadaka za kuteketezwa za Israeli.”
大卫说:“这就是耶和华 神的殿,为以色列人献燔祭的坛。”
2 Hivyo Daudi akaagiza watumishi wake wawakusanye pamoja wageni wote wanao ishi katika nchi ya Israeli. Aliwapangia kuwa wachonga mawe, kuchonga matofali ya mawe, ilikuweza kujenga nyumba ya Mungu.
大卫吩咐聚集住以色列地的外邦人,从其中派石匠凿石头,要建造 神的殿。
3 Daudi alisambaza idadi kubwa ya chuma kwa ajili ya misumari na vitasa vya kuweka kwenye malango. Pia alitoa shaba zaidi kushinda kipimo,
大卫预备许多铁做门上的钉子和钩子,又预备许多铜,多得无法可称;
4 na miti ya mierezi zaidi ya kipimo. (Wasidoni na Watiria walileta mboa nyingi za mierezi kwa Daudi azihesabu.)
又预备无数的香柏木,因为西顿人和泰尔人给大卫运了许多香柏木来。
5 Daudi akasema, “Mwanangu Sulemani ni mdogo na hana uzoefu, na nyumba itayo jengwa kwa Yahweh lazima iwe maridadi, ilikwamba iwe maarufu na ya utukufu kwa nchi zingine. Hivyo nitaanda ujenzi wake.” Hivyo Daudi akafanya maandalizi ya kina kabla ya mauti yake.
大卫说:“我儿子所罗门还年幼娇嫩,要为耶和华建造的殿宇必须高大辉煌,使名誉荣耀传遍万国;所以我要为殿预备材料。”于是,大卫在未死之先预备的材料甚多。
6 Akaagiza Sulemani mwanae kuitwa na kumuamuru ajenge nyumba ya Yahweh, Mungu wa Israeli.
大卫召了他儿子所罗门来,嘱咐他给耶和华—以色列的 神建造殿宇,
7 Daudi akasema kwa Sulemani, “Mwanangu, ilikuwa dhamira yangu kujenga nyumba mwenyewe, kwa ajili ya jina la Yahweh Mungu wangu.
对所罗门说:“我儿啊,我心里本想为耶和华—我 神的名建造殿宇,
8 Lakini Yahweh alikuja kwangu na kusema, 'Wewe umemwaga damu nyingi na umepigana mapambono mengi. Hauta jenga nyumba kwa jina langu, kwasababu umemwaga damu nyingi kwenye ardhi machoni pangu.
只是耶和华的话临到我说:‘你流了多人的血,打了多次大仗,你不可为我的名建造殿宇,因为你在我眼前使多人的血流在地上。
9 Walakini, utapata mwana ambaye atakuwa mtu wa amani. Nitampa kupumzika na maadui zake kwa kila upande. Kwa kuwa jina lake litaitwa Sulemani, na nitatoa amani na utulivu kwa Israeli katika siku zake.
你要生一个儿子,他必作太平的人;我必使他安静,不被四围的仇敌扰乱。他的名要叫所罗门。他在位的日子,我必使以色列人平安康泰。
10 Ata jenga nyumba kwa jina langu. Ata kuwa mwana wangu, na nitakuwa baba yake. Nitaimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake juu ya Israeli.
他必为我的名建造殿宇。他要作我的子;我要作他的父。他作以色列王;我必坚定他的国位,直到永远。’
11 Sasa, mwanangu, Yahweh awe nawe na kukuwezesha kufanikiwa. Uweze kujenga nyumba ya Yahweh Mungu wako, kama alivyo sema utajenga.
我儿啊,现今愿耶和华与你同在,使你亨通,照他指着你说的话,建造耶和华—你 神的殿。
12 Yahweh tu akupe uwelewa na ufahamu, ili utii sheria ya Yahweh Mungu wako, ata kapokuweka kiongozi juu ya Israeli.
但愿耶和华赐你聪明智慧,好治理以色列国,遵行耶和华—你 神的律法。
13 Kisha utafanikiwa, kama tu ukitii maagizo na amri Yahweh alizo mpa Musa kuhusu Israeli. Kuwa hodari na mshujaa. Usiogope wala kufadhaika.
你若谨守遵行耶和华借摩西吩咐以色列的律例典章,就得亨通。你当刚强壮胆,不要惧怕,也不要惊惶。
14 Sasa, ona, kwa bidii kubwa nimeandaa kwa ajili ya nyumba ya Yahweh talanta 100, 000 za dhahabu, talanta milioni moja za fedha, na shaba na chuma katika idadi kubwa. Pia nimetoa mbao na mawe. Lazima uongeze zaidi katika haya.
我在困难之中为耶和华的殿预备了金子十万他连得,银子一百万他连得,铜和铁多得无法可称;我也预备了木头、石头,你还可以增添。
15 Una wafanya kazi wengi: wachonga mawe, maseremala, wanaume wenye ujuzi mbali mbali,
你有许多匠人,就是石匠、木匠,和一切能做各样工的巧匠,
16 wenye uwezo wa kufanya kazi na dhahabu, fedha, shaba, na nishati. Hivyo anza kufanya kazi, na Yahweh awe nawe.
并有无数的金银铜铁。你当起来办事,愿耶和华与你同在。”
17 Daudi akawaagiza viongozi wote Waisraeli wamsaidie Sulemani mwanae, akisema,
大卫又吩咐以色列的众首领帮助他儿子所罗门,说:
18 “Yahweh Mungu wenu yupo nanyi na amewapa amani kila pande. Amewakabidhi mikononi mwangu wenyeji wote mkoa. Mkoa umetiishwa mbele za Yahweh na watu wake.
“耶和华—你们的 神不是与你们同在吗?不是叫你们四围都平安吗?因他已将这地的居民交在我手中,这地就在耶和华与他百姓面前制伏了。
19 Sasa mtafuteni Yahweh Mungu wenu kwa moyo wenu wote na nafsi. Simameni na mjenge sehemu takatifu ya Yahweh Mungu. Kisha mwaweza kuleta sanduku la agano la Yahweh na vitu vya Mungu ndani ya nyumba iliyo jengwa kwa ajili ya jina la Yahweh.
现在你们应当立定心意,寻求耶和华—你们的 神;也当起来建造耶和华 神的圣所,好将耶和华的约柜和供奉 神的圣器皿都搬进为耶和华名建造的殿里。”

< 1 Nyakati 22 >