< Zaburi 89 >

1 Utenzi wa Ethani Mwezrahi. Nitaimba juu ya upendo mkuu wa Bwana milele; kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako ujulikane kwa vizazi vyote.
Nitimba sifa za matendo ya uaminifu wa agano milele. Nitatangaza kweli yako kwa vizazi vijavyo.
2 Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni.
Maana nimesema, “Uaminifu wa agano umeimarishwa milele; na kweli yako umeiimarisha mbinguni.”
3 Ulisema, “Nimefanya agano na mteule wangu, nimemwapia mtumishi wangu Daudi,
“Nimefanya agano na wateule wangu, nimeapa kiapo kwa Daudi mtumishi wangu.
4 ‘Nitaimarisha uzao wako milele na kudumisha ufalme wako kwa vizazi vyote.’”
Nitauimarisha uzao wako milele, na nitauimarisha utawala wako vizazi vyote.” (Selah)
5 Ee Bwana, mbingu zinayasifu maajabu yako, uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu.
Mbingu husifu maajabu yako, Yahwe; kweli yako inasifiwa katika kusanyiko la watakatifu.
6 Kwa kuwa ni nani katika mbingu anayeweza kulinganishwa na Bwana? Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni aliye kama Bwana?
Maana ni nani katika mbingu aweza kulinganishwa na Yahwe? Ambaye kati ya wana wa miungu ni kama Yahwe?
7 Katika kusanyiko la watakatifu, Mungu huogopwa sana, anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka.
Ni Mungu anaye heshimiwa sana katika baraza la watakatifu naye ni wakutisha kati ya wote wanao mzunguka.
8 Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, ni nani aliye kama wewe? Ee Bwana, wewe ni mwenye nguvu, na uaminifu wako unakuzunguka.
Yahwe, Mungu wa majeshi, ni nani aliye na nguvu kama wewe, Yahwe? Kweli yako inakuzunguka.
9 Wewe unatawala bahari yenye msukosuko; wakati mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza.
Wewe huitawala bahari yenye nguvu; mawimbi yainukapo, wewe huyatuliza.
10 Wewe ulimponda Rahabu kama mmojawapo wa waliochinjwa; kwa mkono wako wenye nguvu, uliwatawanya adui zako.
Ulimwangamiza Rahabu kama mmoja aliye uliwa. Uliwatawanya adui zako kwa mkono wako wenye nguvu.
11 Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako, uliuwekea ulimwengu msingi pamoja na vyote vilivyomo.
Mbingu ni zako wewe, na nchi pia. Uliiumba dunia na vyote vilivyomo.
12 Uliumba kaskazini na kusini; Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha.
Uliumba kaskazini na kusini. Tabori na Hermoni hulifurahia jina lako.
13 Mkono wako umejaa uwezo; mkono wako una nguvu, mkono wako wa kuume umetukuzwa.
una mkono wa uweza na mkono wenye nguvu, na mkono wako wa kuume uko juu.
14 Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi; upendo na uaminifu vinakutangulia.
Haki na hukumu ni msingi wa kiti chako. Uaminifu wa agano lako na uaminifu huja mbele zako.
15 Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe, wanaotembea katika mwanga wa uwepo wako, Ee Bwana.
Wamebarikiwa watu wakuabuduo wewe! Yahwe, wanatembea katika nuru ya uso wako.
16 Wanashangilia katika jina lako mchana kutwa, wanafurahi katika haki yako.
Siku zote wanafurahia katika jina lako, na katika haki yako wanakutukuza wewe.
17 Kwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao, kwa wema wako unatukuza pembe yetu.
Wewe ni fahari ya nguvu zao, na kwa nguvu zako tu washindi.
18 Naam, ngao yetu ni mali ya Bwana, na mfalme wetu mali ya Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Maana ngao zetu ni za kwako Yahwe; mfalme wetu ni wa Mtakatifu wa Israeli.
19 Ulizungumza wakati fulani katika maono, kwa watu wako waaminifu, ukasema: “Nimeweka nguvu kwa shujaa, nimemwinua kijana miongoni mwa watu.
Muda mrefu uliopita ulizungumza na waaminfu wako katika maono; ulisema, “Nimeweka taji juu ya mwenye nguvu; nimemuinua aliyechaguliwa kutoka kati ya watu.
20 Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, na nimemtia mafuta yangu matakatifu.
Nimemchagua Daudi mtumishi wangu; kwa mafuta yangu matakatifu nimempaka yeye.
21 Kitanga changu kitamtegemeza, hakika mkono wangu utamtia nguvu.
Mkono wangu utamsaidia yeye; mkono wangu utamtia nguvu.
22 Hakuna adui atakayemtoza ushuru, hakuna mtu mwovu atakayemwonea.
Hakuna adui atakaye mdanganya; hakuna mwana wa uovu atakaye muonea.
23 Nitawaponda adui zake mbele zake na kuwaangamiza watesi wake.
Nitawaangamiza adui zake mbele yake; nitawaua wale wamchukiao.
24 Upendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye, kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa.
Kweli yangu na uaminifu wa agano vitakuwa pamoja naye; kupitia jina langu atakuwa mshindi.
25 Nitauweka mkono wake juu ya bahari, mkono wake wa kuume juu ya mito.
Nitaweka mkono wake juu ya bahari na mkono wake wa kuume juu ya mito.
26 Naye ataniita kwa sauti, ‘Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, Mwamba na Mwokozi wangu.’
Yeye ataniita, 'Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, na mwamba wa wokovu wangu.'
