< Wimbo wa Sulemani 2 >
1 Mimi ni ua la Sharoni, yungiyungi ya bondeni.
I am a rose of Sharon, a lily of the valleys.
2 Kama yungiyungi katikati ya miiba ndivyo alivyo mpenzi wangu katikati ya wanawali.
As a lily among thorns, so is my love among the daughters.
3 Kama mti wa mtofaa miongoni mwa miti ya msituni ndivyo alivyo mpenzi wangu miongoni mwa wanaume vijana. Ninafurahia kuketi kivulini mwa mwanaume huyu, na tunda lake ni tamu kwangu.
As the apple tree among the trees of the wood, so is my beloved among the sons. I sat down under his shadow with great delight, his fruit was sweet to my taste.
4 Amenichukua mpaka kwenye ukumbi wa karamu, na bendera ya huyu mwanaume juu yangu ni upendo.
He brought me to the banquet hall. His banner over me is love.
5 Nitie nguvu kwa zabibu kavu, niburudishe kwa matofaa, kwa maana ninazimia kwa mapenzi.
Strengthen me with raisins, refresh me with apples; for I am faint with love.
6 Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu, na mkono wake wa kuume unanikumbatia.
His left hand is under my head. His right hand embraces me.
7 Binti za Yerusalemu, ninawaagiza kwa paa na kwa ayala wa shambani: Msichochee wala kuamsha mapenzi hata yatakapotaka yenyewe.
I adjure you, daughters of Jerusalem, by the roes, or by the hinds of the field, that you not stir up, nor awaken love, until it so desires.
8 Sikiliza! Mpenzi wangu! Tazama! Huyu hapa anakuja, akirukaruka juu milimani akizunguka juu ya vilima.
The voice of my beloved! Behold, he comes, leaping on the mountains, skipping on the hills.
9 Mpenzi wangu ni kama paa au ayala kijana. Tazama! Anasimama nyuma ya ukuta wetu, akitazama kupitia madirishani, akichungulia kimiani.
My beloved is like a roe or a young deer. Behold, he stands behind our wall! He looks in at the windows. He glances through the lattice.
10 Mpenzi wangu alizungumza na kuniambia, “Inuka, mpenzi wangu, mrembo wangu, tufuatane.
My beloved spoke, and said to me, “Rise up, my love, my beautiful one, and come away.
11 Tazama! Wakati wa masika umepita, mvua imekwisha na ikapita.
For behold, the winter is past. The rain is over and gone.
12 Maua yanatokea juu ya nchi; majira ya kuimba yamewadia, sauti za njiwa zinasikika katika nchi yetu.
The flowers appear on the earth. The time of the singing has come, and the voice of the turtledove is heard in our land.
13 Mtini unatunga matunda yake ya mwanzoni, zabibu zinazochanua zaeneza harufu nzuri. Inuka, njoo mpenzi wangu. Mrembo wangu, tufuatane.”
The fig tree ripens her green figs. The vines are in blossom. They give out their fragrance. Arise, my love, my beautiful one, and come away.”
14 Hua wangu penye nyufa za majabali, mafichoni pembezoni mwa mlima, nionyeshe uso wako, na niisikie sauti yako, kwa maana sauti yako ni tamu, na uso wako unapendeza.
My dove in the clefts of the rock, in the hiding places of the mountainside, let me see your face. Let me hear your voice; for your voice is sweet and your face is lovely.
15 Tukamatie mbweha, mbweha wale wadogo wanaoharibu mashamba ya mizabibu, mashamba yetu ya mizabibu yaliyochanua.
Catch for us the foxes, the little foxes that plunder the vineyards; for our vineyards are in blossom.
16 Mpenzi wangu ni wangu, nami ni wake, yeye hujilisha katikati ya yungiyungi.
My beloved is mine, and I am his. He browses among the lilies.
17 Mpaka jua linapochomoza, na vivuli vikimbie, rudi, mpenzi wangu, na uwe kama paa, au kama ayala kijana juu ya vilima vya Betheri.
Until the day is cool, and the shadows flee away, turn, my beloved, and be like a roe or a young deer on the mountains of Bether.