< 1 Nyakati 14 >

1 Kisha Hiramu mfalme wa Tire alituma wajumbe kwa Daudi, na miti ya mierezi, maseremala, na wajenzi. Walijenga nyumba kwa ajili yake.
茲にツロの王ヒラム使者をダビデに遣はし之がために家を建させんとて香柏および木匠と石工をおくれり
2 Daudi alijua kuwa Yahweh alimfanya kuwa mfalme juu ya Waisraeli, na hivyo ufalme wake ulitukuzwa juu sana kwa ajili ya watu wa Israeli
ダビデはヱホバの固く己をたててイスラエルの王となしたまへるを暁れり其はその民イスラエルの故によりてその國振ひ興りたればなり
3 Ndani ya Yerusalemu, Daudi aliongeza wake, na akawa baba wa wana wengi na mabinti.
ダビデ、ヱルサレムにおいてまた妻妾を納たり而してダビデまた男子女子を得たり
4 Haya yalikuwa majina ya watoto waliozaliwa nae huko yerusalemu: Shammua, Shobabu, nathani, Solimoni,
そのヱルサレムにて得たる子等の名は左のごとしシヤンマ、シヨバブ、ナタン、ソロモン
5 Ibhari, Elishama, Elpeleti,
イブハル、エリシユア、エルバレテ
6 Noga, Nefegi, Jafia,
ノガ、ネベグ、ヤピア
7 Elishama, Beliada, na Elifeleti.
エリシヤマ、ベエリアダ、エリバレテ
8 Sasa tangu Wafilisti waliposikia Daudi amepakwa mafuta kama mfalme juu ya Waisraeli, wote walitoka nje kwenda kumtafuta. Lakini Daudi alisikia kuhusu hilo nae akaenda nje kinyume nao.
茲にダビデの膏そそがれてイスラエル全國の王となれる事ペリシテ人に聞えければペリシテ人みなダビデを獲んとて上れりダビデは聞て之に當らんとて出たりしが
9 Sasa wafilisti walikuja na kufanya shambulio katika bonde la Refaimu.
ペリシテ人すでに來りてレバイムの谷を侵したりき
10 Kisha Daudi akaomba msaada kwa Mungu. Akasema, “Je niwashambulie Wafilisti? Utanipa ushindi juu yao?” Yahweh akamwambia, “Shambulia, kwa uhakika nitawakabidhi kwako.”
時にダビデ神に問て言けるは我ペリシテ人にむかひて攻上るべきや汝彼らを吾手に付し給ふやヱホバ、ダビデに言たまひけるは攻上れ我かれらを汝の手に付さんと
11 Kwa hivyo wakaja Baali Perazimu na akawashinda. Akasema, “Yahweh kapasua maadui zangu kwa mkono wangu kama vile mpasuko wa mafuriko ya maji.” Hivyo jina la sehemu ile likawa Baali Perazimu.
是において皆バアルベラジムに上りゆきけるがダビデつひに彼處にて彼らを打敗り而してダビデ言り神水の破壞り出るごとくに我手をもてわが敵を敗りたまへりと是をもてその處の名をバアルペラジム(破壞の處)と呼ぶなり
12 Wafilisti walitelekeza miungu yao pale, na Daudi akatoa amri wateketezwe kwa moto.
彼ら其處にその神々を遺ゆきたればダビデ命じて火をもてこれを焚せたり
13 Kisha Wafilisti wakavamia kwa mara nyingine tena.
斯て後ペリシテ人復谷を侵しければ
14 Hivyo Daudi akaomba msaada kwa Mungu tena. Mungu akamwambia, “Usiwashambulie kwa mbele, lakini wazunguke kwa nyuma yao na uwajie kupitia misitu ya balisamu.
ダビデまた神に問に神これに言たまひけるは彼らを追て上るべからず彼らを離れて回りベカの樹の方よりこれを襲へ
15 Utakaposikia sauti ya wanajeshi wanatembea kwenye upepo uvumao kutoka juu ya miti ya balisamu, kisha shambulia kwa nguvu. Fanya hivyo kwasababu Mungu atakutangulia kwenda kuwashambulia majeshi ya wafilisti.”
汝ベカの樹の上に進行の音あるを聞ば即ち進んで戰ふべし神汝のまへに進みいでペリシテ人の軍勢を撃たまふべければなりと
16 Hivyo Daudi alifanya kama Mungu alivyo muamuru. Aliwashinda jeshi la Wafilisti kutoka Gibeoni mpaka Gezeri.
ダビデすなはち神の己に命じたまひし如くしてペリシテ人の軍勢を撃やぶりつつギベオンよりガゼルにまでいたれり
17 Kisha umaarufu wa Daudi ukaenda katika nchi zote, na Yahweh akasababisha mataifa yote kumuhofia.
是においてダビデの名諸の國々に聞えわたりヱホバ諸の國人に彼を懼れしめたまへり

< 1 Nyakati 14 >