27 Nitamteua pia awe mzaliwa wangu wa kwanza, aliyetukuka kuliko wafalme wote wa dunia.
Nitamjalia kuwa kama mzaliwa wangu wa kwanza, aliye inuliwa zaidi juu ya wafalme wa nchi.
28 Nitadumisha upendo wangu kwake milele, na agano langu naye litakuwa imara.
Nitaongeza uaminifu wa agano langu kwake milele; na agano langu pamoja naye litakuwa salama.
29 Nitaudumisha uzao wake milele, kiti chake cha enzi kama mbingu zinavyodumu.
Nitaufanya uzao wake kudumu milele na kiti chake cha enzi kitadumu kama mbingu zilizo juu.
30 “Kama wanae wataacha amri yangu na wasifuate sheria zangu,
Ikiwa watoto wake wataziacha sheria zangu na kutokutii amri zangu,
31 kama wakihalifu maagizo yangu na kutoshika amri zangu,
na kama watazivunja sheria zangu na kutokuzishika amri zangu,
32 nitaadhibu dhambi yao kwa fimbo, uovu wao kwa kuwapiga,
ndipo nitauadhiu uasi wao kwa fimbo na uovu wao kwa makofi.
33 lakini sitauondoa upendo wangu kwake, wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe.
Lakini sitauondoa kwake upendo wangu thabiti wala kutokuwa mwaminifu kwa ahadi yangu.
34 Mimi sitavunja agano langu wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka.
Sitavunja agano langu wala kubadilisha maneno ya midomoni mwangu.
35 Mara moja na kwa milele, nimeapa kwa utakatifu wangu, nami sitamdanganya Daudi:
Mara moja na kwa yote, nimeapa kwa utakatifu wangu sitamdanganya Daudi:
36 kwamba uzao wake utaendelea milele, na kiti chake cha enzi kitadumu mbele zangu kama jua;
uzao wake utaendelea milele na kiti chake cha enzi kama vile jua mbele yangu.
37 kitaimarishwa milele kama mwezi, shahidi mwaminifu angani.”
Kitaimarishwa milele kama mwezi, shahidi mwaminifu mawinguni.” (Selah)
38 Lakini wewe umemkataa, umemdharau, umemkasirikia sana mpakwa mafuta wako.
Lakini wewe umemtupa na kumkataa; umemkasirikia mfalme mpakwa mafuta wako.
39 Umelikana agano lako na mtumishi wako, na umeinajisi taji yake mavumbini.
Wewe umelikataa agano la mtumishi wako. Umeinajisi taji yake ardhini.
40 Umebomoa kuta zake zote, na ngome zake zote umezifanya kuwa magofu.
Umevunja kuta zake zote. Umeharibu ngome yake.
41 Wote wapitao karibu wamemnyangʼanya mali zake; amekuwa dharau kwa jirani zake.
Wapita njia wote wamemuibia, amekuwa kitu chenye kinyaa kwa majirani zake.
42 Umeutukuza mkono wa kuume wa adui zake, umewafanya watesi wake wote washangilie.
Umeinua mkono wa kuume wa adui zake; umewafurahisha adui zake wote.
43 Umegeuza makali ya upanga wake, na hukumpa msaada katika vita.
Umeyageuza makali ya upanga wake. Na hukumfanya asimame awapo vitani.
44 Umeikomesha fahari yake, na kukiangusha kiti chake cha enzi.
Umeimaliza fahari yake; umekitupa ardhini kiti chake cha enzi.
45 Umezifupisha siku za ujana wake, umemfunika kwa vazi la aibu.
Umefupisha siku za ujana wake. Umemfunika kwa aibu. (Selah)
46 Hata lini, Ee Bwana? Utajificha milele? Ghadhabu yako itawaka kama moto hata lini?
Mpaka lini, Yahwe? utajificha, milele? Mpaka lini hasira yako itawaka kama moto?
47 Kumbuka jinsi maisha yangu yanavyopita haraka. Ni kwa ubatili kiasi gani umemuumba mwanadamu!
Oh, fikiria jinsi muda wangu ulivyo mfupi, na ni kwa ajili gani umewaumba wana wote wa wanadamu wasio na manufaa!
48 Ni mtu gani awezaye kuishi na asione kifo, au kujiokoa mwenyewe kutoka nguvu za kaburi? (Sheol h7585)
Ni nani aweza kuishi na asife, au atakaye iokoa nafsi yake dhidi ya mkono wa kuzimu? (Selah) (Sheol h7585)
49 Ee Bwana, uko wapi upendo wako mkuu wa mwanzoni, ambao katika uaminifu wako ulimwapia Daudi?
Bwana, yako wapi matendo yako ya zamani ya uaminifu wa agano ambayo ulimwapia Daudi katika kweli yako?
50 Bwana kumbuka jinsi mtumishi wako amesimangwa, jinsi ninavyovumilia moyoni mwangu dhihaka za mataifa yote,
Kumbuka, Bwana, watumishi wako walivyodhihakiwa na vile nilivyo vumilia moyoni mwangu matusi mengi dhidi ya mataifa.
51 dhihaka ambazo kwazo adui zako wamenisimanga, Ee Bwana, ambazo kwazo wamesimanga kila hatua ya mpakwa mafuta wako.
Maadui zako wanavurumiza matusi, Yahwe; wanadhihaki nyayo za mpakwa mafuta wako.
52 Msifuni Bwana milele!
Atukuzwe Yahwe milele. Amina na Amina. Kitabu cha Nne

< Zaburi 89 >