< Zaburi 87 >
1 Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo. Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;
Mji aliouanzisha umesimama juu ya mlima mtakatifu;
2 Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo.
Yahwe anapenda zaidi malango ya Sayuni kuliko mahema yote ya Yakobo.
3 Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu:
Mambo matukufu yamesemwa kwako, mji wa Mungu. (Selah)
4 “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’”
Ninataja Rahabu na Babeli kwa wafuasi wangu. Tazama, Filisti, na Tiro, pamoja na Ethiopia nao watasema, 'Huyu alizaliwa humo.'”
5 Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.”
Itasemwa juu ya Sayuni, “Kila mmoja wa hawa alizaliwa katika yeye; na yeye Aliye Juu atamuimarisha.
6 Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.”
Yahwe anaandika katika kitabau cha sensa ya mataifa, “Huyu alizaliwa humo.” (Selah)
7 Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.”
Hivyo waimbaji na wachezaji kwa pamoja waseme, “chemchem zangu zimo kwako.”