< 1 Nyakati 1 >

1 Adamu, Sethi, Enoshi,
Adam Seth Enos
2 Kenani, Mahalaleli, Yaredi,
Cainan Malelehel Iared
3 Henoko, Methusela, Lameki.
Enoch Matusale Lamech
4 Wana wa Nuhu walikuwa ni Shemu, Hamu, na Yafethi.
Noe Sem Ham et Iafeth
5 Wana wa Yafethi walikuwa ni Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki, na Tirasi.
filii Iafeth Gomer Magog Madai et Iavan Thubal Mosoch Thiras
6 Wana wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Rifathi na Togama.
porro filii Gomer Aschenez et Rifath et Thogorma
7 Wana wa Yavani walikuwa ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani.
filii autem Iavan Elisa et Tharsis Cetthim et Dodanim
8 Wana wa Hamu walikuwa ni Kushi, Misri, Putu, na Kanaani.
filii Ham Chus et Mesraim Phut et Chanaan
9 Wana wa Kushi walikuwa ni Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa ni Sheba na Dedani.
filii autem Chus Saba et Evila Sabatha et Rechma et Sabathaca porro filii Rechma Saba et Dadan
10 Kushi akawa baba wa Nimrodi, aliyekuwa shujaa wa Kwanza katika dunia.
Chus autem genuit Nemrod iste coepit esse potens in terra
11 Misri akawa babu wa Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,
Mesraim vero genuit Ludim et Anamim et Laabim et Nepthuim
12 Wapathrusi, Wakasluhi (Wafilisti walipotoka), na Wakaftori.
Phethrosim quoque et Chasluim de quibus egressi sunt Philisthim et Capthurim
13 Kanaani akawa baba wa Sidoni, mwanae wa kwanza, na wa Hethi.
Chanaan vero genuit Sidonem primogenitum et Heth
14 Pia akawa babu wa Myebusi, Mwamori, Mgirgashi,
Iebuseum quoque et Amorreum et Gergeseum
15 Mhivi, Mwarki, Msini,
Evheumque et Aruceum et Asineum
16 Mwarvadi, Msemari, na Mhamathi.
Aradium quoque et Samareum et Ematheum
17 Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi, Aramu, Usi, Huli, Getheri, na Mashi.
filii Sem Aelam et Assur et Arfaxad et Lud et Aram et Us et Hul et Gothor et Mosoch
18 Arfaksadi akawa baba wa Sala, na Sala akawa baba wa Eberi.
Arfaxad autem genuit Sala qui et ipse genuit Heber
19 Eberi alikuwa na wana wawili wa kiume. Jina la wa kwanza lilikuwa Pelegi, kwa kuwa katika siku zake dunia ilikuwa imegawanyika. Jina la kaka yake lilikuwa Yoktani.
porro Heber nati sunt duo filii nomen uni Phaleg quia in diebus eius divisa est terra et nomen fratris eius Iectan
20 Yoktani akawa baba wa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
Iectan autem genuit Helmodad et Saleph et Asermoth et Iare
21 Hadoramu, Uzali, Dikla,
Aduram quoque et Uzal et Decla
22 Obali, Abimaeli, Sheba,
Ebal etiam et Abimahel et Saba necnon
23 Ofiri, Havila, na Yobabu; wote hawa walikuwa uzao wa Yoktani.
et Ophir et Evila et Iobab omnes isti filii Iectan
24 Shemu, Arfaksadi, Sala,
Sem Arfaxad Sale
25 Eberi, Pelegi, Reu,
Heber Phaleg Raau
26 Serugi, Nahori, Tera,
Serug Nahor Thare
27 Abramu, aliye kuwa Ibrahimu.
Abram iste est Abraham
28 Wana wa Ibrahimu walikuwa Isaka na Ishmaeli.
filii autem Abraham Isaac et Ismahel
29 Hawa ndio wanao: mzaliwa wa kwanza alikuwa ni Nebayothi, kisha Kedari, Abdeeli, Mibsamu,
et hae generationes eorum primogenitus Ismahelis Nabaioth et Cedar et Adbeel et Mabsam
30 Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema,
Masma et Duma Massa Adad et Thema
31 Yeturi, Nafishi, na Kedama. Hawa ndio wana wa Ishamaeli.
Iathur Naphis Cedma hii sunt filii Ismahelis
32 Wana wa Ketura, suria wa Ibrahimu, walikuwa Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki, na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa Sheba na Dedani.
