< Zekaria 7 >
1 Katika mwaka wa nne wa utawala wa Mfalme Dario, neno la Bwana lilimjia Zekaria siku ya nne ya mwezi wa tisa, mwezi wa Kisleu.
And it came to pass, in the fourth year of King Darius, that the word of Jehovah came to Zechariah, on the fourth day of the ninth month, even in Chisleu;
2 Watu wa Betheli walikuwa wamemtuma Shareza na Regem-Meleki pamoja na watu wao, kumsihi Bwana
when they had sent to the house of God Sherezer and Regem-melech, and their men, to pray before Jehovah,
3 kwa kuwauliza makuhani wa nyumba ya Bwana Mwenye Nguvu Zote na manabii, “Je, imempasa kuomboleza na kufunga katika mwezi wa tano, kama ambavyo nimekuwa nikifanya kwa miaka mingi?”
and to speak to the priests that were in the house of Jehovah of hosts, and to the prophets, saying, “Shall I weep in the fifth month, separating myself, as I have done these so many years?”
4 Kisha neno la Bwana Mwenye Nguvu Zote likanijia kusema:
Then came the word of Jehovah of hosts to me, saying,
5 “Waulize watu wote wa nchi na makuhani, ‘Je, mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na wa saba kwa miaka sabini iliyopita, mlifunga kweli kwa ajili yangu?
Speak to all the people of the land, and to the priests, saying, When ye fasted and mourned in the fifth month and in the seventh month, even those seventy years, did ye at all fast for me, even for me?
6 Na mlipokuwa mkila na kunywa, je, hamkuwa mnasherehekea kwa ajili ya nafsi zenu?
And when ye eat and drink, is it not ye that eat, and ye that drink?
7 Je, haya sio maneno ya Bwana aliyosema kupitia manabii waliotangulia, wakati Yerusalemu pamoja na miji inayoizunguka ilipokuwa katika hali ya utulivu na ya mafanikio, wakati Negebu na Shefala zikiwa zimekaliwa na watu?’”
Are not these the words which Jehovah proclaimed by the former prophets, when Jerusalem was inhabited and in prosperity, and her cities round about her, and when the South and the Plain were inhabited?
8 Neno la Bwana likamjia tena Zekaria:
And the word of Jehovah came to Zechariah, saying,
9 “Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Fanyeni hukumu za haki, onyesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi.
Thus spake Jehovah of hosts, saying, Judge true judgment, and show mercy and compassion every man to his brother.
10 Msimwonee mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’
And the widow, and the orphan, and the stranger, and the poor, oppress not, and meditate not evil against one another in your heart.
11 “Lakini wakakataa kusikiliza, wakanipa kisogo kwa ukaidi na kuziba masikio yao.
But they refused to hearken, and showed a refractory shoulder, and made their ears dull, that they might not hear;
12 Wakaifanya mioyo yao migumu kama jiwe gumu na hawakuisikiliza sheria au maneno ambayo Bwana Mwenye Nguvu Zote aliyatuma kwa njia ya Roho wake kupitia manabii waliotangulia. Kwa hiyo Bwana Mwenye Nguvu Zote alikasirika sana.
yea, they made their hearts as an adamant stone, that they might not hear the law, and the words which Jehovah of hosts sent through his spirit by the former prophets. Therefore came great anger from Jehovah of hosts.
13 “‘Wakati nilipoita, hawakusikiliza, kwa hiyo walipoita, sikusikiliza,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
And as he called and they would not hear, so they called and I would not hear, saith Jehovah of hosts.
14 ‘Niliwatawanya kwa upepo wa kisulisuli miongoni mwa mataifa yote, mahali ambapo walikuwa wageni. Nchi ikaachwa ukiwa nyuma yao kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuingia au kutoka. Hivi ndivyo walivyoifanya ile nchi iliyokuwa imependeza kuwa ukiwa.’”
And I scattered them as with a whirlwind among all the nations, which they knew not. And the land was desolate after them, so that no man passed through, nor returned; and thus the beautiful land was made a desolation.