< Zekaria 13 >

1 “Katika siku hiyo, chemchemi itafunguliwa kwa nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu, kuwatakasa dhambi na unajisi.
Katika siku hiyo kijito kitafunguliwa kwa ajili ya nyumba ya Daudi na wenyeji wa Yerusalemu, kwa ajili ya dhambi na uchafu wao.
2 “Katika siku hiyo, nitayakatilia mbali majina ya sanamu kutoka nchi, nayo hayatakumbukwa tena,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. “Nitaondoa manabii wao pamoja na roho ya uchafu katika nchi.
Katika siku hiyo - asema Yahwe wa majeshi - kwamba nitaondoa majina ya sanamu katika nchi ili kwamba yasikumbukwe tena. Nitawaondoa pia katika nchi manabii wa uongo na roho wao mchafu
3 Ikiwa yupo yeyote atakayeendelea kutabiri, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Ni lazima ufe, kwa sababu umesema uongo kwa jina la Bwana.’ Atakapotabiri, wazazi wake mwenyewe watampasua tumbo.
Ikiwa mtu yeyote ataendelea kutoa unabii, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, 'Hautaishi, kwa kuwa umenena uongo kwa jina la Yahwe! Ndipo baba na mama waliomzaa watakapomchoma wakati akitabiri.
4 “Katika siku hiyo, kila nabii ataaibika kwa maono ya unabii wake. Hatavaa vazi la kinabii la nywele ili apate kudanganya watu.
Katika siku hiyo kila nabii ataonea aibu maono yake aelekeapo kutoa unabii. Manabii hawa hawatavaa tena vazi la singa, ili kuwadanganya watu.
5 Atasema, ‘Mimi sio nabii. Mimi ni mkulima; ardhi imekuwa kazi yangu tangu ujana wangu.’
Kwa maana kila mmoja atasema, 'Mimi siyo nabii! mimi ni mkulima, kwa maana ardhi ndiyo kazi yangu tangu ujana wangu!
6 Ikiwa mtu atamuuliza, ‘Majeraha haya yaliyo mwilini mwako ni ya nini?’ Atajibu, ‘Ni majeraha niliyoyapata katika nyumba ya rafiki zangu.’
Lakini mtu mwingine atamwambia, 'Majeraha haya kati ya mikono yako ni ya nini?' naye atajibu, nilijeruhiwa na waliokuwa katika nyumba ya rafiki zangu.”
7 “Amka, ee upanga, dhidi ya mchungaji wangu, dhidi ya mtu aliye karibu nami!” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. “Mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika, nami nitageuza mkono wangu dhidi ya walio wadogo,
Upanga! inuka mwenyewe dhidi ya mchungaji wangu, mtu asimamaye karibu nami - hivi ndivyo asemavyo Yahwe wa majeshi. Mpige mchungaji, na kondoo watatawanyika! Kwa maana nitageuza mkono wangu dhidi ya wadogo.
8 katika nchi yote,” asema Bwana, “theluthi mbili watapigwa na kuangamia; hata hivyo theluthi moja watabaki ndani yake.
Kisha itakuwa kwamba katika nchi yote - hivi ndivyo asemavyo Yahwe - kwamba theluthi mbili yake itaondolewa! Watu hao wataangamia; theluthi moja tu ndiyo itakayosalia.
9 Hii theluthi moja nitaileta katika moto; nitawasafisha kama fedha isafishwavyo na kuwajaribu kama dhahabu. Wataliitia Jina langu nami nitawajibu; nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’ nao watasema, ‘Bwana ni Mungu wetu.’”
Nitaipitisha hiyo ya tatu motoni na kuwasafisha kama fedha isafishwavyo; nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo. Wataliitia jina langu nami nitawajibu na kusema, 'Hawa ni watu wangu!' nao watasema, Yahwe ndiye Mungu wangu!”

< Zekaria 13 >