< Warumi 11 >
1 Basi nauliza: Je, Mungu amewakataa watu wake? La, hasha! Mimi mwenyewe ni Mwisraeli, tena uzao wa Abrahamu kutoka kabila la Benyamini.
我且说, 神弃绝了他的百姓吗?断乎没有!因为我也是以色列人,亚伯拉罕的后裔,属便雅悯支派的。
2 Mungu hajawakataa watu wake, ambao yeye aliwajua tangu mwanzo. Je, hamjui yale Maandiko yasemayo kuhusu Eliya, jinsi alivyomlalamikia Mungu kuhusu Israeli?
神并没有弃绝他预先所知道的百姓。你们岂不晓得经上论到以利亚是怎么说的呢?他在 神面前怎样控告以色列人说:
3 Alisema, “Bwana, wamewaua manabii wako na kuzibomoa madhabahu zako, nimebaki mimi peke yangu, nao wanataka kuniua?”
“主啊,他们杀了你的先知,拆了你的祭坛,只剩下我一个人;他们还要寻索我的命。”
4 Je, Mungu alimjibuje? “Nimejibakizia watu elfu saba ambao hawajapiga magoti kumwabudu Baali.”
神的回话是怎么说的呢?他说:“我为自己留下七千人,是未曾向巴力屈膝的。”
5 Vivyo hivyo pia, sasa wapo mabaki waliochaguliwa kwa neema ya Mungu.
如今也是这样,照着拣选的恩典,还有所留的余数。
6 Lakini ikiwa wamechaguliwa kwa neema, si tena kwa msingi wa matendo. Kama ingekuwa kwa matendo, neema isingekuwa neema tena.
既是出于恩典,就不在乎行为;不然,恩典就不是恩典了。
7 Tuseme nini basi? Kile kitu ambacho Israeli alikitafuta kwa bidii hakukipata. Lakini waliochaguliwa walikipata. Waliobaki walifanywa wagumu,
这是怎么样呢?以色列人所求的,他们没有得着。惟有蒙拣选的人得着了;其余的就成了顽梗不化的。
8 kama ilivyoandikwa: “Mungu aliwapa bumbuazi la mioyo, macho ili wasiweze kuona, na masikio ili wasiweze kusikia, hadi leo.”
如经上所记: 神给他们昏迷的心, 眼睛不能看见, 耳朵不能听见, 直到今日。
9 Naye Daudi anasema: “Karamu zao na ziwe tanzi na mtego wa kuwanasa, kitu cha kuwakwaza waanguke, na adhabu kwao.
大卫也说: 愿他们的筵席变为网罗,变为机槛, 变为绊脚石,作他们的报应。
10 Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona, nayo migongo yao iinamishwe daima.”
愿他们的眼睛昏蒙,不得看见; 愿你时常弯下他们的腰。
11 Hivyo nauliza tena: Je, Waisraeli walijikwaa ili waanguke na kuangamia kabisa? La, hasha! Lakini kwa sababu ya makosa yao, wokovu umewafikia watu wa Mataifa, ili kuwafanya Waisraeli waone wivu.
我且说,他们失脚是要他们跌倒吗?断乎不是!反倒因他们的过失,救恩便临到外邦人,要激动他们发愤。
12 Basi ikiwa kukosa kwao kumekuwa utajiri mkubwa kwa ulimwengu, tena kama kuangamia kwao kumeleta utajiri kwa watu wa Mataifa, kurudishwa kwao kutaleta utajiri mkuu zaidi.
若他们的过失为天下的富足,他们的缺乏为外邦人的富足,何况他们的丰满呢?
13 Sasa ninasema nanyi watu wa Mataifa. Maadamu mimi ni mtume kwa watu wa Mataifa, naitukuza huduma yangu
我对你们外邦人说这话;因我是外邦人的使徒,所以敬重我的职分,
14 ili kuwafanya watu wangu waone wivu na hivyo kuwaokoa baadhi yao.
或者可以激动我骨肉之亲发愤,好救他们一些人。
15 Kwa kuwa ikiwa kukataliwa kwao ni kupatanishwa kwa ulimwengu, kukubaliwa kwao si kutakuwa ni uhai baada ya kufa?
若他们被丢弃,天下就得与 神和好,他们被收纳,岂不是死而复生吗?
16 Kama sehemu ya donge la unga uliotolewa kuwa limbuko ni mtakatifu, basi unga wote ni mtakatifu, nalo shina kama ni takatifu, vivyo hivyo na matawi nayo.
所献的新面若是圣洁,全团也就圣洁了;树根若是圣洁,树枝也就圣洁了。
17 Lakini kama baadhi ya matawi yalikatwa, nawe chipukizi la mzeituni mwitu ukapandikizwa mahali pao ili kushiriki unono pamoja na matawi mengine kutoka shina la mzeituni,
若有几根枝子被折下来,你这野橄榄得接在其中,一同得着橄榄根的肥汁,
18 basi usijivune juu ya hayo matawi. Kama ukijivuna, kumbuka jambo hili: si wewe unayelishikilia shina, bali ni shina linalokushikilia wewe.
