< Zaburi 98 >

1 Zaburi. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu; kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu umemfanyia wokovu.
Oh, mwimbieni Yahwe wimbo mpya, kwa kuwa ametenda mambo ya ajabu; mkono wake wa kuume na mkono wake mtakatifu vimempa ushindi.
2 Bwana ameufanya wokovu wake ujulikane na amedhihirisha haki yake kwa mataifa.
Yahwe ameufanya wokovu wake ujulikane; ameidhihirisha haki yake kwa mataifa yote.
3 Ameukumbuka upendo wake na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli; miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.
Hukumbuka uaminifu wa agano lake na uaminifu kwa ajili ya nyumba ya Israeli; miisho yote ya dunia itauona ushindi wa Mungu wetu.
4 Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote, ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;
Mshangilieni Yahwe, nchi yote; pazeni sauti kwa wimbo, imbeni kwa furaha, na imbeni sifa.
5 mwimbieni Bwana kwa kinubi, kwa kinubi na sauti za kuimba,
Mwimbieni Yahwe sifa kwa kinubi, kwa kinubi na wimbo wenye muiki wa kupendeza.
6 kwa tarumbeta na mvumo wa baragumu za pembe za kondoo dume: shangilieni kwa furaha mbele za Bwana, aliye Mfalme.
Kwa panda na sauti ya baragumu, fanyeni kelele za shangwe mbele ya Mfalme, Yahwe.
7 Bahari na ivume na kila kiliomo ndani yake, dunia na wote wakaao ndani yake.
Bahari na ipige kelele na vyote vilivyomo, ulimwengu na wale wakaao ndani yake!
8 Mito na ipige makofi, milima na iimbe pamoja kwa furaha,
Mito na ipige makofi, na milima ipige kelele kwa furaha.
9 vyote na viimbe mbele za Bwana, kwa maana yuaja kuhukumu dunia. Atahukumu dunia kwa haki na mataifa kwa haki.
Yahwe anakuja kuihukumu nchi; naye ataihukumu dunia kwa haki na mataifa kwa adili.

< Zaburi 98 >