< Zaburi 89 >

1 Utenzi wa Ethani Mwezrahi. Nitaimba juu ya upendo mkuu wa Bwana milele; kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako ujulikane kwa vizazi vyote.
משכיל לאיתן האזרחי חסדי יהוה עולם אשירה לדר ודר אודיע אמונתך בפי׃
2 Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni.
כי אמרתי עולם חסד יבנה שמים תכן אמונתך בהם׃
3 Ulisema, “Nimefanya agano na mteule wangu, nimemwapia mtumishi wangu Daudi,
כרתי ברית לבחירי נשבעתי לדוד עבדי׃
4 ‘Nitaimarisha uzao wako milele na kudumisha ufalme wako kwa vizazi vyote.’”
עד עולם אכין זרעך ובניתי לדר ודור כסאך סלה׃
5 Ee Bwana, mbingu zinayasifu maajabu yako, uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu.
ויודו שמים פלאך יהוה אף אמונתך בקהל קדשים׃
6 Kwa kuwa ni nani katika mbingu anayeweza kulinganishwa na Bwana? Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni aliye kama Bwana?
כי מי בשחק יערך ליהוה ידמה ליהוה בבני אלים׃
7 Katika kusanyiko la watakatifu, Mungu huogopwa sana, anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka.
אל נערץ בסוד קדשים רבה ונורא על כל סביביו׃
8 Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, ni nani aliye kama wewe? Ee Bwana, wewe ni mwenye nguvu, na uaminifu wako unakuzunguka.
יהוה אלהי צבאות מי כמוך חסין יה ואמונתך סביבותיך׃
9 Wewe unatawala bahari yenye msukosuko; wakati mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza.
אתה מושל בגאות הים בשוא גליו אתה תשבחם׃
10 Wewe ulimponda Rahabu kama mmojawapo wa waliochinjwa; kwa mkono wako wenye nguvu, uliwatawanya adui zako.
אתה דכאת כחלל רהב בזרוע עזך פזרת אויביך׃
11 Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako, uliuwekea ulimwengu msingi pamoja na vyote vilivyomo.
לך שמים אף לך ארץ תבל ומלאה אתה יסדתם׃
12 Uliumba kaskazini na kusini; Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha.
צפון וימין אתה בראתם תבור וחרמון בשמך ירננו׃
13 Mkono wako umejaa uwezo; mkono wako una nguvu, mkono wako wa kuume umetukuzwa.
לך זרוע עם גבורה תעז ידך תרום ימינך׃
14 Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi; upendo na uaminifu vinakutangulia.
צדק ומשפט מכון כסאך חסד ואמת יקדמו פניך׃
15 Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe, wanaotembea katika mwanga wa uwepo wako, Ee Bwana.
אשרי העם יודעי תרועה יהוה באור פניך יהלכון׃
16 Wanashangilia katika jina lako mchana kutwa, wanafurahi katika haki yako.
בשמך יגילון כל היום ובצדקתך ירומו׃
17 Kwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao, kwa wema wako unatukuza pembe yetu.
כי תפארת עזמו אתה וברצנך תרים קרננו׃
18 Naam, ngao yetu ni mali ya Bwana, na mfalme wetu mali ya Aliye Mtakatifu wa Israeli.
כי ליהוה מגננו ולקדוש ישראל מלכנו׃
19 Ulizungumza wakati fulani katika maono, kwa watu wako waaminifu, ukasema: “Nimeweka nguvu kwa shujaa, nimemwinua kijana miongoni mwa watu.
אז דברת בחזון לחסידיך ותאמר שויתי עזר על גבור הרימותי בחור מעם׃
20 Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, na nimemtia mafuta yangu matakatifu.
מצאתי דוד עבדי בשמן קדשי משחתיו׃
21 Kitanga changu kitamtegemeza, hakika mkono wangu utamtia nguvu.
אשר ידי תכון עמו אף זרועי תאמצנו׃
22 Hakuna adui atakayemtoza ushuru, hakuna mtu mwovu atakayemwonea.
לא ישא אויב בו ובן עולה לא יעננו׃
23 Nitawaponda adui zake mbele zake na kuwaangamiza watesi wake.
וכתותי מפניו צריו ומשנאיו אגוף׃
24 Upendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye, kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa.
