< 1 Nyakati 2 >

1 Hawa ndio wana wa Israeli: Reubeni, Simioni, Lawi, Yuda, Isakari, Zebuloni,
Hawa ndio waliokuwa wana wa Israeli: Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zabuloni,
2 Dani, Yusufu, Benyamini, Naftali, Gadi, na Asheri.
Dani, Yosefu, Benyamini, Naftali, Gadi na Asheri.
3 Wana wa Yuda walikuwa Eri, Onani, na Shela, ambao walizaliwa na binti wa Shua, Wakanaani. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa muovu katika macho ya Yahweh, na Yahweh akamwua.
Wana wa Yuda walikuwa: Eri, Onani na Shela. Hawa watatu walizaliwa kwake na mkewe Mkanaani, binti wa Shua. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Bwana, kwa hiyo Bwana alimuua.
4 Tamari, mkwe wake, alimzalia Peresi na Zera. Yuda alikuwa na wana wa kiume wa tano.
Tamari, mkwewe Yuda, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera. Yuda alikuwa na jumla ya wana watano.
5 Wana wa Peresi walikuwa Hesroni na Hamuli.
Wana wa Peresi walikuwa: Hesroni na Hamuli.
6 Wana wa Zera walikuwa Zimri, Ethani, Hemani, Kalikoli na Darda, wote kwa jumla ni watano.
Wana wa Zera walikuwa: Zimri, Ethani, Hemani, Kalkoli na Dara. Jumla ya wana wa Zera walikuwa watano.
7 Mwana wa Karmi alikuwa ni Akani, aliye leta taabu katika Israeli alipo iba kile kilicho hifadhiwa kwa ajili ya Mungu.
Mwana wa Karmi alikuwa: Akari, ambaye alileta taabu kwa Waisraeli kwa kukiuka onyo la kutokuchukua vitu vilivyokuwa vimewekwa wakfu.
8 Mwana wa Ethani alikuwa Azaria.
Mwana wa Ethani alikuwa: Azariya.
9 Wana wa Hezroni walikuwa ni Yerameeli, Ramu, na Kalebu.
Wana wa Hesroni walikuwa: Yerameeli, Ramu na Kalebu.
10 Ramu akawa baba wa Aminadabu, na Aminadabu akawa baba wa Nashoni, kiongozi miongoni uzao wa Yuda.
Ramu alimzaa Aminadabu, na Aminadabu akamzaa Nashoni, kiongozi wa kabila la Yuda.
11 Nashoni akawa baba wa Salmoni, na Salmon akawa baba wa Boazi.
Nashoni akamzaa Salmoni, Salmoni akamzaa Boazi,
12 Boazi akawa baba wa Obedi, na Obedi akawa baba wa Yese.
Boazi akamzaa Obedi, Obedi akamzaa Yese.
13 Yese akawa baba wa mzaliwa wake wa kwanza Eliabu, wa pili Abinadabu, wa tatu Shama.
Yese akawazaa Eliabu mwanawe wa kwanza; wa pili Abinadabu, wa tatu Shimea,
14 Nethaneli wa nne, Radai wa tano.
wa nne Nethaneli, wa tano Radai,
15 Ozemu wa sita, na Daudi wa saba.
wa sita Osemu, na wa saba Daudi.
16 Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa Abishai, Yoabu, na Asaheli, jumla watatu.
Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli.
17 Abigali akamzaa Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri Mwishmaeli.
Abigaili alikuwa mama yake Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri, Mwishmaeli.
18 Kalebu mwana wa Hesroni akawa baba wa watoto wa Azubu mkewe, na Yeriothi. Wanawe walikuwa Yesheri, Shobabu, na Ardoni.
Kalebu mwana wa Hesroni akazaa wana na mkewe Azuba (na pia na Yeriothi). Hawa ndio wana Azuba aliomzalia Kalebu: Yesheri, Shobabu na Ardoni.
19 Azuba akafa, na Kalebu akamuoa Efrathi, aliye mzalia Huri.
Azuba alipofariki, Kalebu akamwoa Efrathi, ambaye alimzalia Huri.
20 Huri akawa baba wa Uri, na Uri akawa baba wa Besaleli.
Huri akamzaa Uri, Uri akamzaa Bezaleli.
