< Ruth 1 >

1 Wakati Waamuzi walipotawala Israeli, kulikuwa na njaa katika nchi. Mtu mmoja kutoka nchi ya Bethlehemu ya Yuda, pamoja na mke wake na wanawe wawili, akaenda kuishi katika nchi ya Moabu.
Ilitokea katika siku za utawala wa majaji kuwa kulikuwa na njaa katika nchi, na mtu mmoja wa Bethelehemu ya Yuda alikwenda katika nchi ya Moabu pamoja na mke wake na watoto wake walili wa kiume.
2 Mtu huyu aliitwa Elimeleki, mkewe aliitwa Naomi, na hao wanawe wawili waliitwa Maloni na Kilioni. Walikuwa Waefrathi kutoka Bethlehemu ya Yuda. Wakaenda katika nchi ya Moabu, wakaishi huko.
Jina la mtu huyo lilikuwa Elimeleki, na jina la mke wake lilikuwa Naomi. Majina ya watoto wake wawili wa kiume waliitwa Mahiloni na Kileoni, ambao walikuwa Waefraimu wa Betherehemu ya Yuda. Waliwasili katika nchi ya Moabu na kuishi hapo.
3 Elimeleki mumewe Naomi akafa, hivyo Naomi akabaki na wanawe wawili.
Ndipo Elimeleki, mume wa Naomi, alikufa, na Naomi aliachwa na watoto wake wa kiume wawili.
4 Nao wakaoa wanawake Wamoabu, jina la mmoja aliitwa Orpa, na wa pili aliitwa Ruthu. Baada ya kama miaka kumi,
Watoto hawa walioa wanawake wa Moabu; jina la mmoja lilikuwa Oripa, na jina la mwingine lilikuwa Ruth. waliishi huko kwa takribani miaka kumi.
5 Maloni na Kilioni pia wakafa. Basi Naomi akabaki hana mume wala wanawe wawili.
Kisha wote Mahiloni na Kileoni walikufa, na kumuacha Naomi bila mme wake na bila watoto wake wawili.
6 Aliposikia akiwa huko Moabu kwamba Bwana amewasaidia watu wake kwa kuwapa chakula, Naomi na wakweze wakajiandaa kurudi nyumbani.
Ndipo Naomi aliamua kuondoka Moabu pamoja na wake wa watoto wake na kurudi Yuda kwa sababu alikuwa amesikia katika mkoa wa Moabu kuwa Yahweh amewasaidia watu wake katika uhitaji na amewapa chakula.
7 Yeye na wakweze wawili wakaondoka pale walipokuwa wakiishi na kushika njia kurudi nchi ya Yuda.
Hivyo aliondoka sehemu aliyokuwa pamoja na wake wa watoto wake wawili, walitelemka njia kurudi kwenye nchi ya Yuda.
8 Ndipo Naomi akawaambia wale wakwe zake wawili, “Rudini, kila mmoja wenu nyumbani kwa mama yake. Bwana na awatendee fadhili kama mlivyowatendea hao waliofariki, na pia mimi.
Naomi aliwaambia wake wa watoto wake, “Nendeni, mrudi, kila mmoja wenu, kwenye nyumba ya mama yake. na Mungu aonyeshe wema juu yenu, kama mlivyo onyesha wema kwao waliokufa na kwangu.
9 Bwana na amjalie kila mmoja wenu maisha mema nyumbani kwa mume mwingine.” Kisha akawabusu, nao wakalia kwa sauti kubwa,
Mungu awajalie ninyi kupata pumziko, kila mmoja wenu katika nyumba ya mme mwingine.” Kisha akawabusu, na wakapaza sauti zao na kulia.
10 wakamwambia, “Tutarudi pamoja na wewe nyumbani kwa watu wako.”
Wakamwambia, “Hapana! tutarudi pamoja na wewe kwa watu wako.”
11 Lakini Naomi akasema, “Rudini nyumbani, binti zangu. Kwa nini mnifuate? Je, mimi nitaweza tena kuwa na wana wengine ambao wataweza kuwaoa ninyi?
Lakini Naomi alisema, “Rudini, wanangu! Kwa nini mtakwenda na mimi? Kwani bado nina watoto katika tumbo langu kwa ajili yenu, ili kwamba waje wawe waume zenu?
