< Wimbo wa Sulemani 3 >

1 Usiku kucha kwenye kitanda changu nilimtafuta yule moyo wangu umpendaye; nilimtafuta, lakini sikumpata.
Usiku katika kitanda changu nilikuwa na shauku ya yeye ni mpendaye; nilimtafuta, lakini sikumpata.
2 Sasa nitaondoka na kuzunguka mjini, katika barabara zake na viwanja; nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye. Kwa hiyo nilimtafuta lakini sikumpata.
Nilisema binafsi, “Nitainuka na kwenda kupitia mji, kupitia mitaa na sokoni; nitamtafuta.” Nilimtafuta, lakini sikumpata.
3 Walinzi walinikuta walipokuwa wakizunguka mji. Nikawauliza, “Je, mmemwona yule moyo wangu umpendaye?”
Walinzi walinipata walipo kuwa doria katika mji. Nikawauliza, “Mmemuona mpenzi wangu?”
4 Kitambo kidogo tu baada ya kuwapita nilimpata yule moyo wangu umpendaye. Nilimshika na sikumwachia aende mpaka nilipomleta katika nyumba ya mama yangu, katika chumba cha yule aliyenichukua mimba.
Ni baada ya mda mfupi kupita nilipo wapita nikampata ninaye mpenda. Nilimshika na sikumuacha hadi nilipo mleta nyumbani mwa mama yangu, katika chumba cha yeye aliyenichukua mimba. Mwanamke akiongea na wanawake wengine.
5 Binti za Yerusalemu, ninawaagiza kwa paa na kwa ayala wa shambani: Msichochee wala kuamsha mapenzi hata yatakapotaka yenyewe.
Ninataka muape, mabinti wa wanaume waYerusalemu, kwa ayala na paa wa porini, kuwa hamtavuruga mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
6 Ni nani huyu anayekuja kutoka jangwani kama nguzo ya moshi, anayenukia manemane na uvumba iliyotengenezwa kwa vikolezo vyote vya mfanyabiashara?
Nini hiyo inayo toka nyikani kama nguzo za moshi, umefukizwa manemane na ubani, pamoja na unga wote wa manukato unao uzwa na wafanya biashara?
7 Tazama! Ni gari la Solomoni lisindikizwalo na mashujaa sitini, walio wakuu sana wa Israeli,
Angalia, nikitanda cha Sulemani; mashujaa sitini wamekizunguka, wanajeshi elfu sitini wa Israeli
8 wote wamevaa panga, wote wazoefu katika vita, kila mmoja na upanga wake pajani, wamejiandaa kwa ajili ya hofu za usiku.
Wao ni wazoefu wa upanga na wanaujuzi wa vita. Kila mwanaume ana upanga wake pembeni yake, akijizatiti na maasi ya usiku.
9 Mfalme Solomoni alijitengenezea gari; alilitengeneza kwa mbao kutoka Lebanoni.
Mfalme Sulemani akajijengea kiti cha kifalme cha kubebwa na mbao za Lebanoni.
10 Nguzo zake alizitengeneza kwa fedha, kitako chake kwa dhahabu. Kiti chake kilipambwa kwa zambarau, gari lake likanakshiwa njumu kwa upendo na binti za Yerusalemu.
Nguzo zake zilijengwa kwa fedha; nyuma kuliekwa dhahabu, na kiti kitambaa cha zambarau. Ndani mwake kulipambwa na upendo na mabinti wa wanaume wa Yerusalemu. Mwanamke mdogo akizungumza na wanawake wa Yerusalemu
11 Tokeni nje, ninyi binti za Sayuni, mkamtazame Mfalme Solomoni akiwa amevaa taji, taji ambalo mama yake alimvika siku ya arusi yake, siku ambayo moyo wake ulishangilia.
Nenda nje, mabinti wa wanaume wa Sayuni, na mtazame mfalme Sulemani, akivikwa taji ambalo mamaye alimvika siku ya arusi yake, katika siku ya furaha ya maisha yake.

< Wimbo wa Sulemani 3 >