< Wimbo wa Sulemani 4 >
1 Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! Ee, jinsi ulivyo mzuri! Macho yako nyuma ya shela yako ni kama ya hua. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi zikishuka kutoka Mlima Gileadi.
我的佳偶,你甚美丽!你甚美丽! 你的眼在帕子内好像鸽子眼。 你的头发如同山羊群卧在基列山旁。
2 Meno yako ni kama kundi la kondoo waliokatwa manyoya sasa hivi, watokao kuogeshwa. Kila mmoja ana pacha lake, hakuna hata mmoja aliye peke yake.
你的牙齿如新剪毛的一群母羊, 洗净上来,个个都有双生, 没有一只丧掉子的。
3 Midomo yako ni kama uzi mwekundu, kinywa chako kinapendeza. Mashavu yako nyuma ya shela yako ni kama vipande viwili vya komamanga.
你的唇好像一条朱红线; 你的嘴也秀美。 你的两太阳在帕子内, 如同一块石榴。
4 Shingo yako ni kama mnara wa Daudi, uliojengwa kwa madaha, juu yake zimetundikwa ngao elfu, zote ni ngao za mashujaa.
你的颈项好像大卫建造收藏军器的高台, 其上悬挂一千盾牌, 都是勇士的藤牌。
5 Matiti yako mawili ni kama wana-paa wawili, kama wana-paa mapacha wajilishao katikati ya yungiyungi.
你的两乳好像百合花中吃草的一对小鹿, 就是母鹿双生的。
6 Hata kupambazuke na vivuli vikimbie, nitakwenda kwenye mlima wa manemane na kwenye kilima cha uvumba.
我要往没药山和乳香冈去, 直等到天起凉风、 日影飞去的时候回来。
7 Wewe ni mzuri kote, mpenzi wangu, hakuna hitilafu ndani yako.
我的佳偶,你全然美丽, 毫无瑕疵!
8 Enda nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu, enda nami kutoka Lebanoni. Shuka kutoka ncha ya Amana, kutoka juu ya Seniri, kilele cha Hermoni, kutoka mapango ya simba na kutoka mlima wapendapo kukaa chui.
我的新妇,求你与我一同离开黎巴嫩, 与我一同离开黎巴嫩。 从亚玛拿顶, 从示尼珥与黑门顶, 从有狮子的洞, 从有豹子的山往下观看。
9 Umeiba moyo wangu, dada yangu, bibi arusi wangu; umeiba moyo wangu kwa mtazamo mmoja wa macho yako, kwa kito kimoja cha mkufu wako.
我妹子,我新妇, 你夺了我的心。 你用眼一看, 用你项上的一条金链, 夺了我的心!
10 Tazama jinsi pendo lako linavyofurahisha, dada yangu, bibi arusi wangu! Pendo lako linafurahisha aje zaidi ya divai, na harufu ya manukato yako zaidi ya kikolezo chochote!
我妹子,我新妇, 你的爱情何其美! 你的爱情比酒更美! 你膏油的香气胜过一切香品!
11 Midomo yako inadondosha utamu kama sega la asali, bibi arusi wangu; maziwa na asali viko chini ya ulimi wako. Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ile ya Lebanoni.
我新妇,你的嘴唇滴蜜, 好像蜂房滴蜜; 你的舌下有蜜,有奶。 你衣服的香气如黎巴嫩的香气。
12 Wewe ni bustani iliyofungwa, dada yangu, bibi arusi wangu; wewe ni chanzo cha maji kilichozungushiwa kabisa, chemchemi yangu peke yangu.
我妹子,我新妇, 乃是关锁的园, 禁闭的井,封闭的泉源。
13 Mimea yako ni bustani ya mikomamanga yenye matunda mazuri sana, yenye hina na nardo,
你园内所种的结了石榴, 有佳美的果子, 并凤仙花与哪哒树。
14 nardo na zafarani, mchai na mdalasini, pamoja na kila aina ya mti wa uvumba, manemane na udi, na aina zote za vikolezo bora kuliko vyote.
有哪哒和番红花, 菖蒲和桂树, 并各样乳香木、没药、沉香, 与一切上等的果品。
15 Wewe ni chemchemi ya bustani, kisima cha maji yatiririkayo, yakitiririka kutoka Lebanoni.
你是园中的泉,活水的井, 从黎巴嫩流下来的溪水。
16 Amka, upepo wa kaskazini, na uje, upepo wa kusini! Vuma juu ya bustani yangu, ili harufu yake nzuri iweze kuenea mpaka ngʼambo. Mpendwa wangu na aje bustanini mwake na kuonja matunda mazuri sana.
北风啊,兴起! 南风啊,吹来! 吹在我的园内, 使其中的香气发出来。 愿我的良人进入自己园里, 吃他佳美的果子。