< 1 Nyakati 16 >

1 Wakaleta ndani Sanduku la Mungu na kuweka katika ya hema ambalo Daudi aliandaa. Kisha wakatoa sadaka ya kuteketeza na sadaka ya ushirika mbele ya Mungu.
Wakaleta Sanduku la Mungu na kuliweka ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili yake, na wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu.
2 Daudi alipo maliza kutoa dhabiu ya kuteketeza na sadaka za ushirika, aliwabariki watu kwa jina la Yahweh.
Baada ya Daudi kumaliza kutoa hizo sadaka za kuteketezwa na hizo sadaka za amani, akawabariki watu katika jina la Bwana.
3 Alisambaza kwa kila Misraeli, mwanaume na mwanamke, kipande cha mkate, na kipande cha nyama, na keki ya mzabibu.
Kisha akamgawia kila Mwisraeli mwanaume na mwanamke mkate, andazi la tende na andazi la zabibu kavu.
4 Daudi aliewapangia baadhi ya Walawi kutumika mbele ya sanduku la Yahweh, na kusheherekea, kushukuru na kumsifu Yahweh, Mungu wa Israeli.
Akawaweka pia baadhi ya Walawi ili wahudumu mbele ya Sanduku la Bwana kufanya maombi, kumshukuru na kumsifu Bwana, Mungu wa Israeli:
5 Hawa Walawi walikuwa Asafu kiongozi, wa pili kutoka kwake Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaia, Obedi Edomu, na Yeieli. Hawa walikuwa wacheze na vyombo vya uzi na vinubi. Asafu alikuwa apige upatu, kwa kelele.
Asafu ndiye alikuwa mkuu wao, akisaidiwa na Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaya, Obed-Edomu na Yeieli. Hawa ndio wangepiga zeze na vinubi, Asafu angepiga matoazi,
6 Benaia na Yahazieli walikuwa wakupiga tarumbeta kila mara, mbele sanduku la agano la Mungu.
nao Benaya na Yahazieli makuhani, ndio wangepiga tarumbeta mara kwa mara mbele ya Sanduku la Agano la Mungu.
7 Kisha katika hiyo siku Daudi akawachagua Asafu na kaka zake kuimba hii nyimbo ya shukurani kwa Yahweh.
Siku ile, kitu cha kwanza Daudi alichofanya ni kumkabidhi Asafu na wenzake zaburi hii ya shukrani kwa Bwana:
8 Mpeni shukurani Yahweh, liitieni jina lake; fahamisheni mataifa matendo yake.
Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.
9 Mwiimbieni, imbeni sifa kwake; semeni matendo yake ya ajabu.
Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa; waambieni matendo yake yote ya ajabu.
10 Jisifuni katika jina lake takatifu; mioyo ya wanao mtafuta Yahweh ishangilie.
Lishangilieni jina lake takatifu; mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi.
11 Mtafute Yahweh na nguvu zake; tafuteni uwepo wake siku zote.
Mtafuteni Bwana na nguvu zake; utafuteni uso wake siku zote.
12 Kumbukeni matendo aliyo ya fanya kwenu, miujiza yake na amri za kinywa chake,
Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka,
13 enyi uzao wa Israeli mtumishi wake, enyi watu wa Yakobo, wateule wake.
enyi wazao wa Israeli mtumishi wake, enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
14 Yeye ni Yahweh, Mungu wetu. Amri zake zipo duniani kote.
Yeye ndiye Bwana Mungu wetu; hukumu zake zimo duniani pote.
15 Tunzeni agano lake akilini mwenu milele, neno alilo liamuru kwa vizazi elfu moja.
Hulikumbuka agano lake milele, neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,
16 Anakumbuka agano alilo lifanya na Ibrahimu, na nadhiri yake kwake Isaka.
agano alilolifanya na Abrahamu, kiapo alichomwapia Isaki.
17 Hili ndilo alilo lithibitisha kwa Yakobo kama amri maalumu, na kwa Israeli kama agano la milele.
Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri, kwa Israeli liwe agano la milele:
18 Alisema, “Nitakupa nchi ya Kanani kama sehemu ya urithi wako.”
“Nitakupa wewe nchi ya Kanaani kuwa sehemu utakayoirithi.”
19 Nilisema hili mlipo kuwa wachache kwa idadi, wachache sana, mlipo kuwa wageni katika nchi.
Walipokuwa wachache kwa idadi, wachache sana na wageni ndani yake,
20 Walienda taifa hadi taifa, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
21 Hakuwaruhusu yeyote awatese; aliwahadhibu wafalme kwa ajili yao.
Hakuruhusu mtu yeyote awaonee; kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:
22 Alisema, “Msiwaguse wapakwa mafuta wangu, na msiwadhuru manabii wangu.”
“Msiwaguse niliowatia mafuta; msiwadhuru manabii wangu.”
23 Imbeni kwa Yahweh, dunia yote; tangazeni wokovu wake siku hadi siku.
Mwimbieni Bwana dunia yote; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.
24 Kirini utukufu wake kwa mataifa, matendo yake makuu kwa mataifa yote.
Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.
25 Kwa kuwa Yahweh ni mkuu na ni wakusifiwa sana, na ni wakuogopewa kuliko miungu yote.
Kwa kuwa Bwana ni mkuu, mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.