12 Rudini nyumbani, binti zangu; mimi ni mzee kiasi kwamba siwezi kumpata mume mwingine. Hata kama ningefikiria kuwa bado kuna tumaini kwangu, hata kama ningekuwa na mume usiku huu na kuwazaa wana,
Rudini, wanangu, nendeni katika njia zenu wenyewe, kwa kuwa mimi ni mzee sana kuwa na mme. Kama nikisema, 'Natumaini nipate mume usiku huu,' na kisha kuzaa watoto wakiume, kwa hiyo mnaweza kusubiri mpaka wakue?
13 je, mngesubiri mpaka wakue? Mngebakia bila kuolewa mkiwasubiri? La, hasha, binti zangu. Nimepata uchungu kuliko ninyi, kwa sababu mkono wa Bwana umekuwa kinyume nami!”
Mtasubiri na msiolewe sasa? Hapana, wanangu! Ina nihuzunisha zaidi, kuliko inavyo wahuzunisha ninyi, kwa sababu mkono wa Yahweh umeenda kinyume na mimi.”
14 Kisha wakalia tena kwa sauti. Orpa akambusu mama mkwe wake, akaenda zake, lakini Ruthu akaambatana naye.
Ndipo wake wa watoto wake wakapaza sauti zao na kulia tena. Oripa alimuaga kwa kumbusu, lakini Ruth aliendelea kubaki naye.
15 Naomi akamwambia, “Tazama, mwenzako anarejea kwa watu wake na kwa miungu yake. Rudi pamoja naye.”
Naomi alisema, “sikiliza, mwenzako amerudi kwa watu wake na miungu yake. Ruri pamoja naye.”
16 Lakini Ruthu akajibu, “Usinisihi nikuache au niache kukufuata. Utakakokwenda nami nitakwenda, na wewe utakapoishi nitaishi. Watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu.
lakini Ruth alisema, “Usiniache niondoke mbali nawe, kwa kuwa uendako, nitakwenda, utakapoishi, nitaishi; watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu.
17 Pale utakapofia nami nitafia hapo, na papo hapo nitazikwa. Bwana na aniadhibu vikali, kama kitu kingine chochote kitanitenga nawe isipokuwa kifo.”
Mahali utakapofia, nitafia hapo, na hapo nitazikwa. Yahweh aniwezeshe, na hata zaidi, ikiwa kuna chochote isipokuwa kifo kamwe hakiwezi kututenganisha.
18 Naomi alipotambua kwamba Ruthu amenuia kufuatana naye, hakuendelea kumsihi tena.
Naomi alipoona kuwa Ruth alikuwa ameamua kwenda naye, aliacha kubishana naye.
19 Kwa hiyo hao wanawake wawili wakaondoka, wakafika Bethlehemu. Walipofika Bethlehemu, mji mzima ulitaharuki, wanawake wakashangaa, wakasema, “Huyu aweza kuwa ni Naomi?”
Hivyo wote wawili walisafiri mpaka walipofika mjini Bethelehemu. Kwa hiyo walipofika Bethlehemu, mji wote uliwafurahia, wanawake walisema, “Huyu ni Naomi?”
20 Akawaambia, “Msiniite tena Naomi, niiteni Mara, kwa sababu Mwenyezi amenitendea mambo machungu sana.
Lakini aliwaambia, “Msiniite Naomi. Niiteni Mchungu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana.
21 Mimi niliondoka hali nimejaa, lakini Bwana amenirudisha mtupu. Kwa nini kuniita Naomi? Bwana amenitendea mambo machungu; Mwenyezi ameniletea msiba.”
Nilikwenda nikiwa nimejaa, lakini Yahweh kanirudisha nyumbani nikiwa sina wote. Hivyo kwa nini mnaniita Naomi, wakati mnaona Yahweh amenihukumu, kuwa Mwenyezi Mungu amenitaabisha?”
22 Kwa hiyo Naomi alirudi pamoja na Ruthu Mmoabu mkwe wake, nao wakafika Bethlehemu mwanzoni mwa kuvuna shayiri.
Kwa hivyo Naomi na Ruth Mmoabu, mke wa mtoto wake, walirudi kutoka nchi ya Moabu. walirudi Bethrehemu mwazo wa mavuno ya shairi.

< Ruth 1 >