< 1 Nyakati 11 >
1 Kisha Waisraeli wote walikuja Hebroni kwa Daudi na kusema, “Angalia, sisi ni nyama na mifupa yako.
Israeli yote walimjia Daudi kwa pamoja huko Hebroni wakamwambia, “Sisi ni nyama yako na damu yako.
2 Katika wakati uliopita, Sauli alipoo kuwa mfalme juu yetu, ni wewe uliye ongoza jeshi la Israeli. Yahweh Mungu wako alisema kwako, 'utawachunga watu wangu wa Isaraeli, na utakuwa mtawala wa watu wangu wa Israeli”'.
Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani, naye Bwana Mungu wako alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’”
3 Kwaiyo wazee wote wa Israeli wakamjia mfalme huko Hebroni, na Daudi akafanya agano nao mbele ya Yahweh. Wakampaka mafuta Daudi kuwa mfalme wa Israeli. Kwa namna hii, neno la Yahweh lilo nenwa na Samweli likawa kweli.
Wazee wote wa Israeli walipokuwa wamewasili kwa Mfalme Daudi huko Hebroni, alifanya mapatano nao huko Hebroni mbele za Bwana, nao wakamtia Daudi mafuta awe mfalme wa Israeli, sawasawa na Bwana alivyoahidi kupitia kwa Samweli.
4 Daudi na Israeli yote wakaenda Yerusalemu (yani, Yebusi). Sasa Wayebusi, wakazi wa nchi, walikuwa pale.
Daudi na Waisraeli wote wakaenda Yerusalemu (ndio Yebusi). Nao Wayebusi walioishi humo
5 Wakazi wa yebusi wakamwabia Daudi, “Hautakuja humu.” Lakini Daudi alichukuwa ngome ya Sayuni, mji wa Daudi.
wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu.” Hata hivyo, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, Mji wa Daudi.
6 Daudi alisema, “Yeyote atakaye washambulia Wayebusi wa kwanza atakuwa mkuu wa jeshi” kwaiyo Yoabu mwana wa Zeruia akashambulia wa kwanza, hivyo akafanywa mkuu wa jeshi.
Daudi alikuwa amesema, “Yeyote aongozaye mashambulizi dhidi ya Wayebusi, atakuwa jemadari mkuu.” Yoabu mwana wa Seruya akawa wa kwanza kukwea, naye akawa mkuu.
7 Daudi akaanza kuishi katika hiyo ngome. Kwaiyo wakaiita mji wa Daudi.
Daudi akafanya makao yake kwenye ngome, hivyo ukaitwa Mji wa Daudi.
8 Akaimarisha mji kutoka Milo na hadi mpaka ukuta unao zunguka. Yoabu akaimairisha mji wote uliyo baki.
Akajenga mji pande zote, kuanzia kwenye mito hadi kwenye ukuta kuzunguka, wakati huo huo Yoabu akajenga sehemu zingine zilizobaki za Yerusalemu.
9 Daudi akawa mkuu na mkuu kwa sababu Yahweh wa Majeshi alikuwa naye.
Daudi akazidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi, kwa sababu Bwana Mwenye Nguvu Zote alikuwa pamoja naye.
10 Hawa walikuwa viongozi Daudi aliyo kuwa nao, waliyo jionyesha imara katika ufalme wake, pamoja na Israeli, kumfanya mfalme, kutii neno la Yahweh kuhusu Israeli.
Hawa ndio waliokuwa wakuu wa mashujaa wa Daudi: wao pamoja na Israeli wote wakauimarisha ufalme wake ili kuenea katika nchi yote, kama Bwana alivyoahidi.
11 Hii ni orodha ya wanajeshi shupavu wa Daudi. Yashobeami, mwana wa Mhakimoni, alikuwa mkuu wa kikosi cha thelathini. Aliwaua wanaume mia tatu na mkuki wake katika sehemu moja.
Hii ndio orodha ya mashujaa wa Daudi: Yashobeamu, Mhakmoni, alikuwa mkuu wa maafisa; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua katika pambano moja.
