< Zaburi 88 >
1 Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi leanothi. Utenzi wa Hemani Mwezrahi. Ee Bwana, Mungu uniokoaye, nimelia mbele zako usiku na mchana.
[A Song. A Psalm by the sons of Korah. For the Chief Musician. To the tune of "The Suffering of Affliction." A contemplation by Heman, the Ezrahite.] Jehovah, the God of my salvation, I have cried day and night before you.
2 Maombi yangu yafike mbele zako, utegee kilio changu sikio lako.
Let my prayer enter into your presence. Turn your ear to my cry.
3 Kwa maana nafsi yangu imejaa taabu, na maisha yangu yanakaribia kaburi. (Sheol )
For my soul is full of troubles. My life draws near to Sheol. (Sheol )
4 Nimehesabiwa miongoni mwa wale waendao shimoni, niko kama mtu asiye na nguvu.
I am counted among those who go down into the pit. I am like a man who has no help,
5 Nimetengwa pamoja na wafu, kama waliochinjwa walalao kaburini, ambao huwakumbuki tena, ambao wamekatiliwa mbali na uangalizi wako.
set apart among the dead, like the slain who lie in the grave, whom you remember no more. They are cut off from your hand.
6 Umenitupa katika shimo lenye kina kirefu sana, katika vina vya giza nene.
You have laid me in the lowest pit, in the darkest depths.
7 Ghadhabu yako imekuwa nzito juu yangu, umenigharikisha kwa mawimbi yako yote.
Your wrath lies heavily on me. You have afflicted me with all your waves. (Selah)
8 Umenitenga na rafiki zangu wa karibu na kunifanya chukizo kwao. Nimezuiliwa, wala siwezi kutoroka;
You have taken my friends from me. You have made me an abomination to them. I am confined, and I can't escape.
9 nuru ya macho yangu imefifia kwa ajili ya huzuni. Ee Bwana, ninakuita kila siku, ninakunyooshea wewe mikono yangu.
My eyes are dim from grief. I have called on you daily, Jehovah. I have spread out my hands to you.
10 Je, wewe huwaonyesha wafu maajabu yako? Je, wale waliokufa huinuka na kukusifu?
Do you show wonders to the dead? Do the dead rise up and praise you? (Selah)
11 Je, upendo wako hutangazwa kaburini, uaminifu wako katika Uharibifu?
Is your loving kindness declared in the grave? Or your faithfulness in Destruction?
12 Je, maajabu yako hujulikana mahali pa giza, au matendo yako ya haki katika nchi ya usahaulifu?
Are your wonders made known in the dark? Or your righteousness in the land of forgetfulness?
13 Lakini ninakulilia wewe, Ee Bwana, unisaidie; asubuhi maombi yangu huja mbele zako.
But to you, Jehovah, I have cried. In the morning, my prayer comes before you.
14 Ee Bwana, kwa nini unanikataa na kunificha uso wako?
Jehovah, why do you reject my soul? Why do you hide your face from me?
15 Tangu ujana wangu nimeteseka, nikakaribia kifo; nimepatwa na hofu zako, nami nimekata tamaa.
I am afflicted and ready to die from my youth up. While I suffer your terrors, I am distracted.
16 Ghadhabu yako imepita juu yangu; hofu zako zimeniangamiza.
Your fierce wrath has gone over me. Your terrors have cut me off.
17 Mchana kutwa zinanizunguka kama mafuriko; zimenimeza kabisa.
They came around me like water all day long. They completely engulfed me.
18 Umeniondolea marafiki na wapendwa wangu; giza limekuwa ndilo rafiki yangu wa karibu kuliko wote.
You have put lover and friend far from me, and my friends into darkness.