< Ufunuo 19 >
1 Baada ya haya nikasikia sauti kama ya umati mkubwa mbinguni wakipiga kelele wakisema: “Haleluya! Wokovu na utukufu na uweza ni vya Mungu wetu,
些事以後,我聽見天上彷彿有一大夥人群發出的大聲音說:「亞肋路亞!勝利、光榮和能力,應歸於我們的天主,
2 kwa maana hukumu zake ni za kweli na za haki. Amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeuharibu ulimwengu kwa uzinzi wake. Mungu amemlipiza kisasi kwa ajili ya damu ya watumishi wake.”
因為,他的判斷是正確而正義的;他懲罰的了那曾以自己的邪淫敗壞了下地的大淫婦,並給被她所殺的僕人報了仇。」
3 Wakasema tena kwa nguvu: “Haleluya! Moshi wake huyo kahaba unapanda juu milele na milele.” (aiōn )
他們又重覆說:「亞肋路亞!她的煙向上直冒,至於無窮之世。」 (aiōn )
4 Wale wazee ishirini na wanne pamoja na wale viumbe wanne wenye uhai wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu, aliyekuwa ameketi kwenye kile kiti cha enzi. Wakasema kwa sauti kuu: “Amen, Haleluya!”
於是,那二十四位長老和那四個活物,便俯伏朝拜那坐在寶座上的天主說:「阿們。亞肋路亞!」
5 Kisha sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi, ikisema: “Msifuni Mungu wetu, ninyi watumishi wake wote, ninyi nyote mnaomcha, wadogo kwa wakubwa!”
遂有聲音由寶座那裏發出說:「天主的眾僕人,凡敬畏他的,無論大小,請讚美我們的天主罷!」
6 Kisha nikasikia sauti kama ya umati mkubwa, kama sauti ya maji mengi yaendayo kasi na kama ngurumo kubwa ya radi wakipiga kelele wakisema: “Haleluya! Kwa maana Bwana Mungu wetu Mwenyezi anatawala.
我聽見彷彿有一大夥人群的聲音,就如大水的響聲,又如巨雷的響聲,說:「亞肋路亞!因為我們全能的天主,上主為王了!
7 Tufurahi, tushangilie na kumpa utukufu! Kwa maana arusi ya Mwana-Kondoo imewadia na bibi arusi wake amejiweka tayari.
讓我們歡樂鼓舞,將光榮歸於他罷!因為羔羊的婚期來近了,他的新娘也準備好了;
8 Akapewa kitani safi, nyeupe inayongʼaa, ili avae.” (Hiyo kitani safi inawakilisha matendo ya haki ya watakatifu.)
天主又賞賜她穿上了華麗而潔白的細麻衣:這細麻衣就是聖徒們的義行。」
9 Ndipo malaika akaniambia, “Andika: ‘Wamebarikiwa wale walioalikwa kwenye karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo!’” Naye akaongeza kusema, “Haya ndiyo maneno ya kweli ya Mungu.”
有位天使給我說:「你寫下:被召赴羔羊婚宴的人,是有福的!」他又給我說:「這都是天主真實的話。」
10 Ndipo nikaanguka kifudifudi miguuni pake ili kumwabudu, lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi pia ni mtumishi mwenzako pamoja na ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Mwabudu Mungu! Maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.”
我就俯伏在他腳前要朝拜他;他給我說:「萬不要這樣作,我只是你和你那些為耶穌作見證的弟兄們的同僕,你只該朝拜天主!」因為預言之神就是為耶穌作證。
11 Kisha nikaona mbingu imefunguka na hapo mbele yangu akiwepo farasi mweupe, ambaye yeye aliyempanda aliitwa Mwaminifu na Kweli. Yeye huhukumu kwa haki na kufanya vita.
隨後我看見天開了,見有一匹白馬;騎馬的那位,稱為「忠信和真實者,」他憑正義去審判,去作戰。
12 Macho yake ni kama miali ya moto na juu ya kichwa chake kuna taji nyingi. Ana jina lililoandikwa ambalo hakuna mtu yeyote anayelijua isipokuwa yeye mwenyewe.
他的眼睛有如火焰,他頭上戴著許多冠冕,還有寫的一個名號,除他自己外,誰也不認識;
13 Amevaa joho lililochoviwa katika damu, na Jina lake ni “Neno la Mungu.”
他身披一件染過血的衣服,他的名字叫作:「天主的聖言。」
14 Majeshi ya mbinguni walikuwa wakimfuata, wakiwa wamepanda farasi weupe, hali wamevaa mavazi ya kitani safi, nyeupe na nzuri.
天上的軍隊也乘著白馬,穿著潔白的細麻衣跟隨著他。
15 Kinywani mwake hutoka upanga mkali ambao kwa huo atayaangusha mataifa. “Atayatawala kwa fimbo yake ya utawala ya chuma.” Hulikanyaga shinikizo la mvinyo wa ghadhabu ya Mungu Mwenyezi.
從他口中射出一把利劍,用來打敗異民;他要用鐵杖統治他們,並踐踏那充滿全能天主忿怒的榨酒池。
16 Kwenye joho lake na paja lake pameandikwa jina hili: Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana.
在衣服上,即在蓋他大腿的衣服上寫著「萬王之王,萬主之主」的名號。
17 Nami nikamwona malaika amesimama ndani kwenye jua, akaita ndege wote warukao angani kwa sauti kuu, “Njooni, kusanyikeni kwa ajili ya karamu kubwa ya Mungu,
我又看見一位天使,站在太陽上,大聲向一切飛翔於天空的飛鳥喊說:「請你們來一齊赴天主的大宴席,
18 ili mpate kula nyama ya wafalme na ya majemadari, ya mashujaa, ya farasi na ya wapanda farasi, nyama ya wanadamu, wote walio huru na watumwa, wadogo na wakubwa.”
前來吃列王的肉、諸將帥的肉、眾勇士的肉、駿馬和騎馬者的肉,並一切自主的或為奴的,以及大小人民的肉。」
19 Kisha nikamwona yule mnyama na wafalme wa dunia pamoja na majeshi yao wakiwa wamekusanyika pamoja ili kufanya vita dhidi ya yule aliyempanda farasi pamoja na jeshi lake.
我也看見那獸、地上的君王和他們的軍隊都聚在一起,要與騎馬的那位和他的軍隊作戰。
20 Lakini yule mnyama akakamatwa pamoja na huyo nabii wa uongo ambaye alikuwa amefanya ishara kwa niaba ya huyo mnyama, ambaye kwa ishara hizi aliwadanganya wale waliopokea chapa ya huyo mnyama na kuiabudu sanamu yake. Hawa wawili wakatupwa wakiwa hai ndani ya ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti. (Limnē Pyr )
可是,那獸被捉住了,在牠面前行過奇蹟,並藉著這些奇蹟,欺騙了那些接受那獸的印號,和朝拜獸像的那位假先知,也和牠一起被捉住了;牠們兩個活活的被扔到那用硫磺燃燒的火坑裏去了。 (Limnē Pyr )
21 Wale waliosalia waliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwa yule aliyekuwa amempanda farasi nao ndege wote wakajishibisha kwa nyama yao.
其餘的人也被騎馬者口中所射出的劍殺死了;所有的飛鳥都吃飽了他們的肉。