< Zekaria 3 >
1 Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, akiwa amesimama mbele ya malaika wa Bwana, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshtaki.
Kisha Yahwe akanionesha Yoshua kuhani mkuu amesimama mbele za malaika wa Yahwe na Shetani amesimama mkono wake wa kushoto kumshitaki kwa ajili ya dhambi.
2 Bwana akamwambia Shetani, “Bwana akukemee Shetani! Bwana, ambaye ameichagua Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye moto?”
Malaika wa Yahwe akamwambia Shetani, “Yahwe na akukemee, Yahwe, aliyeuchagua Yerusalemu, akukemee! Je hiki si kinga kilichotolewa motoni”
3 Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika.
Yoshua alikuwa na mavazi machafu aliposimama mbele ya malaika.
4 Malaika akawaambia wale waliokuwa wamesimama mbele yake, “Mvueni hizo nguo zake chafu.” Kisha akamwambia Yoshua, “Tazama, nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mavazi ya kitajiri.”
Malaika akawaambia waliosimama mbele yake, “Mvulisheni hayo mavazi machafu.” Kisha akamwambia Yoshua, “Tazama! nimeuondoa uovu wako na nitakuvika mavazi safi.”
5 Kisha nikasema, “Mvike kilemba kilicho safi kichwani mwake.” Kwa hiyo wakamvika kilemba safi kichwani na kumvika yale mavazi mengine, wakati malaika wa Bwana akiwa amesimama karibu.
Haya wamvike kilemba safi kichwani!” Hivyo wakaweka kilemba safi kichwani pa Yoshua na wakamvika mavazi safi wakati malaika wa Yahwe amesimama kando.
6 Malaika wa Bwana akamwamuru Yoshua:
Kisha malaika wa Yahwe akamwagiza Yoshua na kusema,
7 “Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Ikiwa utakwenda katika njia zangu na kushika masharti yangu, basi utaitawala nyumba yangu na kuwa na amri juu ya nyua zangu, nami nitakupa nafasi miongoni mwa hawa wasimamao hapa.
Yahwe wa majeshi asema hivi: “Ikiwa utatembea katika njia zangu, na kutunza amri zangu, ndipo utakapoisimamia nyumba yangu na kulinda nyua zangu, kwa maana nitakuruhusu kwenda na kutoka kati ya wasimamao mbele zangu.
8 “‘Sikiliza, ee Yoshua kuhani mkuu, pamoja na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni watu walio ishara ya mambo yatakayokuja: Ninakwenda kumleta mtumishi wangu, Tawi.
WeweYoshua kuhani mkuu na wenzako wanaoishi nawe! Sikilizeni. Watu hawa ni ishara, kwa kuwa mimi mwenyewe nitamwinua mtumishi wangu aitwaye Tawi.
9 Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua! Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami nitachora maandishi juu yake,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, ‘nami nitaiondoa dhambi ya nchi hii kwa siku moja.
Tazameni jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua. Kuna macho saba juu ya jiwe hili moja, nami nitaandika maneno juu yake - asema Yahwe wa majeshi - nami nitaondoa dhambi katika nchi hii kwa siku moja.
10 “‘Katika siku hiyo kila mmoja wenu atamwalika jirani yake akae chini ya mzabibu wake na mtini wake,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.”
Katika siku hiyo kila mtu atamwalika jirani yake kukaa chini ya mzabibu na mtini wake.” asema Yahwe wa majeshi.