21 Baadae Hesroni (alipo kuwa na miaka sitini) akamuoa binti wa Makiri, baba wa Gileadi. Akamzalia Segubu.
Hatimaye, Hesroni akakutana kimwili na binti wa Makiri babaye Gileadi (ambaye alimwoa alipokuwa na umri wa miaka sitini), naye akamzaa Segubu.
22 Segubu akawa baba wa Yairi, aliye miliki miji ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi.
Segubu akamzaa Yairi, ambaye alitawala miji ishirini na mitatu katika Gileadi.
23 Geshuri na Aramu wakawapokonya miji ya Yairi na Kenathi, pamoja na miji sitini iliyo zunguka. Hawa wakazi wote walikuwa ni uzao wa Makiri, baba wa Gileadi.
(Lakini Geshuri na Aramu wakateka miji ya Hawoth-Yairi, pamoja na Kenathi na viunga vyake; jumla ilikuwa miji sitini.) Wote hawa walikuwa wazao wa Makiri babaye Gileadi.
24 Baada ya kifo cha Hesroni, Kalebu akalala na Efrata, mke wa baba yake Hesroni. Akamzalia Ashuri, baba wa Tekoa.
Baada ya Hesroni kufa huko Efrathi, Abiya mjane wa Hesroni akamzalia Ashuru, aliye baba wa Tekoa.
25 Wana wa Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, walikuwa ni Ramu mzaliwa wa kwanza, Buna, Oreni, Ozemu, na Ahiya.
Wana wa Yerameeli mzaliwa wa kwanza wa Hesroni walikuwa: Ramu mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya.
26 Yerameeli alikuwa na mke mwingine, Jina lake lilikuwa Atara. Yeye alikuwa mama wa Onamu.
Yerameeli alikuwa na mke mwingine, aliyeitwa Atara, aliyekuwa mama yake Onamu.
27 Wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, Yamini, na Ekeri.
Wana wa Ramu mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli walikuwa: Maasi, Yamini na Ekeri.
28 Wana wa Onamu walikuwa ni Shamai na Yada. Wana wa Shamai walikuwa ni Nadabu na Abishuri.
Wana wa Onamu walikuwa: Shamai na Yada. Wana wa Shamai walikuwa: Nadabu na Abishuri.
29 Jina la mke wa Abishuri lilikuwa Abihaili, na akamzalia Abani na Molidi.
Mke wa Abishuri aliitwa Abihaili, ambaye alimzalia Abani na Molidi.
30 Wana wa Nadabu walikuwa Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa pasipo watoto.
Wana wa Nadabu walikuwa Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa bila kuzaa watoto.
31 Mwana wa Apaimu alikuwa Ishi. Mwana wa Ishi alikuwa Sheshani. Mwana wa Sheshani alikuwa Alai.
Apaimu akamzaa: Ishi ambaye alikuwa baba wa Sheshani. Sheshani akamzaa Alai.
32 Wana wa Yada, kaka yake Shamai, walikuwa Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa pasipo mtoto.
Wana wa Yada, nduguye Shamai walikuwa: Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa bila kuzaa watoto.
33 Wana wa Yonathani walikuwa Pelethi na Zaza. Hawa ndio uzao wa Yerameeli.
Wana wa Yonathani walikuwa: Pelethi na Zaza. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yerameeli.
34 Sasa Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, bali wa kike pekee. Sheshani alikuwa na mtumishi, wa Kimisri, ambaye jina lake lilikuwa Yariha.
Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, ila wasichana tu. Alikuwa na mtumishi Mmisri aliyeitwa Yarha.
35 Sheshani alimkabidhi binti yake kwa Yariha mtumishi wake kama mke wake. Akamzalia Atai.
Sheshani akamwoza huyu mtumishi wake Yarha binti yake, akamzalia mwana jina lake Atai.
36 Atai akawa baba wa Nathani, na Nathani akawa baba wa Zabadi.
Atai akamzaa Nathani, Nathani akamzaa Zabadi,
37 Zabadi akawa baba wa Efalali, na Afalali akawa baba wa Obedi.
Zabadi akamzaa Eflali, Eflali akamzaa Obedi,
38 Obedi akawa baba wa Yehu, na Yehu akawa baba wa Azaria.
Obedi akamzaa Yehu, Yehu akamzaa Azaria,
39 Azaria akawa baba wa Helesi, na Helesi akawa baba wa Eleasa.
Azaria akamzaa Helesi, Helesi akamzaa Eleasa,
40 Eleasa akawa baba wa Sismai, na Sismai akawa baba wa Shalumu.
Eleasa akamzaa Sismai, Sismai akamzaa Shalumu,
41 Shalumu akawa baba wa Yekamia, na Yekamia akawa baba wa Elishama.
Shalumu akamzaa Yekamia, naye Yekamia akamzaa Elishama.
