< Wimbo wa Sulemani 2 >

1 Mimi ni ua la Sharoni, yungiyungi ya bondeni.
Mimi ni ua katika tambarare, nyinyoro katika bonde. Mwanaume akizungumza naye
2 Kama yungiyungi katikati ya miiba ndivyo alivyo mpenzi wangu katikati ya wanawali.
Kama nyinyoro miongoni mwa mimba, ndivyo wewe, mpenzi wangu, miongoni mwa mabinti wengine wote. Mwanamke akizungumza mwenyewe
3 Kama mti wa mtofaa miongoni mwa miti ya msituni ndivyo alivyo mpenzi wangu miongoni mwa wanaume vijana. Ninafurahia kuketi kivulini mwa mwanaume huyu, na tunda lake ni tamu kwangu.
Kama mti wa mpera ulivyo miongoni mwa miti ya misituni, ndivyo mpenzi wangu alivyo miongoni mwa wanaume. Nina kaa chini ya kivuli chake kwa furaha sana, na tunda lake ni tamu kwa ladha yangu.
4 Amenichukua mpaka kwenye ukumbi wa karamu, na bendera ya huyu mwanaume juu yangu ni upendo.
Amenileta kwenye ukumbi wa maakuli, na bendera yake juu yangu ilikuwa upendo. Mwanamke akizungumza na mpenzi wake.
5 Nitie nguvu kwa zabibu kavu, niburudishe kwa matofaa, kwa maana ninazimia kwa mapenzi.
Ni uishe kwa keki za mizabibu na kuniuisha na mapera, kwa kuwa nimedhohofika na mapenzi. Mwanamke akizungumza mwenyewe
6 Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu, na mkono wake wa kuume unanikumbatia.
Mkono wake wakushuto upo chini ya kichwa changu, na mkono wake wa kulia wanikumbatia. Mwanamke akizungumza na wanawake wengine.
7 Binti za Yerusalemu, ninawaagiza kwa paa na kwa ayala wa shambani: Msichochee wala kuamsha mapenzi hata yatakapotaka yenyewe.
Ninataka muhaidi, mabinti wa Yerusalemu, kwa swala na paa wa porini, kwamba hamtavuruga mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe. Mwanamke akizungumza mwenyewe.
8 Sikiliza! Mpenzi wangu! Tazama! Huyu hapa anakuja, akirukaruka juu milimani akizunguka juu ya vilima.
Sauti ya mpenzi wangu hiyo! O, huyu yuwaja, akiruka ruka juu milima, akiruka vilimani.
9 Mpenzi wangu ni kama paa au ayala kijana. Tazama! Anasimama nyuma ya ukuta wetu, akitazama kupitia madirishani, akichungulia kimiani.
Mpenzi wangu ni kama swala au mtoto mdogo wa paa; angalia, amesimama nyuma ya ukuta wetu, akishangaa kupitia dirishani, akichungulia wavuni.
10 Mpenzi wangu alizungumza na kuniambia, “Inuka, mpenzi wangu, mrembo wangu, tufuatane.
Mpenzi wangu alizungumza na mimi na kusema, “Amka, mpenzi wangu; mzuri wangu, twende pamoja nami.
11 Tazama! Wakati wa masika umepita, mvua imekwisha na ikapita.
Angalia, baridi imepita; mvua imeisha na kwenda.
12 Maua yanatokea juu ya nchi; majira ya kuimba yamewadia, sauti za njiwa zinasikika katika nchi yetu.
Maua yametokeza juu ya nchi; wakati wa kupunguza matawi na kuimba kwa ndege umekuja, na sauti za hua zimesikika nchini kwetu.
13 Mtini unatunga matunda yake ya mwanzoni, zabibu zinazochanua zaeneza harufu nzuri. Inuka, njoo mpenzi wangu. Mrembo wangu, tufuatane.”
Mti wa tini umepevusha tini zake za kijani, na mizabibu imestawi; yatoa marashi yake. Inuka, mpenzi wangu, mzuri wangu, na uje nami.
14 Hua wangu penye nyufa za majabali, mafichoni pembezoni mwa mlima, nionyeshe uso wako, na niisikie sauti yako, kwa maana sauti yako ni tamu, na uso wako unapendeza.
Hua wangu, katika miamba ya mawe, katika miamba ya siri ya mipasuko ya milima, acha nione uso wako. Acha nisikie sauti yako, kwa kuwa sauti ni tamu, na uso wako ni mzuri.” Mwanamke akiongea mwenyewe
15 Tukamatie mbweha, mbweha wale wadogo wanaoharibu mashamba ya mizabibu, mashamba yetu ya mizabibu yaliyochanua.
Wakamate mbweha kwa ajili yetu, mbweha wadogo wanao haribu shamba za mizabibu, kwa kuwa shamba la mizabibu limestawi.
16 Mpenzi wangu ni wangu, nami ni wake, yeye hujilisha katikati ya yungiyungi.
Mpenzi wangu ni wangu, na mimi ni wake; anakula penye nyinyoro kwa raha. Mwanamke anaongea na mpenzi wake
17 Mpaka jua linapochomoza, na vivuli vikimbie, rudi, mpenzi wangu, na uwe kama paa, au kama ayala kijana juu ya vilima vya Betheri.
Enenda zako, mpenzi wangu, kabla pepo za jioni hazija vuma na vivuli kutoweka. Nenda zako; kuwa kama ayala au mtoto mdogo wa paa katika milima mawe mengi.

< Wimbo wa Sulemani 2 >