< Wimbo wa Sulemani 4 >
1 Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! Ee, jinsi ulivyo mzuri! Macho yako nyuma ya shela yako ni kama ya hua. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi zikishuka kutoka Mlima Gileadi.
O, wewe ni mzuri, mpenzi wangu; wewe ni mzuri. Macho yako ni ya hua nyuma kitamba chako cha uso. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi likienda chini kutoka Mlima Gileadi.
2 Meno yako ni kama kundi la kondoo waliokatwa manyoya sasa hivi, watokao kuogeshwa. Kila mmoja ana pacha lake, hakuna hata mmoja aliye peke yake.
Meno yako ni kama kondoo walio nyolewa, wakitoka sehemu ya kuoshwa. Kila mmoja ana pacha, na hamna ata mmoja miongoni mwao aliyefiwa.
3 Midomo yako ni kama uzi mwekundu, kinywa chako kinapendeza. Mashavu yako nyuma ya shela yako ni kama vipande viwili vya komamanga.
Mdomo wako ni kama uzi mwekendu; mdo wako wapendeza. Mashavu yako ni kama majani ya komamanga nyuma ya kitambaa chako cha uso.
4 Shingo yako ni kama mnara wa Daudi, uliojengwa kwa madaha, juu yake zimetundikwa ngao elfu, zote ni ngao za mashujaa.
Shingo yako ni kama mnara wa Daudi ukiwa umejengwa kwa mistari ya mawe, na ngao elfu moja ikining'nia juu yake, ngao zote za wanajeshi.
5 Matiti yako mawili ni kama wana-paa wawili, kama wana-paa mapacha wajilishao katikati ya yungiyungi.
Maziwa yako mawili ni kama swala wawili, mapacha wa ayala, wakila miongoni mwa nyinyoro.
6 Hata kupambazuke na vivuli vikimbie, nitakwenda kwenye mlima wa manemane na kwenye kilima cha uvumba.
Hadi jioni ifike na vivuli viondoke, nitaenda kwenye mlima wa manemane na vilima vya ubani.
7 Wewe ni mzuri kote, mpenzi wangu, hakuna hitilafu ndani yako.
Wewe ni mzuri kwa kila namna, mpenzi wangu na hakuna lawama ndani yako.
8 Enda nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu, enda nami kutoka Lebanoni. Shuka kutoka ncha ya Amana, kutoka juu ya Seniri, kilele cha Hermoni, kutoka mapango ya simba na kutoka mlima wapendapo kukaa chui.
Njoo nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu. Njoo nami kutoka Lebanoni; njoo kutoka juu ya Amana, kutoka juu ya Seneri na Herimoni, kutoka shimoni mwa simba, kutoka mashimo ya milima ya chuwi.
9 Umeiba moyo wangu, dada yangu, bibi arusi wangu; umeiba moyo wangu kwa mtazamo mmoja wa macho yako, kwa kito kimoja cha mkufu wako.
Umeuiba moyo wangu, dada yangu, bibi arusi wangu; umeuiba moyo wangu, kwa mtazamo mmoja tu wako kwangu, kwa mkufu mmoja wa shingo yako.
10 Tazama jinsi pendo lako linavyofurahisha, dada yangu, bibi arusi wangu! Pendo lako linafurahisha aje zaidi ya divai, na harufu ya manukato yako zaidi ya kikolezo chochote!
Jinisi gani upendo wako ulivyo mzuri, dada yangu, bibi arusi wangu! Jinsi gani zaidi upendo wako ulivyo bora kuliko mvinyo, na arufu ya marashi yako kuliko manukato yeyote.
11 Midomo yako inadondosha utamu kama sega la asali, bibi arusi wangu; maziwa na asali viko chini ya ulimi wako. Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ile ya Lebanoni.
Midomo yako, bibi arusi wangu, yatiririka asali; asali na maziwa vichini ya ulimi wako; arufu ya mavazi yako ni kama marashi ya Lebanoni.
12 Wewe ni bustani iliyofungwa, dada yangu, bibi arusi wangu; wewe ni chanzo cha maji kilichozungushiwa kabisa, chemchemi yangu peke yangu.
Dada yangu, bibi arusi wangu ni bustani ilio fungwa, bustani ilio fungwa, chemchemi iliyo fungwa kwa muhuri.
13 Mimea yako ni bustani ya mikomamanga yenye matunda mazuri sana, yenye hina na nardo,
Matawi yako ni kichaka cha miti ya komamanga yenye matunda tofauti, na ya mimea ya hina na nardo,
14 nardo na zafarani, mchai na mdalasini, pamoja na kila aina ya mti wa uvumba, manemane na udi, na aina zote za vikolezo bora kuliko vyote.
Nardo na Zafarani, mchai na mdalasini pamoja na aina zote za uvumba, manemane na udi na aina tofauti za manukato.
15 Wewe ni chemchemi ya bustani, kisima cha maji yatiririkayo, yakitiririka kutoka Lebanoni.
Wewe ni bustani ya chemchemi, kisima cha maji safi, mifereji inayo shuka kutoka Lebanoni. Mwanamke mdogo akizungumza peke yake
16 Amka, upepo wa kaskazini, na uje, upepo wa kusini! Vuma juu ya bustani yangu, ili harufu yake nzuri iweze kuenea mpaka ngʼambo. Mpendwa wangu na aje bustanini mwake na kuonja matunda mazuri sana.
Amka, upepo wa kaskazini; njoo, upepo wa kusini; vuma katika bustani yangu ili manukato yake yatoe marashi. Mpenzi wangu na aje katika bustani yake na kula matunda ya chaguo lake.