< Zaburi 92 >

1 Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato. Ni vyema kumshukuru Bwana na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,
מזמור שיר ליום השבת טוב להדות ליהוה ולזמר לשמך עליון׃
2 kuutangaza upendo wako asubuhi, na uaminifu wako wakati wa usiku,
להגיד בבקר חסדך ואמונתך בלילות׃
3 kwa zeze yenye nyuzi kumi na kwa sauti ya kinubi.
עלי עשור ועלי נבל עלי הגיון בכנור׃
4 Ee Bwana, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha, nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako.
כי שמחתני יהוה בפעלך במעשי ידיך ארנן׃
5 Ee Bwana, tazama jinsi yalivyo makuu matendo yako, tazama jinsi yalivyo ya kina mawazo yako!
מה גדלו מעשיך יהוה מאד עמקו מחשבתיך׃
6 Mjinga hafahamu, mpumbavu haelewi,
איש בער לא ידע וכסיל לא יבין את זאת׃
7 ingawa waovu huchipua kama majani na wote watendao mabaya wanastawi, wataangamizwa milele.
בפרח רשעים כמו עשב ויציצו כל פעלי און להשמדם עדי עד׃
8 Bali wewe, Ee Bwana, utatukuzwa milele.
ואתה מרום לעלם יהוה׃
9 Ee Bwana, hakika adui zako, hakika adui zako wataangamia. Wote watendao mabaya watatawanyika.
כי הנה איביך יהוה כי הנה איביך יאבדו יתפרדו כל פעלי און׃
10 Umeitukuza pembe yangu kama ile ya nyati dume, mafuta mazuri yamemiminwa juu yangu.
ותרם כראים קרני בלתי בשמן רענן׃
11 Macho yangu yamewaona adui zangu wakishindwa, masikio yangu yamesikia maangamizi ya adui zangu waovu.
ותבט עיני בשורי בקמים עלי מרעים תשמענה אזני׃
12 Wenye haki watastawi kama mtende, watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni,
צדיק כתמר יפרח כארז בלבנון ישגה׃
13 waliopandwa katika nyumba ya Bwana, watastawi katika nyua za Mungu wetu.
שתולים בבית יהוה בחצרות אלהינו יפריחו׃
14 Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda, watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu,
עוד ינובון בשיבה דשנים ורעננים יהיו׃
15 wakitangaza, “Bwana ni mkamilifu; yeye ni Mwamba wangu, na ndani yake hamna uovu.”
להגיד כי ישר יהוה צורי ולא עלתה בו׃

< Zaburi 92 >