< Zekaria 2 >
1 Kisha nikatazama juu: pale mbele yangu alikuwepo mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake!
Kisha nikainua macho yangu na kuona mtu akiwa na timazi mkononi mwake.
2 Nikamuuliza, “Unakwenda wapi?” Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata urefu na upana wake.”
Nikamwuliza, “Unakwenda wapi?” Akaniambia, “Ninakwenda kuupima Yerusalemu ili kujua upana na urefu wake.”
3 Kisha malaika aliyekuwa akizungumza nami akaondoka, malaika mwingine akaja kukutana naye
Ndipo malaika aliyekuwa anaongea nami akaondoka na malaika mwingine akaenda kukutana naye.
4 na kumwambia: “Kimbia, umwambie yule kijana, ‘Yerusalemu utakuwa mji usio na kuta kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo.
Malaika wa pili akamwambia, “Nenda uongee na yule kijana umwambie, 'Yerusalemu utakuwa bila kuta kwa sababu ya wingi wa watu na wanyama ndani yake.
5 Mimi mwenyewe nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka,’ asema Bwana, ‘nami nitakuwa utukufu wake ndani yake.’
Kwa maana Yahwe asema, Nitakuwa ulinzi wake, na nitakuwa utukufu katikati yake.
6 “Njooni! Njooni! Kimbieni mtoke katika nchi ya kaskazini,” asema Bwana, “Kwa kuwa nimewatawanya kwenye pande nne za mbingu,” asema Bwana.
Kimbieni! kimbieni! kimbieni kutoka nchi ya kaskazini - asema Yahwe - kwa maana nimewatawanya kama pepo nne za anga! - Asema Yahwe.
7 “Njoo, ee Sayuni! Kimbia, wewe ukaaye ndani ya Binti Babeli!”
Kimbilieni Sayuni haraka! ninyi mnaokaa na binti Babeli!” Asema Yahwe.
8 Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Baada ya yeye kuniheshimu na kunituma mimi dhidi ya mataifa yaliyokuteka nyara, kwa kuwa yeyote awagusaye ninyi, anaigusa mboni ya jicho lake,
Kwa maana baada ya Yahwe wa majeshi kuniheshimu aliniweka kinyume na mataifa yaliyowateka - kwani awagusaye, agusa mboni ya jicho la Mungu! - baada ya Yahwe kutenda hivi, alisema,
9 hakika nitauinua mkono wangu dhidi yao ili watumwa wao wawateke nyara. Ndipo mtakapojua ya kwamba Bwana Mwenye Nguvu Zote amenituma.
“Mimi mwenyewe nitatikisa mkono wangu juu yao, nao watakuwa mateka kwa watumwa wao.” Ndipo mtakapojua kwamba Yahwe wa majeshi amenituma.
10 “Piga kelele na ufurahie, ee Binti Sayuni, kwa maana ninakuja, nami nitaishi miongoni mwenu,” asema Bwana.
“Imba kwa furaha, binti Sayuni, kwa maana mimi mwenyewe nitakaa nawe! - asema Yahwe
11 “Mataifa mengi yataunganishwa na Bwana siku hiyo, nao watakuwa watu wangu. Nitaishi miongoni mwenu nanyi mtajua kwamba Bwana Mwenye Nguvu Zote amenituma kwenu.
Mataifa makubwa yataungana na Yahwe siku hiyo. “Nanyi mtakuwa watu wangu; kwa kuwa nitakaa kati yenu,” nanyi mtajua kuwa Yahwe wa majeshi amenituma kwenu.
12 Bwana atairithi Yuda kama fungu lake katika nchi takatifu na atachagua tena Yerusalemu.
Kwa maana Yahwe ataimilki Yuda kama milki yake halali katika nchi takatifu na kwa mara nyingine tena atauchagua Yerusalema kwa ajili yake mwenyewe.
13 Tulieni mbele za Bwana, enyi watu wote, kwa sababu ameinuka kutoka makao yake matakatifu.”
Nyamazeni, mbele za Yahwe, ninyi wote wenye mwili, maana ameinuka kutoka mahali patakatifu pake!