< Ruth 3 >
1 Kisha Naomi akamwambia mkwewe, “Binti yangu, je, nisingelikutafutia pumziko ambako utatunzika vyema?
Naomi, mama mkwe wake, alimwambia, “Mwanangu, hainilazimu kutafuta mahali pa wewe kupumzika, ili kwamba mambo yako yaende vizuri?
2 Je, Boazi, ambaye umekuwa pamoja na watumishi wake wasichana, si jamaa yetu wa karibu? Usiku wa leo atakuwa anapepeta ngano kwenye sakafu ya kupuria.
Naye Boazi, mtu ambaye umekuwa pamoja na wasichana wake wa kazi, yeye si jamaa yetu? Tazama, jioni hii atakuwa akikung'uta shairi katika sakafu ya kupuria.
3 Basi oga na ukajipake marashi, ujivalie nguo zako nzuri. Kisha uende kwenye sakafu ya kupuria, lakini angalia asijue kwamba upo pale mpaka atakapomaliza kula na kunywa.
Kwa hiyo, oga, jipake mafuta, uvae nguo zako nzuri, na ushuke kwenda kwenye sakafu ya kupuria. Lakini usijulikane kwa mtu huyu mpaka atakapo maliza kula na kunywa.
4 Atakapokwenda kulala, angalia mahali atakapolala. Kisha uende ufunue miguu yake, ulale. Naye atakuambia utakalofanya.”
Na uhakikishe kuwa, atakapo lala chini, ukumbuke mahali alipo lala ili kwamba baadaye uende kwake, ufunue miguu yake, na ulale hapo. Kisha atakuambia cha kufanya.”
5 Ruthu akajibu, “Lolote usemalo nitatenda.”
Ruth alimwambia Naomi, “Nitafanya kila kitu ulicho sema.”
6 Basi akashuka mpaka kwenye sakafu ya kupuria, akafanya kila kitu mama mkwe wake alichomwambia kufanya.
Alishuka kwenda kwenye sakafu ya kupuria, na alifuata maelekezo aliyopewa na mama mkwe wake.
7 Wakati Boazi alipomaliza kula na kunywa, naye akawa amejawa na furaha, alikwenda kulala mwisho wa lundo la nafaka. Ruthu akanyemelea polepole, akafunua miguu yake, na akalala.
Boazi alipomaliza kula na kunywa na moyo wake ulikuwa na furaha, alienda kulala chini mwisho wa sehemu ya kuhifadhia nafaka. Kisha Ruth akaenda taratibu, akaaifunua miguu ya Boazi, na kulala hapo chini.
8 Usiku wa manane, kitu kilimshtua Boazi, akajigeuza, akagundua yupo mwanamke amelala miguuni pake.
Panapo usiku wa manane Boazi alisituka. Akajigeuza, na hapo mwanamke alikuwa amelala katika miguu yake!
9 Akauliza, “Wewe ni nani?” Akajibu, “Ni mimi Ruthu, mjakazi wako. Uitande nguo yako juu yangu, kwa sababu wewe ndiwe jamaa wa karibu wa kutukomboa.”
Akamwambia, “Wewe ni nani?” Akajibu, “Mimi ni Ruth, mtumishi wako wa kike. Nifunike shuka lako mimi mtumishi wako wa kike, kwa kuwa wewe ni jamaa wa karibu.”
10 Akamwambia, “Binti yangu, ubarikiwe na Bwana. Wema huu wa sasa ni mkuu kushinda hata ule ulioonyesha mwanzoni. Hukuwakimbilia vijana, wakiwa matajiri au maskini.
Boazi akamwambia, “Mwanangu, Yahweh akubariki. Umeonyesha wema mwishoni kuliko mwazoni, kwa sababu hukwenda kwa wanaume vijana, awe tajiri au masikini.
11 Sasa, binti yangu, usiogope. Nitakufanyia yote uliyoomba. Kwa maana mji wote wa watu wangu wanakujua ya kwamba wewe ni mwanamke mwenye tabia nzuri.
Na sasa, mwanangu, usiogope! Nitakufanyia yote unayosema, kwa sababu mji wa watu wangu wote wanajua kuwa wewe ni mwanamke unayestahili.
12 Ingawa ni kweli kwamba mimi ndiye jamaa aliye karibu, bado kuna mtu mwingine wa jamaa aliye karibu zaidi wa kukomboa kuliko mimi.
Nikweli kuwa mimi ni jamaa wa karibu; hata hivyo, kuna jamaa wa karibu kuliko mimi.
13 Wewe kaa hapa usiku huu, kisha asubuhi kama akikubali kukomboa, vyema na akomboe. La sivyo kama hayuko tayari, hakika kama Bwana aishivyo nitafanya hivyo. Lala hapa mpaka asubuhi.”
Baki hapa usiku huu, na asubuhi, ikiwa atafanya jukumu lake la jamaa wa karibu, vizuri, muache afanye jukumu lake la kindugu. lakini kama hata fanya jukumu la kindugu kwako, ndipo mimi nitafanya, kama Yahweh aishivyo. Lala mpaka asubuhi.”
14 Hivyo huyo mwanamke akalala miguuni pake mpaka asubuhi, akaondoka mapema pasipo mtu kuweza kumtambua mwenzake, maana Boazi alisema, “Isijulikane kabisa ya kuwa mwanamke alifika kwenye sakafu ya kupuria.”
Kwa hiyo Ruth alilala kwenye miguu ya Boazi hadi asubuhi. Lakini aliamka mapema kabla ya yeyote kuweza kumtambua mtu mwingine. Kwa kuwa alikwisha mwambia, “Isijulikane kuwa mwanamke alikuja kwenye sakafu ya kupuria.”
15 Pia akamwambia, “Leta shela yako uliyoivaa, uitandaze.” Naye alipoitandaza, akamimina vipimo sita vya shayiri, akamtwika. Kisha Ruthu akarudi zake mjini.
Kisha Boazi akamwambia, lete mtandio wako na uushikilie.” Alipo fanya hivyo, alipima vipimo vikubwa sita vya shairi katika mtandio na kumtwisha Ruth. Kisha Boazi akaenda mjini.
16 Basi Ruthu alipofika kwa mama mkwe wake Naomi, akamuuliza, “Je, binti yangu, ilikuwaje huko?” Ndipo akamwelezea kila kitu Boazi alichomfanyia.
Ruth aliporudi kwa mama mkwe wake, alisema, “Ulifanyaje, mwanangu?” Ndipo Ruth akamwambia mambo yote aliyotendewa na mtu huyo.
17 Akaendelea kusema, “Amenipa shayiri vipimo sita akisema, ‘Usiende kwa mama mkwe wako mikono mitupu.’”
Alimwambia, “Hivi vipimo sita vya shairi ni vile alivyonipa yeye, kwa kuwa alisema, 'Usiende mikono mitupu kwa mama mkwe wako.'”
18 Kisha Naomi akasema, “Subiri binti yangu, mpaka utakapojua kwamba hili jambo limekwendaje. Kwa sababu mtu huyu hatatulia mpaka akamilishe jambo hili leo.”
Kisha Naomi akasema, “Baki hapa, mwanangu, mpaka utakapojua yatakavyo kuwa, kwa kuwa Boazi hata pumzika mpaka atakapolimaliza jambo hili leo.”