< 1 Nyakati 10 >

1 Wafilisti wakapigana dhidi ya Israeli. Kila mwanaume wa Israeli alikimbia Wafilisti na kuanguka na kufa katika Mlima Giliboa.
Basi Wafilisti wakapigana na Israeli. Waisraeli wakawakimbia, na wengi wakauawa katika mlima Gilboa.
2 Wafilisti waliwakimbiza Sauli na mwanae. Waflisti walimuua Yonathani, Abinadabu, na Malichishua, wana wake.
Wafilisti wakawafuatia kwa bidii Sauli na wanawe, wakawaua Yonathani, Abinadabu na Malki-Shua.
3 Pambano lilikuwa zito kwa Sauli, na wapiga mishale wakamshambulia. Alipatwa na maumivu makali sababu ya wapiga mishale.
Mapigano yakawa makali kumzunguka Sauli na wakati wapiga mishale walipompata, wakamjeruhi.
4 Kisha Sauli akasema kwa mbeba ngao wake, “Vuta upanga wako na unichome nao. Lasihivyo, hawa wasio tahiriwa watukuja na kunitesa”. Lakini mbeba ngao wake hakutaka, kwa kuwa aliogopa sana. Kwa hiyo Sauli akachukuwa upanga wake na kuuangukia.
Sauli akamwambia mbeba silaha wake, “Futa upanga wako unichome nao, la sivyo hawa watu wasiotahiriwa watakuja na kunidhalilisha.” Lakini mbeba silaha wake akaogopa sana wala hakuweza kufanya hivyo. Kwa hiyo Sauli akachukua upanga wake mwenyewe na kuuangukia.
5 Mbeba ngao alivyoona kuwa Sauli amekufa, naye akaangukia upanga wake na kufa.
Mbeba silaha wake alipoona kwamba Sauli amekufa, naye pia akauangukia upanga wake akafa.
6 Kwaiyo Sauli akafa, na wana wake watatu, wote wa nyumba yake wakafa pamoja.
Kwa hiyo Sauli na wanawe watatu wakafa, pamoja na nyumba yake yote.
7 Kila mwanaume wa Israeli katika bonde alivyoona kuwa wamekimbia, na Sauli na wana wake wamekufa, walitelekeza miji yao na kukimbia. Kisha Wafilisti wakaja na kuishi humo.
Waisraeli wote waliokuwa bondeni walipoona kwamba jeshi limekimbia na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, waliacha miji yao wakakimbia. Nao Wafilisti wakaja na kukaa humo.
8 Ikawa siku inayofuata, Wafilisti walipo kuja kukagua wafu, walimkuta Sauli na wana wake wameanguka katika Mlima Giliboa.
Kesho yake Wafilisti walipokuja kuwavua maiti silaha, walimkuta Sauli na wanawe wameanguka katika Mlima Gilboa.
9 Wakamvua nguo zote na kuchukuwa kichwa chake na ngao yake. Wakatuma wajumbe wapeleke habari Filistia yote kwa miungu yao na watu wote.
Wakamvua mavazi, wakachukua kichwa chake pamoja na silaha zake, wakawatuma wajumbe katika nchi yote ya Wafilisti kutangaza habari hizi miongoni mwa sanamu zao na watu wao.
10 Ngao yake wakaeka ndani ya hekalu la miungu yao, na kichwa chake waka kining'iniza katika hekalu la Dagoni.
Waliweka silaha zake katika hekalu la miungu yao, wakatundika kichwa chake katika hekalu la Dagoni.
11 Yabeshi Gileadi yote ilipo sikia Wafilisti waliyo mtendea Sauli,
Wakazi wote wa Yabeshi-Gileadi waliposikia yote Wafilisti waliyomtendea Sauli,
12 wanaume wote wa vita wakaenda na kuchukuwa mwili wa Sauli na hiyo ya wanae, na kuirejesha Yabeshi. Walizika mifupa yao chini ya mti huko Yabeshi na wakafunga siku saba.
mashujaa wao wote wakaondoka, wakautwaa mwili wa Sauli na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi. Wakaizika mifupa yao chini ya mti mkubwa huko Yabeshi, nao wakafunga kwa siku saba.
13 Kwaiyo Sauli akafa kwa kuwa hakuwa mwaminifu kwa Yahweh. Hakutii maelekezo ya Yahweh, lakini akauliza ushauri kwa mtu anaye ongea na wafu.
Sauli alikufa kwa sababu hakuwa mwaminifu kwa Bwana. Hakulishika neno la Bwana, hata akataka shauri kwa mwaguzi kwa ajili ya uongozi,
14 Hakutafuta mwongozo kwa Yahweh, hivyo Yahweh akamua na kupindua ufalme kwa Daudi mwana wa Yese.
hakumuuliza Bwana. Kwa hiyo Bwana alimuua, na ufalme akampa Daudi mwana wa Yese.

< 1 Nyakati 10 >