12 Baada ya yeye alikuwa Eleazari mwana wa Dodo, Mahohi, aliyekuwa mmoja wa wanaume watatu hodari.
Aliyefuata alikuwa Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu.
13 Alikuwa na Daudi huko Pasidamimu, na pale Wafilisti wakakusanyika pamoja kwa mapambano, ambapo palikuwa na uwanja wa ngano na jeshi liliwakimbia Wafilisti.
Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pas-Damimu, wakati Wafilisti walikusanyika huko kwa ajili ya vita. Huko ambapo kulikuwa na shamba lililokuwa limejaa shayiri, vikosi vya Israeli vikawakimbia Wafilisti.
14 Walisimama katikati ya uwanja. Wakautetea na kuwakata Wafilisti na Yahweh akawaokoa na ushindi mkubwa.
Lakini Eleazari na Daudi wakasimama imara katikati ya lile shamba, nao wakalishindania na wakawaua Wafilisti. Naye Bwana akawapa ushindi mkubwa.
15 Kisha watatu wa viongozi thelathini wakashuka chini kwenye mwamba wa Daudi, katika pango la Adulamu. Jeshi la Wafilisti walieka kambi katika bonde la Refaim.
Wakuu watatu miongoni mwa wale thelathini, walimwendea Daudi katika mwamba huko kwenye pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai.
16 Kwa wakati huo Daudi alikuwa katika ngome yake, pangoni, Wafilisti walikita kambi yao Bethilehemu.
Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome, na kambi ya Wafilisti ilikuwa huko Bethlehemu.
17 Daudi alikuwa na kiu ya maji na akasema, “Laiti mtu akanipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilicho Bethilehemu, kisima kilicho pembeni mwa lango!”
Daudi akatamani maji, akasema, “Laiti mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilichoko karibu na lango la Bethlehemu!”
18 Hawa wanaume hodari watatu wakatoboa kupita jeshi la Wafilisti na kuchota maji kwenye kisima cha Bethilehemu, kisima pembeni mwa lango. Wakachukuwa maji na kumletea Daudi, lakini alikataa kunywa. Badala yake, akamwaga chini kwa Yahweh.
Kwa hivyo wale watatu, wakapita katikati ya safu za Wafilisti, wakachota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za Bwana.
19 Kisha akasema, “Yahweh, iwe mbali na mimi, kwamba ni yanywe haya maji. Je ninywe damu ya wanaume walio hatarisha maisha yao?” Kwa sababu wameeka maisha ya hatarini, akakataa kunywa. Haya ni mambo wanaume hodari watatu walio fanya.
Akasema, “Mungu apishie mbali kwamba nifanye hivi! Je kweli, niinywe damu ya watu hawa waliohatarisha maisha yao?” Kwa sababu walihatarisha maisha yao kuyaleta yale maji, Daudi hakukubali kuyanywa. Huo ndio uliokuwa ujasiri wa wale mashujaa watatu.
20 Abishai kaka wa Yoabu, alikuwa kiongozi wa watatu. Alitumia mkuki wake dhidi ya watu mia tatu na kuwaua. Ametajwa pamoja na wale watatu.
Abishai, ndugu yake Yoabu ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu.
21 Kati ya wale watatu, yeye alipewa heshima mara mbili na akawa kiongozi wao. Japo hakuwa mmoja wa miongoni mwao.
Alitunukiwa heshima maradufu ya wale Watatu, akawa jemadari wao, ingawa hakuhesabiwa miongoni mwao.
22 Benaia mwana wa Yehoiada alikuwa mwanaume mwenye nguvu aliye fanya mambo makuu. Aliua wana wawili wa Arieli wa Moabu. Pia alishuka chini ya shimo na kumuua simba wakati theluji ikianguka.
Benaya, mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba.
23 Alimua hadi Mmisri, mwanaume mwenye mita mbili na theluthi moja. Mmisri alikuwa na mkuki kama gongo la mshonaji, lakini alimfuata chini na fimbo tu. Akakamata mkuki katika mkono wa Mmisri na kumuua na mkuki wake.
Alimuua Mmisri aliyekuwa na urefu kama dhiraa tano. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi mwake, Benaya alimwendea na rungu. Akamnyangʼanya Mmisri mkuki wake na kumuua nao.