filii autem Cetthurae concubinae Abraham quos genuit Zamram Iecsan Madan Madian Iesboc Sue porro filii Iecsan Saba et Dadan
33 Wana wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Hanoki, Abida, na Eldaa. Wote hawa walikuwa uzaowa Ketura.
filii autem Madian Epha et Apher et Enoch et Abida et Eldaa omnes hii filii Cetthurae
34 Ibrahimu akawa baba wa Isaka. Wana wa Isaka walikuwa Esau na Israeli.
generavit autem Abraham Isaac cuius fuerunt filii Esau et Israhel
35 Wana wa Esau walikuwa ni Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu, na Kora.
filii Esau Eliphaz Rauhel Iaus Ialam Core
36 Wana wa Elifazi walikuwa ni Temani, Omari, Sefo, Gatamu, Kenazi, Timna, na Amaleki.
filii Eliphaz Theman Omer Sepphu Gethem Cenez Thamna Amalech
37 Wana wa Reueli walikuwa ni Nahathi, Zera, Shama, na Miza.
filii Rauhel Naath Zara Samma Maza
38 Wana wa Seiri walikuwa ni Lotani, Shobali, Sebioni, Ana, Dishoni, Eseri, na Dishani.
filii Seir Lothan Sobal Sebeon Ana Dison Eser Disan
39 Wana wa Lotani walikuwa ni Hori na Hemamu, na Timna alikuwa dada yake Lotani.
filii Lothan Horri Humam soror autem Lothan fuit Thamna
40 Wana wa Shobali walikuwa ni Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo, na Onamu. Wana wa Sebeoni walikuwa ni Aya na Ana.
filii Sobal Alian et Manaath et Ebal et Sepphi et Onam filii Sebeon Aia et Ana filii Ana Dison
41 Mwana wa Ana alikuwa ni Dishoni. Wana wa Dishoni walikuwa Hemdani, Eshbani, Ithrani, na Kerani.
filii Dison Amaran et Eseban et Iethran et Charan
42 Wana wa Eseri walikuwa Bilhani, Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani walikuwa Usi na Arani.
filii Eser Balaan et Zaban et Iacan filii Dison Us et Aran
43 Hawa ndio wafalme walio tawala katika nchi ya Edomu kabla ya mfalme yeyote kuwatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori; na jina la mji wake ulikuwa Dinhaba.
isti sunt reges qui imperaverunt in terra Edom antequam esset rex super filios Israhel Bale filius Beor et nomen civitatis eius Denaba
44 Bela alipo kufa, Yohabu mwana wa Zera wa Bosra akatawala badala yake.
mortuus est autem Bale et regnavit pro eo Iobab filius Zare de Bosra
45 Yohabu alipo kufa, Hushamu wa nchi ya Watemani akatawala badala yake.
cumque et Iobab fuisset mortuus regnavit pro eo Husam de terra Themanorum
46 Hushamu alipo kufa, Hadadi mwana wa Bedadi, aliye washinda Wamidiani katika uwanja wa Moabu, akatawa badala yake. Jina la mji wake ulikuwa Avithi.
obiit quoque et Husam et regnavit pro eo Adad filius Badad qui percussit Madian in terra Moab et nomen civitatis eius Avith
47 Hadadi alipo kufa, Samla wa Masreka akatawala badala yake.
cumque et Adad fuisset mortuus regnavit pro eo Semla de Masreca
48 Samla alipo kufa, Shauli wa Rehobothi Hanahari akatawala badala yake.
sed et Semla mortuus est et regnavit pro eo Saul de Rooboth quae iuxta amnem sita est
49 Shauli alipo kufa, Baal-Hanani mwana wa Akbori akatawala badala yake.
mortuo quoque Saul regnavit pro eo Baalanan filius Achobor
50 Baal-Hanani mwana wa Akbori alipo kufa, Hadari akatawala badala yake. Jina la mji wake ni Pau. Jina la mke wake lilikuwa ni Mehetabeli binti wa Matredi binti wa Mezahabu.
sed et hic mortuus est et regnavit pro eo Adad cuius urbis fuit nomen Phou et appellata est uxor eius Mehetabel filia Matred filiae Mezaab
51 Hadadi akafa. Wajumbe wa ukoo wa Edomu walikuwa Timna, Alva, Yethethi,
Adad autem mortuo duces pro regibus in Edom esse coeperunt dux Thamna dux Alva dux Ietheth
52 Oholibama, Ela, Pinoni,
dux Oolibama dux Hela dux Phinon
53 Kenazi, Temani, Mibsari,
dux Cenez dux Theman dux Mabsar
54 Magdieli, na Iramu. Hawa ndio walikuwa wajumbe wa ukoo wa Edomu.
dux Magdihel dux Iram hii duces Edom

< 1 Nyakati 1 >