< Ufunuo 7 >
1 Baada ya hili nikaona malaika wanne wakiwa wamesimama katika pembe nne za dunia, wakizuia hizo pepo nne za dunia, ili kwamba pasiwe na upepo utakaovuma juu ya nchi au juu ya bahari au juu ya mti wowote.
After this I saw four angels standing at the four corners of the earth, holding the four winds of the earth, that no wind should blow on the earth, or on the sea, or upon any tree.
2 Nikaona malaika mwingine akipanda kutoka mawio ya jua akiwa na muhuri wa Mungu aliye hai. Akawaita kwa sauti kubwa wale malaika wanne waliokuwa wamepewa mamlaka ya kuidhuru nchi na bahari, akisema,
And I saw another angel ascend from the sunrising, having the seal of the living God: and he cried with a great voice to the four angels, to whom it was given to hurt the earth and the sea,
3 “Msiidhuru nchi wala bahari, wala miti, hadi tuwe tumetia muhuri kwenye vipaji vya nyuso za watumishi wa Mungu wetu.”
saying, Hurt not the earth, neither the sea, nor the trees, till we shall have sealed the servants of our God on their foreheads.
4 Ndipo nikasikia idadi ya wale waliotiwa muhuri: yaani 144,000 kutoka makabila yote ya Israeli.
And I heard the number of them which were sealed, a hundred and forty and four thousand, sealed out of every tribe of the children of Israel.
5 Kutoka kabila la Yuda 12,000 walitiwa muhuri, kutoka kabila la Reubeni 12,000, kutoka kabila la Gadi 12,000,
Of the tribe of Judah [were] sealed twelve thousand: Of the tribe of Reuben twelve thousand: Of the tribe of Gad twelve thousand:
6 kutoka kabila la Asheri 12,000, kutoka kabila la Naftali 12,000, kutoka kabila la Manase 12,000,
Of the tribe of Asher twelve thousand: Of the tribe of Naphtali twelve thousand: Of the tribe of Manasseh twelve thousand:
7 kutoka kabila la Simeoni 12,000, kutoka kabila la Lawi 12,000, kutoka kabila la Isakari 12,000,
Of the tribe of Simeon twelve thousand: Of the tribe of Levi twelve thousand: Of the tribe of Issachar twelve thousand:
8 kutoka kabila la Zabuloni 12,000, kutoka kabila la Yosefu 12,000, na kutoka kabila la Benyamini 12,000.
Of the tribe of Zebulun twelve thousand: Of the tribe of Joseph twelve thousand: Of the tribe of Benjamin [were] sealed twelve thousand.
9 Baada ya hili nikatazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna yeyote awezaye kuuhesabu, kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao.
After these things I saw, and behold, a great multitude, which no man could number, out of every nation and of [all] tribes and peoples and tongues, standing before the throne and before the Lamb, arrayed in white robes, and palms in their hands;
10 Nao walikuwa wakipiga kelele kwa sauti kubwa wakisema: “Wokovu una Mungu wetu, yeye aketiye kwenye kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo!”
and they cry with a great voice, saying, Salvation unto our God which sitteth on the throne, and unto the Lamb.
11 Malaika wote walikuwa wamesimama kukizunguka kile kiti cha enzi na wale wazee ishirini na wanne na wale viumbe wanne wenye uhai. Wakaanguka kifudifudi mbele ya hicho kiti cha enzi na kumwabudu Mungu,
And all the angels were standing round about the throne, and [about] the elders and the four living creatures; and they fell before the throne on their faces, and worshipped God,
12 wakisema: “Amen! Sifa na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu viwe kwa Mungu wetu milele na milele. Amen!” (aiōn )
saying, Amen: Blessing, and glory, and wisdom, and thanksgiving, and honour, and power, and might, [be] unto our God for ever and ever. Amen. (aiōn )
13 Kisha mmoja wa wale wazee ishirini na wanne akaniuliza, “Ni nani hawa waliovaa mavazi meupe, nao wametoka wapi?”
And one of the elders answered, saying unto me, These which are arrayed in the white robes, who are they, and whence came they?
14 Nikamjibu, “Bwana, wewe wajua.” Naye akasema, “Hawa ni wale waliotoka katika ile dhiki kuu, nao wamefua mavazi yao katika damu ya Mwana-Kondoo na kuyafanya meupe kabisa.
And I say unto him, My lord, thou knowest. And he said to me, These are they which come out of the great tribulation, and they washed their robes, and made them white in the blood of the Lamb.
15 Kwa hiyo, “Wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na kumtumikia usiku na mchana katika hekalu lake; naye aketiye katika kile kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao.
Therefore are they before the throne of God; and they serve him day and night in his temple: and he that sitteth on the throne shall spread his tabernacle over them.
16 Kamwe hawataona njaa wala kiu tena. Jua halitawapiga wala joto lolote liunguzalo.
They shall hunger no more, neither thirst any more; neither shall the sun strike upon them, nor any heat:
17 Kwa maana Mwana-Kondoo aliyeko katikati ya kile kiti cha enzi atakuwa Mchungaji wao; naye atawaongoza kwenda kwenye chemchemi za maji yaliyo hai. Naye Mungu atafuta kila chozi kutoka macho yao.”
for the Lamb which is in the midst of the throne shall be their shepherd, and shall guide them unto fountains of waters of life: and God shall wipe away every tear from their eyes.