< Zekaria 8 >
1 Neno la Bwana Mwenye Nguvu Zote likanijia tena.
Now this message of the Lord of hosts came to me:
2 Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Nina wivu sana kwa ajili ya Sayuni, ninawaka wivu kwa ajili yake.”
The Lord of hosts says: I passionately care for Zion, and I am fiercely protective of her.
3 Hili ndilo asemalo Bwana: “Nitarudi Sayuni na kufanya makao Yerusalemu. Kisha Yerusalemu utaitwa mji wa kweli, mlima wa Bwana Mwenye Nguvu Zote utaitwa Mlima Mtakatifu.”
The Lord says, I have returned to Zion, and will dwell in the midst of Jerusalem and Jerusalem will be called, ‘The City of Truth’ and the mountain of the Lord of hosts, ‘The Holy Mountain.’
4 Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Kwa mara nyingine tena wazee wanaume kwa wanawake walioshiba umri wataketi katika barabara za Yerusalemu, kila mmoja akiwa na mkongojo wake mkononi kwa sababu ya umri wake.
The Lord of hosts says: Old men and old women will sit again in the squares of Jerusalem, each leaning on a staff because of old age.
5 Barabara za mji zitajaa wavulana na wasichana wanaocheza humo.”
And the streets of the city will be full of boys, and of girls playing in its squares.
6 Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Mambo haya yanaweza kuonekana ya ajabu kwa mabaki ya watu wakati huo, lakini yaweza kuwa ya ajabu kwangu?” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
The Lord of hosts says: Just because it seems impossible to the remnant of this people in these days, is it also impossible for me? says the Lord of hosts.
7 Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi za mashariki na magharibi.
The Lord of hosts says: I will rescue my people from the land of the east and the land of the west.
8 Nitawarudisha waje kuishi Yerusalemu, watakuwa watu wangu nami nitakuwa mwaminifu na wa haki kwao kama Mungu wao.”
I will bring them and they will live in Jerusalem, and they will be my people, and I will be their God, in truth and righteousness.
9 Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Ninyi ambao sasa mnasikia maneno haya yanayozungumzwa na manabii ambao walikuwepo wakati wa kuwekwa kwa msingi wa nyumba ya Bwana Mwenye Nguvu Zote, mikono yenu na iwe na nguvu ili Hekalu liweze kujengwa.
The Lord of hosts says: Let your hands be strong, you who hear in these days the words of the prophets spoken when the foundations for the house of the Lord of hosts were laid.
10 Kabla ya wakati huo, hapakuwepo na ujira kwa mtu wala mnyama. Hakuna mtu aliyeweza kufanya shughuli yake kwa usalama kwa sababu ya adui yake, kwa kuwa nilikuwa nimemfanya kila mtu adui wa jirani yake.
For before those days there were no wages for people or animals. No one could go out or return safe from enemies, because I set each against their neighbor.
11 Lakini sasa sitawatendea mabaki ya watu hawa kama nilivyowatenda zamani,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
But now I will treat the remnant of the people differently from former days, says the Lord of hosts.
12 “Mbegu itakua vizuri, mzabibu utazaa matunda yake, ardhi itatoa mazao yake, na mbingu zitadondosha umande wake. Vitu hivi vyote nitawapa mabaki ya watu kama urithi wao.
Peace will be sown. The vine will bear its fruit and the ground will yield its produce, and the skies will give their dew. I will give the remnant of this people all these things.
13 Jinsi mlivyokuwa kitu cha laana katikati ya mataifa, ee Yuda na Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa, nanyi mtakuwa baraka. Msiogope, bali iacheni mikono yenu iwe na nguvu.”
Just as you were accursed among the nations, house of Judah and house of Israel, so I will save you and you will be a blessing. Do not be afraid, but let your hands be strong.
14 Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Kama nilivyokuwa nimekusudia kuleta maangamizi juu yenu, wakati baba zenu waliponikasirisha na sikuonyesha huruma,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote,
For the Lord of hosts says: As I planned to do evil to you when your ancestors provoked me to anger, says the Lord of hosts, and I did not relent,
15 “hivyo sasa nimeazimia kufanya mema tena kwa Yerusalemu na Yuda. Msiogope.
so again have I planned in these days to do good to Jerusalem and to the house of Judah. Do not be afraid.
16 Haya ndiyo mtakayoyafanya: Semeni kweli kila mtu kwa mwenzake, na mtoe hukumu ya kweli na haki kwenye mahakama zenu,
These are the things that you should do: Speak the truth to each other. Render peaceful decisions in your gates.
17 usipange mabaya dhidi ya jirani yako, wala msipende kuapa kwa uongo. Nayachukia yote haya,” asema Bwana.
Let none of you devise evil in your heart against one another. Do not love perjury. All these are things I hate, says the Lord.
18 Neno la Bwana Mwenye Nguvu Zote likanijia tena.
And this message of the Lord of hosts came to me:
19 Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Saumu za miezi ya nne, tano, saba na kumi itakuwa sikukuu za furaha na za shangwe kwa Yuda. Kwa hiyo uipende kweli na amani.”
The Lord of hosts says: The fast of the fourth month, and the fast of the fifth, and the fast of the seventh, and the fast of the tenth, will be festivals of joy and gladness, and cheerful feasts for the house of Judah. Therefore love truth and peace.
20 Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Mataifa mengi na wakazi wa miji mingi watakuja,
The Lord of hosts says: Peoples, and the inhabitants of many cities will come,
21 na wenyeji wa mji mmoja watakwenda kwenye mji mwingine na kusema, ‘Twende mara moja na tukamsihi Bwana, na kumtafuta Bwana Mwenye Nguvu Zote. Mimi mwenyewe ninakwenda.’
and the inhabitants of one city will go to another, saying, “Let us go speedily to entreat the favor of the Lord, and to seek the Lord of hosts; I will go also.”
22 Pia watu wa kabila nyingi na mataifa yenye nguvu yatakuja Yerusalemu kumtafuta Bwana Mwenye Nguvu Zote na kumsihi.”
Many peoples and strong nations will come to seek the Lord of hosts in Jerusalem, and to entreat the favor of the Lord.
23 Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Katika siku hizo watu kumi kutoka lugha zote na mataifa, watangʼangʼania upindo wa joho la Myahudi mmoja na kusema, ‘Twende pamoja nawe kwa sababu tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nawe.’”
The Lord of hosts says: In those days ten people from all languages and nations will take hold of the robe of a Jew, saying, “We will go with you, for we have heard that God is with you.”