42 Wana wa Kalebu, kaka yake Yerameeli, walikuwa ni Mesha mzaliwa wake wa kwanza, aliye kuwa baba wa Zifu. Mwanae wa pili, Maresha, allikuwa baba wa Hebroni.
Wana wa Kalebu nduguye Yerameeli walikuwa: Mesha mzaliwa wake wa kwanza alimzaa Zifu, naye mwanawe Maresha akamzaa Hebroni.
43 Wana wa Hebroni walikuwa Kora, Tapua, Rekemu, na Shema.
Hebroni alikuwa na wana wanne: Kora, Tapua, Rekemu na Shema.
44 Shema akawa baba wa Rahamu, baba wa Yorkeamu. Rekemu akawa baba wa Shamai.
Shema alikuwa baba yake Rahamu na Rahamu alikuwa baba wa Yorkeamu na Rekemu alikuwa baba wa Shamai.
45 Mwana wa Shamai alikuwa Maoni, na Maoni alikuwa baba wa Bethsuri.
Shamai akamzaa Maoni na Maoni akamzaa Beth-Suri.
46 Efa, suria wa Kalebu, alimza Harani, Mosa, na Gazezi. Harani akawa baba wa Gazezi.
Efa, suria wa Kalebu alikuwa mamaye Harani, Mosa na Gazezi. Harani alikuwa baba wa Gazezi.
47 Wana wa Yadai walikuwa Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa, na Shaafa.
Wana wa Yadai walikuwa: Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa na Shaafu.
48 Maaka, suria wa Kalebu, alimza Sheberi na Tirhana.
Maaka suria wa Kalebu alikuwa mamaye Sheberi na Tirhana.
49 Pia akamza Shaafu baba wa Madmana, Sheva baba wa Makbena na baba wa Gibea. Binti wa Kalebu alikuwa Aksa. Hawa walikuwa uzao wa Kalebu.
Pia Maaka akamzaa Shaafu babaye Madmana, na Sheva babaye Makbena na Gibea. Kalebu alikuwa na binti jina lake Aksa.
50 Hawa walikuwa wana wa Huri, mzaliwa wake wa kwanza kwa Efratha: Shobali baba wa Kiriath-Yearimu.
Hawa ndio waliokuwa wazao wa Kalebu. Wana wa Huri, mzaliwa mkuu wao wa Efrathi, walikuwa: Shobali akamzaa Kiriath-Yearimu,
51 Salma baba wa Bethlehemu, na Harefu baba wa Beth-gaderi.
Salma akamzaa Bethlehemu, naye Harefu akamzaa Beth-Gaderi.
52 Shobali baba wa kiriath-Yearimu alikuwa na uzao: Haroe, nusu ya watu Wamenuthite,
Wazao wa Shobali, baba yake Kiriath-Yearimu, walikuwa: Haroe, nusu ya wakazi wa mji wa Menuhothi,
53 na ukoo wa Kiriath-Yearimu: Waithri, Waputhi, Washumathi, na Wamishrai. Wasorathi na Waeshtaoli walitoka huku.
pamoja na koo za Kiriath-Yearimu ambazo ni: Waithiri, Waputhi, Washumathi na Wamishrai. Kutokana na watu hawa walizaliwa Wasorathi na Waeshtaoli.
54 Ukoo wa Salma ulikuwa kama ufatao: Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, na nusu ya Wamenuhothi na Wazori,
Wazao wa Salma walikuwa: Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, nusu ya Wamanahathi, Wasori,
55 ukoo wa waandishi walio ishi Yabesi: Watirathi, Washimeathi, na Wasukathi. Hawa walikuwa Wakeni walio toka katika uzao wa Hamathi, babu wa Warekabu.
pamoja na koo za waandishi zilizoishi katika mji wa Yabesi: yaani Watirathi, Washimeathi na Wasukathi. Hawa ndio Wakeni waliotokana na Hamathi, baba wa nyumba ya Rekabu.

< 1 Nyakati 2 >