26 Kwa kuwa miungu ya mataifa ni sanamu, lakini ni Yahweh aliye umba mbingu.
Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini Bwana aliziumba mbingu.
27 Uzuri wa ajabu na utukufu upo uweponi mwake. Uwezo na furaha upo kwake.
Fahari na enzi viko mbele yake; nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.
28 Mpeni sifa Yahweh, enyi koo za watu, mpeni sifa Yahweh utukufu na uwezo;
Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa, mpeni Bwana utukufu na nguvu,
29 Mpeni Yahweh utukufu upasao jina lake. Leta sadaka na mje kwake. Muinamieni Yahweh katika utakatifu wa uzuri wake.
mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake. Leteni sadaka na mje katika nyua zake; mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake.
30 Mtetemeke mbele zake, dunia yote. Dunia imeimarishwa; haiwezi kutikisika.
Dunia yote na itetemeke mbele zake! Ulimwengu ameuweka imara; hauwezi kusogezwa.
31 Mbingu nazo ziwe nafuraha, na dunia ifurahi; na wasema kwa mataifa yote, “Yahweh anatawala.”
Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; semeni katikati ya mataifa, “Bwana anatawala!”
32 Bahari na ingurume, na inayo ijaza ipige kelele kwa furaha. Mashamba yawe na furaha tele, na vyote vilivyomo ndani yake.
Bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake; mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo ndani yake.
33 Na miti iliyopo misituni ipige kelele kwa Yahweh, kwa kuwa anakuja kuhukumu dunia.
Kisha miti ya msituni itaimba, itaimba kwa furaha mbele za Bwana, kwa maana anakuja kuihukumu dunia.
34 Toeni shukurani kwa Yahweh, kwa kuwa ni mwema, uaminifu wa agano lake la dumu ata milele.
Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.
35 Kisha sema, “Tuokoe, Mungu wa wokovu wetu. Tukusanye pamoja na utuokoe kutoka kwa mataifa mengine, ilikwamba tutoe shukurani kwa jina lako takatifu na tufurahi katika sifa zako.”
Mlilieni, “Ee Mungu Mwokozi wetu, tuokoe. Tukusanye tena na utukomboe kutoka kwa mataifa, ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu, na kushangilia katika sifa zako.”
36 Na Yahweh, Mungu wa Israeli, asifiwe kutoka milele na milele. Watu wote wakasema, “Amina” na wakamsifu Yahweh.
Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Nao watu wote wakasema, “Amen,” na “Msifuni Bwana.”
37 Hivyo Daudi akamwacha Asafu na kaka zake pale mbele ya sanduku la Yahweh, kutumika daima mbele ya sanduku, kama kazi za kila siku zilivyo itaji. Obedi Edomu pamoja na ndugu sitini na nane walijumuishwa.
Daudi akamwacha Asafu na wenzake mbele ya Sanduku la Agano la Bwana ili wahudumu humo mara kwa mara, kulingana na mahitaji ya kila siku.
38 Obedi Edomu mwana wa Yeduthuni, pamoja na Hosa, walikuwa wawe walinzi wa lango.
Pia akamwacha Obed-Edomu pamoja na wenzake sitini na wanane wahudumu pamoja nao. Obed-Edomu mwana wa Yeduthuni na pia Hosa walikuwa mabawabu wa lango.
39 Zadoki kuhani na makuhani wenzake walikuwa watumike mbele ya hema la Yahweh katika mahali pa juu huko Gibeoni.
Daudi akamwacha kuhani Sadoki pamoja na makuhani wenzake mbele ya hema ya ibada ya Bwana katika mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni
40 Walikuwa watoe sadaka za kuteketeza kwa Yahweh kwenye madhabahu ya sadaka za kuteketeza daima asubui na jioni, kwa mujibu wa yote yalio andikwa katika amri za Yahweh, aliyo wapa Waisraeli kama sheria.
ili kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Bwana kwenye madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mara kwa mara, asubuhi na jioni, sawasawa na kila kitu kilichoandikwa katika sheria ya Bwana ambayo alikuwa amempa Israeli.
41 Hemani na Yeduthuni walikuwa nao, pamoja na walio chaguliwa kwa jina, kumpa shukurani Yahweh, kwasababu uaminifu wa agano lake la dumu ata milele
Waliohudumu pamoja nao walikuwa Hemani, Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa na kutajwa kwa jina kumpa Bwana shukrani, “Kwa maana fadhili zake zadumu milele.”
42 Hemani na Yeduthuni walikuwa viongozi wa wao waliopiga tarumbeta, upatu, na vyombo vingine kwa muziki wa kumuabudu Mungu. Wana wa Yeduthuni walilinda lango.
Hemani na Yeduthuni walikuwa na wajibu wa kupiga tarumbeta, matoazi na kutumia vyombo vingine kwa ajili ya nyimbo za sifa kwa Mungu. Wana wa Yeduthuni waliwekwa langoni.
43 Kisha watu wote walirudi nyumbani, na Daudi akarudi kubariki nyumba yake.
Kisha watu wote wakaondoka, kila mmoja akarudi nyumbani kwake, naye Daudi akarudi nyumbani kuibariki jamaa yake.

< 1 Nyakati 16 >