ואמונתי וחסדי עמו ובשמי תרום קרנו׃
25 Nitauweka mkono wake juu ya bahari, mkono wake wa kuume juu ya mito.
ושמתי בים ידו ובנהרות ימינו׃
26 Naye ataniita kwa sauti, ‘Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, Mwamba na Mwokozi wangu.’
הוא יקראני אבי אתה אלי וצור ישועתי׃
27 Nitamteua pia awe mzaliwa wangu wa kwanza, aliyetukuka kuliko wafalme wote wa dunia.
אף אני בכור אתנהו עליון למלכי ארץ׃
28 Nitadumisha upendo wangu kwake milele, na agano langu naye litakuwa imara.
לעולם אשמור לו חסדי ובריתי נאמנת לו׃
29 Nitaudumisha uzao wake milele, kiti chake cha enzi kama mbingu zinavyodumu.
ושמתי לעד זרעו וכסאו כימי שמים׃
30 “Kama wanae wataacha amri yangu na wasifuate sheria zangu,
אם יעזבו בניו תורתי ובמשפטי לא ילכון׃
31 kama wakihalifu maagizo yangu na kutoshika amri zangu,
אם חקתי יחללו ומצותי לא ישמרו׃
32 nitaadhibu dhambi yao kwa fimbo, uovu wao kwa kuwapiga,
ופקדתי בשבט פשעם ובנגעים עונם׃
33 lakini sitauondoa upendo wangu kwake, wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe.
וחסדי לא אפיר מעמו ולא אשקר באמונתי׃
34 Mimi sitavunja agano langu wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka.
לא אחלל בריתי ומוצא שפתי לא אשנה׃
35 Mara moja na kwa milele, nimeapa kwa utakatifu wangu, nami sitamdanganya Daudi:
אחת נשבעתי בקדשי אם לדוד אכזב׃
36 kwamba uzao wake utaendelea milele, na kiti chake cha enzi kitadumu mbele zangu kama jua;
זרעו לעולם יהיה וכסאו כשמש נגדי׃
37 kitaimarishwa milele kama mwezi, shahidi mwaminifu angani.”
כירח יכון עולם ועד בשחק נאמן סלה׃
38 Lakini wewe umemkataa, umemdharau, umemkasirikia sana mpakwa mafuta wako.
ואתה זנחת ותמאס התעברת עם משיחך׃
39 Umelikana agano lako na mtumishi wako, na umeinajisi taji yake mavumbini.
נארתה ברית עבדך חללת לארץ נזרו׃
40 Umebomoa kuta zake zote, na ngome zake zote umezifanya kuwa magofu.
פרצת כל גדרתיו שמת מבצריו מחתה׃
41 Wote wapitao karibu wamemnyangʼanya mali zake; amekuwa dharau kwa jirani zake.
שסהו כל עברי דרך היה חרפה לשכניו׃
42 Umeutukuza mkono wa kuume wa adui zake, umewafanya watesi wake wote washangilie.
הרימות ימין צריו השמחת כל אויביו׃
43 Umegeuza makali ya upanga wake, na hukumpa msaada katika vita.
אף תשיב צור חרבו ולא הקימתו במלחמה׃
44 Umeikomesha fahari yake, na kukiangusha kiti chake cha enzi.
השבת מטהרו וכסאו לארץ מגרתה׃
45 Umezifupisha siku za ujana wake, umemfunika kwa vazi la aibu.
הקצרת ימי עלומיו העטית עליו בושה סלה׃
46 Hata lini, Ee Bwana? Utajificha milele? Ghadhabu yako itawaka kama moto hata lini?
עד מה יהוה תסתר לנצח תבער כמו אש חמתך׃
47 Kumbuka jinsi maisha yangu yanavyopita haraka. Ni kwa ubatili kiasi gani umemuumba mwanadamu!
זכר אני מה חלד על מה שוא בראת כל בני אדם׃
48 Ni mtu gani awezaye kuishi na asione kifo, au kujiokoa mwenyewe kutoka nguvu za kaburi? (Sheol h7585)
מי גבר יחיה ולא יראה מות ימלט נפשו מיד שאול סלה׃ (Sheol h7585)
49 Ee Bwana, uko wapi upendo wako mkuu wa mwanzoni, ambao katika uaminifu wako ulimwapia Daudi?
איה חסדיך הראשנים אדני נשבעת לדוד באמונתך׃
50 Bwana kumbuka jinsi mtumishi wako amesimangwa, jinsi ninavyovumilia moyoni mwangu dhihaka za mataifa yote,
זכר אדני חרפת עבדיך שאתי בחיקי כל רבים עמים׃
51 dhihaka ambazo kwazo adui zako wamenisimanga, Ee Bwana, ambazo kwazo wamesimanga kila hatua ya mpakwa mafuta wako.
אשר חרפו אויביך יהוה אשר חרפו עקבות משיחך׃
52 Msifuni Bwana milele!
ברוך יהוה לעולם אמן ואמן׃

< Zaburi 89 >