24 Benaia mwana wa Yehoiada alifanya haya matukio, na akatajwa miongoni mwa wale wanaume hodari watatu.
Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu.
25 Alisifika zaidi ya wale wanajeshi thelathini kwa ujumla, lakini hakuwa pewa hadhi ya wale wanajeshi watatu hodari. Daudi alimueka kiongozi wa walinzi wake.
Yeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu: Daudi akamweka kuwa kiongozi wa walinzi wake.
26 Wanaume hodari walikuwa Asaheli kaka wa Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo wa Bethilehemu,
Wale watu mashujaa walikuwa: Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu,
27 Shamothi Mherori, Helezi Mpeloni,
Shamothi Mharori, Helesi Mpeloni,
28 Ira mwana wa Ikeshi Mtekoi, Abi Eza Manathothi,
Ira mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa, Abiezeri kutoka Anathothi,
29 Sibekai Mhushathite, Ilai Mahohite,
Sibekai Mhushathi, Ilai Mwahohi,
30 Maharai Mnetofathi, Heledi mwana wa Baana Mnetofathite,
Maharai Mnetofathi, Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi,
31 Itai mwana wa Ribai wa Gibea uzao wa Benjamini, Benaia Mpirathoni,
Itai mwana wa Ribai kutoka Gibea ya Benyamini, Benaya Mpirathoni,
32 Hurai wa mabonde ya Gaashi, Abieli Marbathi,
Hurai kutoka mabonde ya Gaashi, Abieli Mwaribathi,
33 Azmavethi Mbaharumi, Eliaba Mshaalboni,
Azmawethi Mbaharumi, Eliaba Mshaalboni,
34 Mwana wa Hashemu Mgizoni, Yonathani mwana wa Shagee Mhararite,
wana wa Hashemu Mgiloni, Yonathani mwana wa Shagee Mharari,
35 Ahiamu mwana wa Sacari Mhararite, Elifali mwana wa Uri,
Ahiamu mwana wa Sakari Mharari, Elifale mwana wa Uru,
36 Hefa Mmekarathi, Ahija Mpeloni,
Heferi Mmekerathi, Ahiya Mpeloni,
37 Hezro Mcarmeli, Maarai mwana wa Ezibai,
Hezro Mkarmeli, Naarai mwana wa Ezbai,
38 Yoeli kaka wa Nathani, Mibhari mwana wa Hagiri,
Yoeli nduguye Nathani, Mibhari mwana wa Hagri,
39 Zeleki Mamoni, Naharai Mberothi ( mbeba ngao ya Yoabu mwana wa Zeruia),
Seleki Mwamoni, Naharai Mbeerothi, mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya,
40 Ira Mithire, Garebu Mithire,
Ira Mwithiri, Garebu Mwithiri,
41 Uria Mhiti, Zabadi mwana wa Ahlai,
Uria Mhiti, Zabadi mwana wa Alai,
42 Adina mwana wa Shiza Mreubeni ( kiongozi wa Wareubeni) na thelathini pamoja nae,
Adina mwana wa Shiza Mreubeni, ambaye alikuwa mkuu wa Wareubeni, akiwa pamoja na watu thelathini,
43 Hanani mwana wa Maaka, na Yoshafati Mmithini,
Hanani mwana wa Maaka, Yoshafati Mmithni,
44 Uzia Mashiterathi, Shama na Yeieli wana wa Hothamu Waaroeri,
Uzia Mwashterathi, Shama na Yeieli wana wa Hothamu Mwaroeri,
45 Jediaeli mwana wa Shimri, Joha ( kaka yake Mtize),
Yediaeli mwana wa Shimri, nduguye Yoha Mtizi,
46 Elieli Mmahavi, Yeribai na Yoshavia mwana wa Elnaamu, Ithima Mmoabi,
Elieli Mmahawi, Yeribai na Yoshavia wana wa Elnaamu, Ithma Mmoabu,
47 Elieli, Obedi, na Yaasieli Wamezobai.
Elieli, na Obedi na Yaasieli Mmesobai.