你就不可向旧枝子夸口;若是夸口,当知道不是你托着根,乃是根托着你。
19 Basi utasema, “Matawi yale yalikatwa ili nipate kupandikizwa katika hilo shina.”
你若说,那枝子被折下来是特为叫我接上。
20 Hii ni kweli. Matawi hayo yalikatwa kwa sababu ya kutokuamini kwake, lakini wewe umesimama tu kwa sababu ya imani. Kwa hiyo usijivune, bali simama kwa kuogopa.
不错!他们因为不信,所以被折下来;你因为信,所以立得住;你不可自高,反要惧怕。
21 Kwa maana kama Mungu hakuyahurumia matawi ya asili, wala hatakuhurumia wewe.
神既不爱惜原来的枝子,也必不爱惜你。
22 Angalia basi wema na ukali wa Mungu: Kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu, kama utadumu katika wema wake. La sivyo, nawe utakatiliwa mbali.
可见, 神的恩慈和严厉向那跌倒的人是严厉的,向你是有恩慈的,只要你长久在他的恩慈里;不然,你也要被砍下来。
23 Wao nao wasipodumu katika kutokuamini kwao, watapandikizwa tena kwenye shina, kwa maana Mungu anao uwezo wa kuwapandikiza tena kwenye hilo shina.
而且他们若不是长久不信,仍要被接上,因为 神能够把他们从新接上。
24 Ikiwa wewe ulikatwa kutoka kile ambacho kwa asili ni mzeituni mwitu na kupandikizwa kinyume cha asili kwenye mzeituni uliopandwa, si rahisi zaidi matawi haya ya asili kupandikizwa tena kwenye shina lake la mzeituni!
你是从那天生的野橄榄上砍下来的,尚且逆着性得接在好橄榄上,何况这本树的枝子,要接在本树上呢!
25 Ndugu zangu, ili msije mkajidai kuwa wenye hekima kuliko mlivyo, nataka mfahamu siri hii: Ugumu umewapata Israeli kwa sehemu hadi idadi ya watu wa Mataifa watakaoingia itimie.
弟兄们,我不愿意你们不知道这奥秘(恐怕你们自以为聪明),就是以色列人有几分是硬心的,等到外邦人的数目添满了,
26 Hivyo Israeli wote wataokolewa. Kama ilivyoandikwa: “Mkombozi atakuja kutoka Sayuni; ataondoa kutokumcha Mungu katika Yakobo.
于是以色列全家都要得救。如经上所记: 必有一位救主从锡安出来, 要消除雅各家的一切罪恶;
27 Hili ndilo agano langu nao nitakapoziondoa dhambi zao.”
又说:我除去他们罪的时候, 这就是我与他们所立的约。
28 Kwa habari ya Injili, wao ni adui wa Mungu kwa ajili yenu, lakini kuhusu kule kuteuliwa kwao ni wapendwa, kwa ajili ya mababa zao wa zamani,
就着福音说,他们为你们的缘故是仇敌;就着拣选说,他们为列祖的缘故是蒙爱的。
29 kwa maana akishawapa watu karama, Mungu haziondoi, wala wito wake.
因为 神的恩赐和选召是没有后悔的。
30 Kama vile ninyi wakati fulani mlivyokuwa waasi kwa Mungu lakini sasa mmepata rehema kwa sababu ya kutokutii kwao,
你们从前不顺服 神,如今因他们的不顺服,你们倒蒙了怜恤。
31 hivyo nao Waisraeli wamekuwa waasi ili kwamba wao nao sasa waweze kupata rehema kwa ajili ya rehema za Mungu kwenu.
这样,他们也是不顺服,叫他们因着施给你们的怜恤,现在也就蒙怜恤。
32 Kwa maana Mungu amewafunga wanadamu wote kwenye kuasi ili apate kuwarehemu wote. (eleēsē )
因为 神将众人都圈在不顺服之中,特意要怜恤众人。 (eleēsē )
33 Tazama jinsi kilivyo kina cha utajiri wa hekima na maarifa ya Mungu! Tazama jinsi ambavyo hukumu zake hazichunguziki, na ambavyo njia zake zisivyotafutikana!
深哉, 神丰富的智慧和知识! 他的判断何其难测! 他的踪迹何其难寻!
34 “Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya Bwana? Au ni nani ambaye amekuwa mshauri wake?”
谁知道主的心? 谁作过他的谋士呢?
35 “Au ni nani aliyempa chochote ili arudishiwe?”
谁是先给了他, 使他后来偿还呢?
36 Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwake na kwa ajili yake. Utukufu ni wake milele! Amen. (aiōn )
因为万有都是本于他, 倚靠他,归于他。 愿荣耀归给他,直到永远。阿们! (aiōn )