< Zaburi 92 >
1 Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato. Ni vyema kumshukuru Bwana na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,
Ni jambo jema kumshukuru Yahwe na kuliimbia sifa jina lako, Uliye Juu,
2 kuutangaza upendo wako asubuhi, na uaminifu wako wakati wa usiku,
kutangaza uaminifu wa agano lako wakati wa asubuhi na uaminifu wako kila usiku,
3 kwa zeze yenye nyuzi kumi na kwa sauti ya kinubi.
kwa kinubi cha nyuzi kumi na kwa tuni ya kinubi.
4 Ee Bwana, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha, nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako.
Kwa kuwa wewe, Yahwe, matendo yako yamenifurahisha. Nitaimba kwa furaha kwa sababu ya matendo ya mikono yako.
5 Ee Bwana, tazama jinsi yalivyo makuu matendo yako, tazama jinsi yalivyo ya kina mawazo yako!
Ni jinsi gani matendo yako ni makuu, Yahwe! mawazo yako ni ya kina.
6 Mjinga hafahamu, mpumbavu haelewi,
Mtu mpumbavu hawezi kuyajua, wala mjinga kuyaelewa haya:
7 ingawa waovu huchipua kama majani na wote watendao mabaya wanastawi, wataangamizwa milele.
Wasio haki watakapochipuka kama nyasi, na hata watendao uovu watakapo stawi, bado wataangamizwa kwenye uharibifu wa milele.
8 Bali wewe, Ee Bwana, utatukuzwa milele.
Lakini wewe, Yahwe, utatawala milele.
9 Ee Bwana, hakika adui zako, hakika adui zako wataangamia. Wote watendao mabaya watatawanyika.
Hakika, watazame adui zako, Yahwe! Hakika, watazame adui zako. Wataangamia! Wale wote watendao maovu watatawanywa.
10 Umeitukuza pembe yangu kama ile ya nyati dume, mafuta mazuri yamemiminwa juu yangu.
Wewe umeyainua mapembe yangu kama mapembe ya Nyati wa porini; nimepakwa mafuta safi.
11 Macho yangu yamewaona adui zangu wakishindwa, masikio yangu yamesikia maangamizi ya adui zangu waovu.
Macho yangu yameona kuanguka kwa adui zangu; masikio yangu yamesikia maangamizi ya maadui zangu waovu.
12 Wenye haki watastawi kama mtende, watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni,
Wenye haki watastawi kama mtende; watakua kama mwerezi wa Lebanoni.
13 waliopandwa katika nyumba ya Bwana, watastawi katika nyua za Mungu wetu.
Wamepandwa katika nyumba ya Yahwe; wakistawi katika nyua za Mungu wetu.
14 Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda, watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu,
Wao huzaa matunda hata uzeeni; hukaa safi na wenye afya,
15 wakitangaza, “Bwana ni mkamilifu; yeye ni Mwamba wangu, na ndani yake hamna uovu.”
kutangaza kuwa Yahwe ni wa haki. Yeye ni mwamba wangu, na hakuna udhalimu ndani yake.